Vijana waliopo Tanzania wanashangilia ubabe wa Putin

MANKA MUSA

JF-Expert Member
Jul 9, 2014
922
1,093
Kijana mmeba box nikipata nafasi ya kupumzika huwa napitia sana mitandaoni si unajua huku hauli bila kazi, kilichonishangaza ni update za Vijana waliopo Tanzania wakishangilia ubabe wa Putin na story kuhusu uharibifu wa Putini. Nikajiuliza Vijana hawa wanafahamu balaa lililopo mbele Yao hawa?

sasa hivi majuzi hapa Dubai nimeshuhudia bei kali ya mafuta na foleni ndefu ya magari wakigombania kujaza mafuta kabla ya tarehe moja Julai nikajiuliza hapo nyumbani Bongo hali itakuwaje…? Kisha nikawakumbuka wale Vijana wanaomshangilia Putin kwenye mitandao.

Wakati Nikiwa na Peruzi nikakutana na Habari ya anguko la Uchumi wa nchi ya Sri Lanka shule zimefungwa kwa muda wa wiki ya tatu mfululizo, kutokana na uhaba wa mafuta ya kuendeshea magari ya kusafirisha walimu na wanafunzi.

Waziri wa Elimu amewataka walimu na wanafunzi ambao wameathirika na tatizo hilo kutumia mafunzo kwa njia ya mtandao hadi pale tatizo hilo litakapokuwa limepatiwa ufumbuzi.

Waziri wa Nishati wa Sri Lanka, Kanchana Wijesekera amesema, shehena ya kwanza ya mafuta ya tani elfu 40 inatarajiwa kuwasili nchini humo tarehe 22 mwezi huu.

Serikali ya Sri Lanka inahitaji dola milioni 587 kwa ajili ya kununulia mafuta ambapo nchi hiyo inadaiwa dola milioni 800 na wasambazaji wa mafuta kutokana na deni la kuagiza nishati hiyo nchini humo. Vijana wa Sri Lanka hawawezi kumsifia Putin kwa madhara ya vita hivi wameona matokeo yake.

Sisi hapa nyumbani tunaweza kubeza hizi bilioni 100 za Ruzuku ya mafuta kwa kuwa tumejaliwa midomo ya kuongea tungetembea kujionea Marekani wananchi wake wanavyotaabika, majuzi pale Uingereza kwa Malikia watu wakiaandamana juu ya hali ngumu ya maisha.

Hapa JF kuna Uzi zinazomsifia Putin na kuponda Ruzuku ya bilioni 100 inayotolewa na serikali kunusuru kupanda kwa bei ya mafuta nchi.
 
Unajua kuna watu kwa makusudi mmeamua kuwa hamna akili
Vijana humu kumshabikia au kutomshabikia Putin ndio itafanya Vita viishe? Dunia nzima kupitia umoja wa mataifa wamemlaaani na kumuwekea vikwazo Putin, Vita imeisha??
Mnataka kutoa lawama za kipumbavu.
 
Sasa aliyepandisha mafuta ni nani? Putin au Nato?
1. Aliyeweka sanction lukuki ni nani? Putin au Nato?
2. Aliyezuia mafuta ya ya Urusi kwa nchi za Afrika zisinunue ni Putin au Nato?
3. Aliyekiuka mikataba ambayo ilimzuia Urusi asiweke kambi za kijeshi Cuba ili wasizungukane kwa silaha za maangamizi ni nani ni Putin au Nato?
Tumia akili zote kulieleza jambo hili, usitumie moyo unaosukuma damu tu

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Kijana mmeba box nikipata nafasi ya kupumzika huwa napitia sana mitandaoni si unajua huku hauli bila kazi, kilichonishangaza ni update za Vijana waliopo Tanzania wakishangilia ubabe wa Putin na story kuhusu uharibifu wa Putini. Nikajiuliza Vijana hawa wanafahamu balaa lililopo mbele Yao hawa?

sasa hivi majuzi hapa Dubai nimeshuhudia bei kali ya mafuta na foleni ndefu ya magari wakigombania kujaza mafuta kabla ya tarehe moja Julai nikajiuliza hapo nyumbani Bongo hali itakuwaje…? Kisha nikawakumbuka wale Vijana wanaomshangilia Putin kwenye mitandao.

Wakati Nikiwa na Peruzi nikakutana na Habari ya anguko la Uchumi wa nchi ya Sri Lanka shule zimefungwa kwa muda wa wiki ya tatu mfululizo, kutokana na uhaba wa mafuta ya kuendeshea magari ya kusafirisha walimu na wanafunzi.

Waziri wa Elimu amewataka walimu na wanafunzi ambao wameathirika na tatizo hilo kutumia mafunzo kwa njia ya mtandao hadi pale tatizo hilo litakapokuwa limepatiwa ufumbuzi.

Waziri wa Nishati wa Sri Lanka, Kanchana Wijesekera amesema, shehena ya kwanza ya mafuta ya tani elfu 40 inatarajiwa kuwasili nchini humo tarehe 22 mwezi huu.

Serikali ya Sri Lanka inahitaji dola milioni 587 kwa ajili ya kununulia mafuta ambapo nchi hiyo inadaiwa dola milioni 800 na wasambazaji wa mafuta kutokana na deni la kuagiza nishati hiyo nchini humo. Vijana wa Sri Lanka hawawezi kumsifia Putin kwa madhara ya vita hivi wameona matokeo yake.

Sisi hapa nyumbani tunaweza kubeza hizi bilioni 100 za Ruzuku ya mafuta kwa kuwa tumejaliwa midomo ya kuongea tungetembea kujionea Marekani wananchi wake wanavyotaabika, majuzi pale Uingereza kwa Malikia watu wakiaandamana juu ya hali ngumu ya maisha.

Hapa JF kuna Uzi zinazomsifia Putin na kuponda Ruzuku ya bilioni 100 inayotolewa na serikali kunusuru kupanda kwa bei ya mafuta nchi.
🤣🤣🤣 Mpaka vita kuisha tutaona na kusikia mengi sana, kwa hiyo huyu anamaana sisi vijana pro-Russia ni vijana wateule na tukimlaani Putin atatusikia ataacha kumshikisha adabu mdogo ake mwenye dharau eti?

Acha ujinga, vita ameipika US then anampaka tope mwenzie na kama we have to suffer kwa maamuzi ya Putin ili kulinda nchi yake, so be it maana tutaumia zaidi kama Urusi itaanguka mazima akabaki mbwa US
 
Ingekuwa wewe ungefanyaje? Adui yako mkuu anakuzunguka pande zote uwe katikati yake ? Hebu nenda kaweke nukes cuba kama USA atakuchekea vita ya Russia ni halali kabisa anatetea survival ya taifa lake.
Kwani Ukraine wameweka nukes?
 
Sasa aliyepandisha mafuta ni nani? Putin au Nato?
1. Aliyweka sanction lukuki ni nani? Puti au Nato?
2. Aliyezuia mafuta ya ya Urusi kwa nchi za Afrika zisinunue ni Putin au Nato?
3. Aliyekiuka mikataba ambayo ilimzuia Urusi asiweke kambi za kijeshi Cuba ili wasizungukane kwa silaha za maangamizi ni nani ni Putin au Nato?
Tumia akili zote kulieleza jambo hili, usitumie moyo unaosukuma damu tu

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app1. NATO
Putin. Asingevamia mafuta yasingepanda.
1. NATO
2. Hakuna aliyezuia
3. Tuonyeshe huo mkataba.
 
Mkuu mtoa hoja hii usikwazike sana na comments za dot.com ,wao vita wanaona kama ni mchezo wa draft, vita hii inatuathiri zaidi sisi kuliko Ukraine na Russia, na moto zaidi unakuja baada ya hii vita kuisha, mtoa hoja hii tafuta TV ba angalia game ya soccer la wanawake Africa pale Morocco 🇲🇦, usiku huu ni wenyeji vs Uganda 🇺🇬, bado 1-1,Tanzania tunacheza kesho vs ushelisheli!
 
Back
Top Bottom