Vijana wa vyama mbadala mbinu yenu ya kumpamba Rais Samia Suluhu imejulikana

Kilemakyaaro

JF-Expert Member
Jul 19, 2016
5,050
5,078
Tokea jana baada ya Mh. Rais Mama Samia Suluhu Hassan kupokea taarifa ya CAG na kutoa maagizo kadhaa, ikiwemo lile la kumsimamisha kazi DG wa TPA bwana Kakoko, vijana wengi wa Upinzani pamoja na baadhi ya Viongozi wa Kamati Kuu kama bwana Lema wamejitokeza kumshangilia sana Mh. Rais.

Kwangu hili ni jambo jema sana pale opponent wako anapopatia na kumpongeza, ni dalili ya uungwana na hii inafaa kuigwa na kupigiwa mfano.

Ajabu nliyoiona sasa ni muendelezo wa Sifa, mapambio na kusifu, huku sifa hizo zikiendelea kutaja wanaotakiwa kushughulikiwa zaidi na Mh. Rais.

Maajabu ni kwamba ukipita ktk kurasa za vijana wengi wa Upinzani utakachoona ni picha za Mama Samia pamoja vijembe kwa Vijana wenzao wa CCM.

Jambo hili limezidi nipa muda wa kudadisi kinachopelekea hawa jamaa kuwazidi hata wana CCM kwa kumshangilia mama, yaani kama vile baada ya msiba Upinzani umechukua nchi na mama ana Card namba 2 ya CHADEMA baada ya mzee Mtei.

Sasa tafakuri yangu imenipa majibu kama mawili ambayo:
1. Inaonekana kuna maagizo makhsusi kwa vijana na viongozi toka CHADEMA kuhakikisha wanam compromise Mh. Rais ili kuhakikisha anatenda kadiri ya matakwa yao na hivyo kujizolea sifa. Yaani ni kuwa wanataka kumpa presha mama ili aamini kua anaungwa mkono na vyama vya Upinzani hivyo atekeleze yalee wanayotaka na hii kwa baadae utakua mtaji wao kisiasa.

2. Wana lengo jingine la kuhakikisha mama anaingia ktk mtafaruku na wana CCM hususan wale Pro Magu kwa kuona anafichua wabaya waliokua ktk Serikali ya mzee. Mtafuruku huu ukifanikiwa nalo litakua na faida kwa upande wa pili kwani itakua ni vita vya panzi vinavyoishia kumfaidisha bwana Kunguru.

3. Wanajaribu kuonhesha mapungufu ambayo kwa namna moja ama nyingine yakitekelezwa na Mh. Rais yatakua na faida kwao na ikiwa hatafanyiwa kazi watayatumia kama silaha kwenye kampeni za 2024/2025.

USHAURI
Ninachoomba kwa Mh. Rais ni kuhakikisha anafanya maamuzi kwa utashi wake bila shinikizo maana wanaomshinikiza iwe wapo ndani ya chama chake ama nje wengi wana malengo ya kujikwapulia point za kisiasa.

Vilevile wale wanaoshauri nnawaomba ikiwa ni kwa nia njema wamshauri Mh. Rais kwa nia njema na kwa maslahi ya Taifa na sio kwa nia ya kujijenga kisiasa.

ASANTENI
 
Watu walikuwa vifungoni wamepata atakayewapa uhuru lazima wamkubali mwanaccm mwenzangu.

Hao ni vyama vya upinzani inawezekana sio kumbuka kile kikundi kidogo kilichokuwa kinaasisi CCM mpya ndani CCM ndicho kinaonana tofauti kwani hawakuwa wanasiasa bali wanamabavu kwa hiyo lazima uone tofauti.

Kwa hiyo wanaccm asili ambao ni wanasiasa nao lazima wamshauri Mama Samia kwani ni mwanasiasa mwenzao nakuomba usishangae Mama kusifiwa huu ndo wakati wako wa kujifunza siasa ili kuondoa ubabe kwa kuwa wanaongozwa ni Binadamu
 
Back
Top Bottom