Vijana wamsimamisha Kikwete Mwanjelwa; wazomea "fisadi fisadi" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wamsimamisha Kikwete Mwanjelwa; wazomea "fisadi fisadi"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gottee, Oct 10, 2008.

 1. Gottee

  Gottee Senior Member

  #1
  Oct 10, 2008
  Joined: Sep 7, 2008
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Habari za uhakika nilizozipata kutoka Mbeya zinasema Rais JK leo ameanza kuonja joto ya jiwe pale alipokuwa akipita maeneo ya Mwanjelwa. Inasemekana msafara wa Rais ulisimama na Rais akajitokeza kwa juu kuwasalimia wananchi. Mara alipomaliza kuwasalimia wananchi walianza kuzomea huku wakisema: 'Mafisadi, Mafisadi, Mafisadi!' Msafara ulipoanza kuondoka wananchi waliendelea kumsindikiza Rais na huku wakiendelea kuzomea neno 'Mafisadi' Yasemekana Rais aliambiwa kuwa anasubiriwa pia kule Uyole!

  Nawakilisha.
   
 2. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2008
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hali hii haishangazi. Maalim Seif kasema jana jambo la busara sana, "Namwonea huruma rafiki yangu, Rais Kikwete, nchi imevimba na maana yake ni kwamba Watanzania wamekata tamaa ya maisha kutokana na utawala mbovu wa Serikali yake, endapo atawashughulikia mafisadi kwa kuwachukulia hatua za kisheria, basi anaweza kurudisha ndoto za wananchi za kufaidika na rasilimali za nchi yao".
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Duh mkuu hii aibu tupu ndo maana alikuwa anagwaya kwenda kule ana taabu sana...bora asiongozane na Mwandosya maana navyo jua wananchi wa kule wataanza kumshangilia Mwandosya kama rais na kumfunika JK....ngoja tusubili news nyingine.
   
 4. M

  Mulokole Member

  #4
  Oct 10, 2008
  Joined: Aug 6, 2007
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mambo hayo. walifikiri bado tunaishi enzi za kudumisha fikra. inabidi sasa wakodi washangiliaji.
   
 5. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mkuu Gottee,

  Mimi nilisifikiri ulikuwepo kumbe ni habari zile zile za kusikia? Angalia isije ikawa kama ile statement ya Mtikila.

  Nijuavyo mimi JK atakuwa wilaya ya Mbeya tarehe 13 na leo inatakiwa awe Rungwe, kisha Kyela na Ileje. Labda kama wamebadilisha ratiba.
   
 6. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Gottee, pole sana kwa kusikia ila chanzo chako naona kina walakini, Karibu Mbeya Mkuu.
   
 7. Nungunungu

  Nungunungu JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2008
  Joined: Feb 13, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari hizi ni za uongo. Mimi nimeshuhudia msafara wa Rais na hakuzomewa! Hakuwa katika gari ya wazi bali gari alilokuwemo lilikuwa ikienda mwendo wa wastani na aliwasalimia wananchi akiwa ndani ya gari.

  Acheni siasa za majungu wazee. Hiki ndio wengine huwa wanakiita purely nonsense!

  NN.
   
 8. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2008
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  raisi amepokelewa vizuri tu, ila vijana pale mwanjelwa walikuwa wamelala barabarani wanasema mpaka awape maisha bora...
   
 9. Gottee

  Gottee Senior Member

  #9
  Oct 10, 2008
  Joined: Sep 7, 2008
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wewe UJUAVYO, huwezi kujua yote katika dunia hii MKUU adhawaizi unajipachika NGUVU za UMUNGU!!! Taarifa za uhakika JK yupo Mbeya tangu jana jioni! Amelala pale Mbeya Mjini na leo asubuhi ameelekea Rungwe (ndipo alipokutana na 'kikaango' kile) ambapo atalala huko na kesho kuelekea Kyela. Nadhani this time source wako hayuko SAHIHI. Habari za kuzomewa JK sina mashaka nazo kwa sababu mpasha habari wangu alikuwepo kwenye eneo la tukio na kwa taarifa yako kwa kutumia simu ya mkononi nimezisikia zile 'SHAMRASHAMRA'

  Kama una jamaa zako Mwanjelwa waulize, tukio hili halikufanyika chumbani, lakini kwa sasa HA HAA HABARI NDIYO MKUU!
   
 10. M

  Masatu JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jamani haya mambo ya "habari za uhakika" sasa yanatia shaka...
   
 11. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2008
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,213
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280
  Ndugu Gottee,
  Pamoja na kuokuomba utupe habari za uhakika kuhusu ziara ya raisi, sitashangaa sana iwapo JK atazomewa kule Mbeya, kwa sababu ndio kwanza anaenda kuwashukuru wananchi wa kule tangu wamchague mwaka 2005! What a shame!
  Lakini pia kuna mawaziri waliozomewa mwaka jana wakati wa 'kutetea' bajeti ya Meghji, na wengine walimwagiwa mchanga na kutukanwa!

  Naamimi mheshimiwa Mushobozi yuko Mbeya kwenye coverage ya ziara ya raisi, atatupatia nyeti zote.
   
 12. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #12
  Oct 10, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,848
  Likes Received: 2,423
  Trophy Points: 280
  ..du watalala mpaka basi..wajameni si ameshasemaga maisha bora hayanyeshi kama mvua...kabadilika...,na kule iringa akawaambia hatembei na furushi la pesa...au hawa nao walikuwa wanatafuta kupigwa kijembe??
   
 13. Gottee

  Gottee Senior Member

  #13
  Oct 10, 2008
  Joined: Sep 7, 2008
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wewe ndio una siasa za MAJUNGU! Nani kasema JK alikuwa kwenye gari la wazi? Au hujui hilo gari anaweza akatokea kwa juu. UNATUAMBIA umeshuhudia msafara wa Rais. Ukiwa WAPI? Tunakwambia alipozomewa ni Mwanjelwa sasa kama wewe ulikuwa Uzunguni au Soweto au Mama John au mahali popote ambako hakuzomewa UNGEYAJUAJE hayo au unataka kutuambia ULIKUWA umekaa kwenye kiti cha jirani na JK? Najua yatasemwa mengi SITASHANGAA wapambe wakisema aliyezomewa ni 'Bangusilo' Mwakipesile! Mbeya ni pagumu Mkuu!
   
 14. Gottee

  Gottee Senior Member

  #14
  Oct 10, 2008
  Joined: Sep 7, 2008
  Messages: 174
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  RFA wanatangaza sasa hivi katika taarifa ya habari kwamba Rais Kikwete amewaambia vijana wateue wawakilishi wao na amekubali kukutana nao na wameeleza hayo na ufisadi na kulala chini. Haya mliozoea kusikiliza habari za 'kweli', subirini redio zenu na magazeti yenu kutoka ile familia ya TBC na Uhuru na RAI (Rostam Aziz International)
   
 15. PgSoft2008

  PgSoft2008 JF-Expert Member

  #15
  Oct 10, 2008
  Joined: May 15, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  hapo mkuu umenena
   
 16. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  RAI (Rostam Aziz International)[/QUOTE] imekaa vizuri
   
 17. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2008
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa atafakari vema kisha achukue hatua.Prevention is better than cure
   
 18. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2008
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Kwa mujibu wa chanzo cha habari toka mmoja ya vyuo vikuu Mbeya anakiri kutokea hitilafu hiyo iliyopelekea kumzomea JK lakini muungwana aliimudu hali hiyo kwa kutoa fursa kwa vijana hao kueleza yaliyomo rohoni mwao na kwamba yeye yuko pale kuwasikiliza na kufanyia kazi maoni yao kwa dhati hiyo ni pamoja na yeye kuwaeleza maoni yale aliyo nayo katika sakata zima la ufisadi na maisha bora. Bado yuko ktk hali safi na mood ya kuendelea na ziara yake.

  Tutaendelea kuwapatia kinachoendelea wakuu.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,412
  Likes Received: 81,451
  Trophy Points: 280
  Anastahili kuzomewa, miaka mitatu madarakani ameenda US mara chungu nzima ameenda UK mara chungu nzima lakini hii ndiyo mara ya kwnza kufika Mbeya. Halafu ahadi zake zote wakati wa kampeni hakuna hata moja aliyoitekeleza.
   
 20. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #20
  Oct 10, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Wewe mwaga hapa,kuna watu ambao wanataka mambo yaende wanavyotaka wao.Ingekua hivyo dunia ingetawaliwa na Adolf Hitler kirahisi sana.

  Nadhani mkuna watu walijiandaa kusikia JK kashangiliwa, lakini JK bado kaendelea kubugizwa magoli na srikali yake.

  Pia nimegundua hapa kuna watu wanataka kulinda status quo ya chama na hawataki kusikia kuna tofauti za kisiasa ndani ya CCM huko Mbeya.Watakuja kukupinga kwa maneno makali mkuu ila usijali tumewazoea
   
Loading...