Vijana waachwe wakomae kabisa kabla ya kupewa madaraka ya uma.

winnerian

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
335
530
Sabaya akiwawakilisha vijana wengi ambao hawajakomaa kimwili, kiakili na kihisia, amepatwa na janga la uchanga wake katika kufanya mambo (mema + mabaya) bila ya busara na hekima.

Hivyo nashauri taasisi za siasa hususani zenye mamlaka ya nchi zisitishe mara moja kuwaamini vijana wachanga na kuwapa madaraka makubwa ambayo kwayo wanaenda kufanya kinyume na muongozo matokeo yake wanajikuta "wamejikata na wembe mkali" waliopewa wakiwa hawajua kuutumia.

Walio kwenye umri wa makamo na wazee wamepitia mengi katika maisha na angalao kwa uzoefu wao katika kuishi tayari wanakuwa na busara na hekima katika kufanya maamuzi na kutekeleza maagizo ya wakubwa wao.

Sasa mtoto mdogo unampa mamlaka ya kumiliki bunduki unategemea asifanye majanga?
 
Back
Top Bottom