Vijana walio wengi kushindwa maisha ya kujitegemea tatizo ni nini?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Kwa maisha ya hivi sasa ni jambo la kawaida kukutana kijana miaka 30 hadi 40 bado yupo nyumbani kwao maisha ya kujitegemea wengi wanashidwa bado wanategemea wazazi.

Wengine wanaenda mbali zaidi hadi swala la kuoa imefika hatua anaoa akiwa mazingira ya kinyumbani na mkewe anaishi nae kwao akiwa anategemea bado wazazi.

Wengine maisha yao yanaishia kwa shemeji mahala alipolewa dada yake na yeye anaenda kuanzisha maisha pale pale akimtegemea shemeji.

Je, tatizo ni nini vijana wanashidwa kujitegemea?
 
Tatizo Ni wazazi wetu, MZAZI unatakiwa kuwa na misimamo kwa watoto, lazima umwambie mtoto wako ukifika umri wa miak 25 au 26 Anza maisha ya kujitegemea hapa nyumban sikutaki kapange. Mtoto lazima apambane kuanzia miak 22 kujiajili mwenyewe.

Utakuta wazazi wamejenga nyumba mjini wakajenga nyumba nyingine kijijini. Wazazi hawa hawa wanaamua kuondoka mjini kuamia kijijini halafu wanawaambia watoto tunawaachia hii nyumba ya mjini mkae. Watoto hawa hawa wanaumri wa miaka 28,29,30.

Kama Ni mtoto wa kike atazalishwa mtoto wa kwanza mpk 2 mle mle kwenye nyumba ya wazazi wake. Mtoto wa kiume naye atazalisha mlemle kwenye nyumba ya wazazi.

Wanawachukua watoto wao wanawapeleka wakaishi na babu na bibi. Kibaya zaidi bili ya maji na umeme ikifika wanawapelekea wazazi wao huko kijijini wawasaidie kulipa.

Muda wa shule ukifika Babu na bibi wanaangaika kutafuta pesa za kuwapeleka wajukuu shuleni wenye watoto hawana ela.

Unakuwa na mtoto mpaka anafika umri wa miaka 35 hajawahi kupanga kulipa kodi. Hawezi kuoa wala kuhudumia Family.

MZAZI inabidi uwafukuze watoto wenyewe umri 28 na kuendelea ni bora utafute wapangaji wapange.

Watoto kama hawa wazazi wote wakifa ndo kwanza wanauza nyumba.
 
Tatizo Ni wazazi wetu, MZAZI unatakiwa kuwa na misimamo kwa watoto, lazima umwambie mtoto wako ukifika umri wa miak 25 au 26 Anza maisha ya kujitegemea hapa nyumban sikutaki kapange. Mtoto lazima apambane kuanzia miak 22 kujiajili mwenyewe.

Utakuta wazazi wamejenga nyumba mjini wakajenga nyumba nyingine kijijini. Wazazi hawa hawa wanaamua kuondoka mjini kuamia kijijini halafu wanawaambia watoto tunawaachia hii nyumba ya mjini mkae. Watoto hawa hawa wanaumri wa miaka 28,29,30.

Kama Ni mtoto wa kike atazalishwa mtoto wa kwanza mpk 2 mle mle kwenye nyumba ya wazazi wake. Mtoto wa kiume naye atazalisha mlemle kwenye nyumba ya wazazi.

Wanawachukua watoto wao wanawapeleka wakaishi na babu na bibi. Kibaya zaidi bili ya maji na umeme ikifika wanawapelekea wazazi wao huko kijijini wawasaidie kulipa.

Muda wa shule ukifika Babu na bibi wanaangaika kutafuta pesa za kuwapeleka wajukuu shuleni wenye watoto hawana ela.

Unakuwa na mtoto mpaka anafika umri wa miaka 35 hajawahi kupanga kulipa kodi. Hawezi kuoa wala kuhudumia Family.

MZAZI inabidi uwafukuze watoto wenyewe umri 28 na kuendelea ni bora utafute wapangaji wapange.

Watoto kama hawa wazazi wote wakifa ndo kwanza wanauza nyumba.
Wazazi wanaogopa, unaweza kumfukuza mtoto ili ajaribu maisha yake, badala yake wanaona mtoto anaweza kwenda kujihusisha na magenge ya kihuni, umalaya nk.

Muhimu ni kuwaandalia watoto mazingira, misingi bora, tatizo linalotukabili ni kwamba Familia zetu nyingi ni duni
 
Tatizo la kwanza ni umasikini.
Tatizo la pili ni jamii.
Tatizo la tatu ni education system.
Tatizo la la nne ni wewe.
Tatizo la mwisho ni serikali.

Wazazi wamekuzaa wewe wao wapo kwenye lindi la umasikini na wao wanakutegemea wewe.
Wanategemea wakusomeshe wewe ili uje kuwasaidia baadae.
Kuwasaidia ni wewe upate ajira ili uwasaidie kuondoa umasikini.
Hilo ndo wazo pekee lililopo vichwani mwao.

Wazazi wako wanafanya kila njia na nguvu zote.
Wewe mtoto unapelekwa shule unaanza kusoma std1 mpaka std7.
Hapo ukifeli ndio basi hautoweza kujitegemea tena ukichangia wazazi wako ni masikini.
Kwa asilimia 70 tegemea ufike 50yrs hapo kwenu.

Std7 mpaka form4.
Hapo ukifeli ndio basi tena hutoweza kujitegemea ukichangia kwenu ni masikini.
Kwa 70% tegemea ufike 50 hapohapo ulipo.

Let say umemaliza chuo.
Hapo utafurahi kwamba umemaliza chuo hivyo umasikini unauaga.

Bad news ni kwamba education system kwa asilimia 89% ilikufundisha kuajiriwa considering wazazi wako na jamii nzima huo ndio mtazamo wao.

Then unaambiwa ajira hakuna nenda kajiajiri.
Utaanzia wapi wakati wazazi, jamii na education system pia ilikufundisha kuajiriwa ndio msingi wa elimu ili uondoe umasikini.
Na sio wewe utumie elimu uliyonayo kusaidia jamii nzima.

Then unarudi nyumbani ulipotoka kwa wazazi wako ambao ni masikini na kusubiria ajira.
Then miaka inapita bila ajira ambapo muda unapotea then unakuta mtu ana40 as you said anakaaa na kuzaliana kwa wazazi wake.

Hapo kinachofuata ni kuendeleza cycle ya umasikini na hiyo usipokuwa makini vizazi vyako vyote vinakuwa masikini.
Kwani babu wa babu yako wa babu yake alikuwa ni tajiri?

Umeshajiuliza watoto wamatajiri wakimaliza kusoma wanaenda wapi?

Pia cha kushangaza baada ya yote hayo serikali imeshindwa hata kubadirisha education system ili badala ya kutengeneza wakariri ili wapate ajira na sio watu watakao kuja kutengeneza ajira nyingi zaidi iwezekanavyo.
Ili wengine wasikose ajira wakishindwa kuanzisha ajira pia wale waliofeli wapate ajira.

education system itengeneze watu wanaojitambua na kujielewa na kujua wanataka nini pia makusudio yao ya kuishi.
Kama ingekuwa hivi basi tusingekuwa hapa.

Kwanini mpaka leo serikali hawajabadirisha hiyo education system?
sababu hata wao ni za la hiyo education system.


Hii ingeondoa.
Umasikini na ujinga wa jamii kwamba elimu ni kupata ajira tu.
then yote yasingetokea ya mtu mwenye 30 kukaa na wazazi.

Chanzo kikubwa ni mfumo mbovu wa elimu.
 
Wakuu, heshima kwenu.

Tatizo la vijana wengi kukaa nyumbani kwa wazazi muda mrefu bila kujishughulisha kijana apate maendeleo ni mtazamo mgando kwamba kwa kuwa amesoma ni lazima itatokea siku ataajiriwa na kupata mshahara mnono. Wazazi wao pia huamini kuwa wamesomesha mwanao wakitarajia ataajiriwa na kulipwa hela ndefu.

Sasa kama wazazi wenyewe hawajawahi kuanzisha shughuli binafsi za kujipatia kipato maishani,walipata bahati wakaajiriwa,hawaoni mantiki kijana wao kuhangaika kuumiza kichwa wakati wao ni wasomi wanapata mshahara kiulaini na pensheni ya uzeeni watapata. Shule na vyuo vikuu vipo, wahitimu wanajivunia vyeti na shahada za kuajiriwa tu.

Hakuna mwanafunzi anayesoma chuo kikuu mwenye maono ya kujiajiri,wengi hutegemea kuajiriwa tu,hawathubutu kuanzisha mradi wao binafsi wa kupata hata shilingi moja. Mtazamo mgando juu ya elimu hufanya vijana wakae muda mrefu bila shughuli maalumu ya kufanya kupata hela wakisubiria kuajiriwa.
 
Hiii mada nzito sana lakini naomba niseme.

Tatizo la kwanza Ni la kijana mwenyewe yaani ameshidwa kutengeneza mfumo wa maisha yake ya badae akitegemea kuajiriwa hivyo jinsi swala la ajira linavyozidi kuchukua muda mrefu na ndio jinsi kijana anavyozidi kukaa nyumbani.

Tatizo la pili ni umasikini unakuta mtu anatamani apate hela ya kufungua mradi wa biashara lakini anaukosa mtaji.

Tatizo la tatu ni wazazi yaani kuna wazazi wanashidwa kutengeneza mazingira kijana wao kujitegemea hivyo hujikuta anaishia kuwa tegemezi.
 
Kwa maisha ya hivi sasa ni jambo la kawaida kukutana kijana miaka 30 hadi 40 bado yupo nyumbani kwao maisha ya kujitegemea wengi wanashidwa bado wanategemea wazazi

Wengine wanaenda mbali zaidi hadi swala la kuoa imefika hatua anaoa akiwa mazingira ya kinyumbani na mkewe anaishi nae kwao akiwa anategemea bado wazazi

Wengine maisha yao yanaishia kwa shemeji mahala alipolewa dada yake na yeye anaenda kuanzisha maisha pale pale akimtegemea shemeji

Je tatizo ni nini vijana wanashidwa kujitegemea
Vijana wa Tanzania wengi nu kama Mabolizozo.

Wanajiita wanyonge
 
Hapo tatizo sio vijana tatizo wazazi hawaandalii watoto mazingira ya kujitegemea.

Kama mzazi hujamuandaa mwanao kujiajijiri au kuntafutia connection za ajira asipoondoka hapo kwako usilaumu mtu.

Hii miaka ya 2020's tulipofika hali ni mbaya kwa kweli kama umechelewa hadi leo hujaanza harakati basi kazi ipo so wazazi tupambane watoto wetu waje kula bata mana tumefika pahala mwenye nacho anaongezewa asie nacho anaporwa watu wanapambana ila vikwazo vingi sio kwamba wamebweteka.

Mimi siamini kama kuna mtu anapenda kukaa kwao mpaka anafika miaka 30 lazma kuna pahala mtu atakua kakwama so tukibahatika kutoboa tusione wenzetu wazembe.
 
Back
Top Bottom