Vijana wamiminika Tanga kusaka ajira kwenye bomba la mafuta

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,412
2,000
Wimbi la vijana wanaokwenda eneo litakapoishia bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda kwa ajili ya kutafuta vibarua linazidi kuongezeka.

Hali hiyo imeulazimu uongozi wa mtaa wa Putini, Kata ya Chongoleani jijini Tanga kubeba majukumu ya kuwahifadhi.

Kufuatia wimbi hilo, Serikali za mitaa ya Putini na Chongoleani, zimeomba vijana walioko mikoa mbalimbali nchini kutokwenda Tanga kwa sababu hakuna kinachoendelea.

Hivi karibuni, Rais John Magufuli alisaini makubaliano na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kwa ajili ya ujenzi wa bomba hilo kutoka Hoima, Uganda.

Wakizungumza na Mwananchi, mwenyekiti wa mtaa wa Putini, Abdallah Kanuni na wa Chongoleani, Mbwana Dondo walisema tangu mawaziri wa Uganda na Tanzania walipotia saini ya makubaliano ya mwisho ya mradi huo, wimbi la vijana kwenda eneo hilo lililopo.

"Hadi jana vijana zaidi ya 300 kutoka mikoa mbalimbali wamekuja hapa wakidai kuwa wamesikia kuna vibarua vya ujenzi wa bomba la mafuta, wengine hawana hata nauli za kurejea kwao, tunalazimika kuwahifadhi na wengine tunawachangia nauli," amesema Kanuni.

Mwenyekiti huyo wa Putini aliviomba vyombo vinavyohusika na mradi wa bomba la mafuta kuhakikisha vinatoa taarifa za uhakika kwenye vyombo vya habari juu ya lini ujenzi utaanza na ajira zitatolewa kwa utaratibu gani ili wananchi nchini kote wawe na taarifa sahihi.

"Hata jana jioni mimi na mwenyekiti mwenzangu wa Chongoleani tulipokea vijana waliojitambulisha kwamba wanatokea Mwanza na wamekuja kutafuta kibarua cha kujenga bomba la mafuta lakini wameshangaa kuona hakuna chochote,"amesema Kanuni.

Dondo amesema yeye kama kiongozi wa eneo hilo anaamini lazima kwanza uanze mchakato wa kulipa fidia kwa waliopisha ndipo maandalizi mengine yatafuata na mambo hayo yatafanyika kwa uwazi.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa aliwataka wananchi kutofuata taarifa za mitaani juu ya mradi huo wa bomba la mafuta na kwamba ujenzi utakapoanza, zitatolewa taarifa kuhusu aina ya vibarua vitatokavyotolewa na sifa za watakaotakiwa kuajiriwa.

"Nikiwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Tanga, nasema si busara vijana kumiminika Chongoleani na Putini kwa kisingizio cha kutafuta vibarua,"amesema Mwilapwa.

Hata hivyo alisema Serikali imeweka utaratibu wa kuwatambua wageni wanaoingia katika eneo hilo ili kudhibiti uhalifu ambao unaweza kujitokeza.

Chanzo: Mwananchi
 

majoto

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
2,040
2,000
Vijana wenyewe wa Tanga wanashangaa shangaa tu vijiweni, wa mbali watachukuwa ajira
 

nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
8,067
2,000
Mi ntalisubiria njiani likifika mpakani mwa mkoa wangu hapohapo nazama kuomba ajira
 

jozzeva

JF-Expert Member
Oct 27, 2012
2,201
2,000
Tunawajua vijana wa Tanga mlivyo wavivu... mmebwetekaaaa... mmeridhika na maisha ya shikamoo..... endeleeni kulala na kukaa vibarazani kunywa kahawa na maneno mengiiii
Kwani kuna tatizo gani kukaa kibarazani kunywa kahawa?au we ulitaka wakae juu ya mti kama nyani?kwani kuna tatizo kuongea maneno mengi?ungeumbwa bubu ungeanza kumkufuru mungu.
 

majoto

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
2,040
2,000
Kwani kuna tatizo gani kukaa kibarazani kunywa kahawa?au we ulitaka wakae juu ya mti kama nyani?kwani kuna tatizo kuongea maneno mengi?ungeumbwa bubu ungeanza kumkufuru mungu.
Tatizo ni uvivu mlio nao.
 

weed

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
2,111
2,000
Hao wana matatizo kwakweli.. hawan hata nauli za kurudi?
 

APEFACE

JF-Expert Member
Oct 1, 2016
3,438
2,000
ngoja nami nikope nauli niende huko....mana hali si shwari..............
 

Mookiesbad98

JF-Expert Member
Feb 1, 2015
1,671
2,000
Hizi ajira zimeshaanza kutangazwa na kampuni ya TOTAL na kuna ki recruitment cha wakenya kipo mikocheni nacho kimepata tenda ya kutangaza ajira
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom