Vijana wadogo mnaopata ajira/pesa na kuanza maisha huru mbali na wazazi, pombe/ulevi, sio starehe pekee duniani

CarloJesus

JF-Expert Member
Nov 5, 2019
431
1,000
Naandika kwa masikitiko, imejengeka namna hii, kuwa ili tuwafurahishe watu ama watu/mtu afurahi ni lazima uwepo ulevi fulani.

Viko vilevi vingi, wengine shisha, wengine kungu, wengine madawa, wengine bangi/jani nk. Bahati mbaya hili limekuwa kama fashion, ambao hawakuwa walevi wengi wameingia kwa mkumbo.

Haya yameingia katika akili ya mtu kutoka ama, katika familia, jamii inayotuzunguka hata vitu kama picha na movies ambayo pombe inasifiwa sana bila nguvu hiyo hiyo kutumika kuonyesha madhara yake, humu pia kuna uzi wa walevi.

Ieleweke kuwa siongei ukamilifu wa maadili ya kidini au miiko fulani, hayo siwezi kuyagusia kwa sababu kila mtu kafungwa kwa imani yake, na bahati mbaya imani si rahisi kuhoji.

Naongea haya baada ya kuona rafiki yangu ambaye tayari alikuwa na future nzuri, alikuwa na ajira yake, lakini kwa ajili ya mkumbo mambo yote yameharibika.

Amefika hatua mbaya, alitemwa kazini kwa sababu ya pombe, udhuru ulizidi ikafika hatua akawa anaenda ama anaamka nazo kazini.

Navyoongea yuko kijijini anakunywa gongo hana mbele wala nyuma, amekuwa kama chizi, zaidi alichobaki nacho ni Kiingereza tu.

Mimi nakunywa pombe, lakini si tegemezi wa pombe katika furaha yangu.

Vijana wadogo mnaopata ajira na kuanza maisha ya uhuru mbali na wazazi, pombe/ulevi si starehe pekee ya kukupa furaha.
 

Puyet Babel

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
3,674
2,000
kijana kama hunwyi pombe utaishia kuwa mlevi wa mademu na mwisho wake kupata ukimwi na kufa!
madhara ya pombe ni nafuu kuliko starehe hizo zingine, basi tu hyo jamaa yako hana kichwa ya pombe

sikiliza wewe, sisi ndio wataalamu
tunakunywa pombe tangu tumepata kazi na maisha yanaenda poa hapa jijini
 

chigaile

Senior Member
Mar 21, 2017
150
250
Ni kweli,mbaya zaid apate kazi/ajira mbali na nyumbani anakua na uhuru wa kupitiliza na hakuna anayemsikiliza kwa ushauri
 

CarloJesus

JF-Expert Member
Nov 5, 2019
431
1,000
kijana kama hunwyi pombe utaishia kuwa mlevi wa mademu na mwisho wake kupata ukimwi na kufa!
madhara ya pombe ni nafuu kuliko starehe hizo zingine, basi tu hyo jamaa yako hana kichwa ya pombe

sikiliza wewe, sisi ndio wataalamu
tunakunywa pombe tangu tumepata kazi na maisha yanaenda poa hapa jijini
Upotoshaji huu umekua wa siku nyingi,nakunywa pombe pia,pombe imekua catalyst wa tabia nyingine mbaya Kama uchafu na uasherati

Achilia mbali kuwa baadae mtu mlevi huonekana irresponsible kuanzisha familia na yeyote Kama kupata mchumba vile,baadae huishi maisha ya kujikataa Kama ngono zembe...na dalili nyingine ni kusifia upuuzi huu

Lakini pia mtu huangukia katika ubnafsi mkubwa,akasahau mahitaji ya familia yake,lakini pia kusaidia wanaomzunguka ambao anabanwa na wajibu huo Kama mwanajamii...si kwa pesa tuu,lakini hata mfano mwema wa maisha yake

Baadae huwa hamsemi majuto yake,Nani asiejua kuwa ,wafanyakazi walioajiriwa,sio waliojiajiri,wengi wao asilimia kubwa ya mshahara Mwisho wa mwezi huishia kwenye madeni ya pombe,chanzo wengi kulaumu mshahara haitoshi?(sio wote lakini ni walevi)
 

CarloJesus

JF-Expert Member
Nov 5, 2019
431
1,000
Ni kweli,mbaya zaid apate kazi/ajira mbali na nyumbani anakua na uhuru wa kupitiliza na hakuna anayemsikiliza kwa ushauri
Ni hatari...na wengi huwa wanaanza kwa kuiga Kwanza...ni vema tukatumia nguvu ile ile kutangaza madhara,Kama jinsi yinavyotangaza raha zake
 

Eyce

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
3,141
2,000
Daniel Agger,

Kwa nini watu mnaishi kwa misconceptions.

Ni nani alikuambia kuna starehe ya lazma katika dunia hii ???.....

Mbaya zaidi ni lazma uchague pombe au ngono !!!!...

Haya bhana ndio exposure yako ilivyo, hata mimi kuna mahali imeishia. Hakuna haja ya kushangaana just fanya kinachokupa furaha while minding your own space
 

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
7,192
2,000
Eyce

Sitetei ulevi kama Daniel Agger ila napishana na wewe kuhusu ‘starehe ya lazima’ kama ilivyo ‘hobbies’ zingine ni muhimu kuwa nayo moja, ngono sio starehe kwa vile hata wadudu na viumbe wengine wote kwa jinsi zao hufanya ngono.... ila katika ‘options’ zako hapo juu kama ni starehe basi madhara ya ngono ni ghali zaidi.
 

Eyce

JF-Expert Member
Mar 16, 2016
3,141
2,000
Eyce

Sitetei ulevi kama Daniel Agger ila napishana na wewe kuhusu ‘starehe ya lazima’ kama ilivyo ‘hobbies’ zingine ni muhimu kuwa nayo moja, ngono sio starehe kwa vile hata wadudu na viumbe wengine wote kwa jinsi zao hufanya ngono.... ila katika ‘options’ zako hapo juu kama ni starehe basi madhara ya ngono ni ghali zaidi.

Nilichokuwa nakimaanisha ni kuwa si lazma kila mtu apende kitu common, watu tupo tofauti na tuna njia tofauti ya kupata furaha na fullfillment na hapo ndipo concept ya "starehe ya lazma" nilipoipinga.

By the way sex yaweza isiwe starehe kwa asilia yake ila watu wanaichukulia kama sehemu ya kujistarehesha. Mmojawapo ni niliyemquote
 

mulaga

JF-Expert Member
Sep 2, 2019
3,159
2,000
Huwa wanaambiwa wakiwa shule wasome kwanza starehe watazikuta baada ya shule. Hivyo wanatimiza kumalizia starehe kabla awajawa na familia
 

McCarthy

JF-Expert Member
Aug 24, 2017
506
1,000
In this world there's neither right nor wrong, only what is! Tusilazimishane mkuu kwa kupeana orientation fulani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom