Vijana waliokuwa wanatorosha mabinti miaka ya zamani wana afadhali kuliko wa sasa

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
Nakumbuka zamani nikiwa mdogo miaka ya 90 mwishoni na 2000s miaka ya mwanzoni nlikuwa naskia sana binti wa fulani katoroshwa na kijana flani, House girl wa nyumba flani katoroshwa, dada yake flani katoroshwa, n.k. hapo ni kwamba wanaenda kuanza maisha kama mme na mke, hadi mje kuwaona tena basi huenda wana mtoto tayari, sio kama utoroshaji ulizozoeleka siku hizi binti anatoroshwa usiku anarudishwa asubuhi, kumtorosha binti lengo lilikuwa ni kuanza nae maisha na sio kujamiana tu.

Kiukweli lilikuwa ni jambo ambalo lilikuwa ni zito sana na kuonekana ni kosa kubwa, lakini nikianza kulinganisha na hali ya sasa, naona kabisa hio tabia ya zamani ilikuwa na unafuu.

Zamani miaka hio mpaka mtu inafikia steji anatoroshwa ilikuwa wameshajipanga mithiri ya ndege ambao wameshaandaa kiota tayari kwa kuisbi pamoja na kulea familia, bila kujali hali ya uchumi.

Nakumbuka wengi waliokuwa wametoroshwa, wakija kujulikana basi tayari wana watoto na wanaishi na huyo mtoroshaji ambae kawa baba,

Kwa upande wa mahusiano ya siku hizi mambo yamekuwa tofauti sana, mahusiano yamekuwa ni shake well before use na wengi wanaishia kuwa na mahusiano ya muda mfupi.

Vijana wa kiume wamekuwa waoga sana wa majukumu huku wakiwa na tamaa ya hali ya juu ya kuwa na mahusiano ya kutoa tamaa za kimwili kuliko kuwa na mahusiano ya kujenga familia.

Kiukweli naona ni heri system ya zamani japo ilikuwa ni kosa kubwa na la kushushia heshima familia flani kumtorosha binti bila kulipia mahari, lakini ilikuwa ni dhahiri kwamba vijana wamepandana na huko walikokwenda wana malengo tayari.
 
Back
Top Bottom