Vijana wa zanzibar na uhitaji wa "Marshall plan"

Yussufhaji

Member
Sep 9, 2018
35
28
Kutoka Mataifa Hohehahe ya Ulaya Magharibi, Hadi Mataifa yenye Nguvu duniani...........

VIJANA WA ZANZIBAR NA UHITAJI WA "MARSHALL PLAN"


"Around the world, there is growing recognition of the need to strengthen policies and investments involving young people. Youth can determine whether this era moves toward greater peril or more positive change. Let us support them developing into productive and powerful leaders." Ban Ki-Moon; United Nations, 2012.

Na
@Mtoto_wa_Mkulima

Naelewa mshtuko ulionao ndugu msomaji wa makala hii haswa kwa nilivyo husisha sera ya kipepari katika jamii ya wajamaa, nilichokizingatia ni mafanikio ya malengo ya sera hiyo.

Wote tunaelewa kuwa sera ya "Marshall Plan" iliibuliwa na Rais wa 33 wa Marekani bwana Harry S. Truman ikiwa ni mpango mkakati wake wa kukuza upebari na kupambana na ukomunist ulioanza kuenea Ulaya Magharibi mara baada ya kumalizika kwa vita ya 2 ya dunia.

Hivyo, sera ya "Marshall Plan" ilijikita katika kuzisaidia nchi za Ulaya Magharibi ambazo zilikuwa hoi kutokana na athari za kivita kuinuka kiuchumi na Kuboresha huduma za kijamii kama njia ya kuziepusha nchi hizo kuangukia katika ukomunist.

Kwa kuzingatia mafanikio ya sera hiyo na hali halisi ya tatizo la ajira kwa vijana visiwani Zanzibar pasi na shaka tuna uhitaji mpango huo.

Natambua kuwepo kwa mipango mbalimbali ya kusaidia vijana kiuchumi na wananchi kwa ujumla, lakini mipango hiyo inaonekana bado kutokutibu tatizo la ajira kwa vijana.

Pamoja na kuwepo na mipango mbalimbali inayo tarajiwa kuekwa na kutekelezwa visiwani kwetu, bado upo umuhimu wa kipekee wa kuwa na mpango mkakati maalum wa kutushajihisha na kutushawishi vijana tuwekeze na kuweza kujiajiri.

Ni wazi kuwa sisi vijana tumeonesha kiu yetu na utayari wetu kuwa watengenezaji ajira badala ya kuwa wasaka ajira, hivyo napendekeza kuwepo kwa Mpango mkakati maalum wa kutusaidia lengo na kiu yetu hio, huku masuala yafuatayo yakizingatiwa:-

1) Urahisi na Unafuu wa upatikanaji mitaji/mikopo: Urahisi kwa maana ya kuwepo kwa masharti yasiomfunga kijana na kushindwa kupata mtaji/mkopo husika, pia unafuu wa mkopo husika kwa kuzingatia muda wa kuanza kurudisha mkopo na riba. Itawezekanaje mkopo wa Tsh milioni 1 kijana aanze kurudisha mwezi mmoja baadae? Bila ya shaka ni kumwekea vikwazo na kuharibu biashara husika, hivyo ni vyema muda wa kuanza kulipa mkopo ukawa mkubwa, afadhali kuanzia mienzi 4 baada ya upatikanaji mkopo husika ndipo ulipaji mkopo huo uanze.

2)Unafuu wa ulipaji kodi na usajili wa biashara husika: Ingependeza iwapo biashara mpya itakayo anzishwa na vijana ikasajiliwa bure na kuanza kulipiwa kodi baada ya mienzi 6 ya kuanzishwa biashara husika, hii itasaidia kutuhamasisha vijana kuanzisha na kufanya biashara mbalimbali huku ikikuza kiwango cha biashara halali na rasmi pamoja na kiwango cha ulipaji kodi kitaongezeka, ada kubwa ya usajili wa biashara, kodi kiwango kikubwa hutukatisha tamaa na kutukwamisha kufanya biashara au kukuza biashara zetu.

3)Utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali: katika hili Serikali na taasisi mbalimbali zinajitahidi sana, hata hivyo mkao zaidi unahitajika.


Kwa maoni yangu @Mtoto_wa_Mkulima, mambo hayo yatasaidia kutuhamasisha vijana kuanzisha miradi mbalimbali na kuiendeleza, ikiwa ni mpango wa papo kwa papo wa kutusaidia vijana kujiajiri, wakati huo huo mipango ya muda mrefu ikitekelezwa kama vision 2050.

Nimalize kwa nukuu.....

"The illiterate of the 21st century will not be those who cannot read and write, but those who cannot learn, unlearn, and relearn." Alvin Toffler, 1970


Mawasiliano:
Mobile N :0777158131
Email :hajjyussuf2@gmail.com
Facebook :Yussuf hajj Khatib
 
Back
Top Bottom