Vijana wa Tanzania wameandaliwa Kujiajiri au kuajiriwa Taasisi za serikali [Mada Radio One] | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wa Tanzania wameandaliwa Kujiajiri au kuajiriwa Taasisi za serikali [Mada Radio One]

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by DSN, Jul 12, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kuna Dada anaitwa Rozemary Mwakitwange anauzoefu wa miaka ishirini kama meneja uajiri [Human Resource Manager] anasema vijana wa Tanzania hawauziki, kwenye sekta binafsi kwa kuwa hawana content yaani hawafanani na maitaji ya soko.Kwa kuwa lugha inayotawala soko ni Kiiingeleza,na kiingeleza cha vijana wetu wetu wa vyuo vikuu vyetu ni cha kuungaunga.Dada anamwaga kuwa jukumu la Serikali ilipaswa kuandaa watu.

  Yupo Dk Lweitama

  Dk anampongeza dada Roze kwa uchambuzi wake.Dokta anasema atuwekezi kwenye elimu.,anasema Chuo kikuu akitayarishi vijana kwenda kujiajili,anasema lugha ya kutayarisha vijana kwenda kujiajili ni misemo ya benki ya dunia.Anasema siku hizi kuna lugha mpya kuwa UJASILIMALI ambayo anasema lugha hiyo aiendani na mazingira.Chuo kikiuu ni kumfundisha kijana kuwa Mtaalamu au mwelewa.Anasema elimu inayotolewa leo Je inamfanya kijana kuwa MWELEVU?Je elimu inampa nafasi ya kuwa mdadisi kwa maswala ya msingi.

  Anasema mfumo wa elimu [Mitala] hautoi nafasi ya kumfanya kijana kuweza kumudu maisha na kukabiliana.

  Michael Sabuni
  Anasema watoa mitala ya elimu yetu wanahujumu Taifa,kwa kuwa mitala hiyo inatoa watu wasio weza hata kujieleza,pia hawana cofindence,yaani hawajiamini hivyo kushindwa kumudu uwezo wa kukabiliana na maitaji ya soko.[Asema Taifa linazalisha mayai mabovu]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mbona tunaharibu kiswahili hivyo? Kujiajili au Kuajiliwa (R is missing)
   
 3. m

  mdawa Senior Member

  #3
  Jul 12, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 104
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Vijana wa Tanzania Wameandaliwa Kujiajili au Kuajiliwa Taasisi za Serikali [Mada Radio One]

  Gazeti la Mwananchi la leo kuna article nzuri sana jinsi watanzania walivyoporomoka katika lugha ya kiswahili kimetushinda. Utafiti uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwa Kenya wapo mbele yetu katika matumizi ya kiswahili fasaha. Hiki ni kiashirio cha taifa lililoporomoka. Ukizungumzia juu ya sisi kushindwa kutumia lugha fasaha wengi wanaona ni ktu cha kawaida tu, ya kwamba ni lafudhi za lugha zetu. Mbona zamani watu waliongea na kuandika lugha hii vizuri tuu. Siku hizi hata viongozi wengi tu hawawezi kuongea lugha yetu kwa ufasaha.
   
 4. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Siunajua kwa Watanzania kwa kuwa Kiswahili ni lugha yetu basi tumejisahau kiasi kuwa kwa kuwa hakuna anaesimamia uthabiti wa kuhakikisha lugha hii ya kiswahili inadumishwa kama tunu inayohitaji kulindwa na kukuzwa.Hivyo lugha hii kwa upande wa watanznaia imekuwa ni lugha tu ya kuendeshea mawasiliano lakini bila vihakiki kuwa matumizi yake ni yenye usanifu kulingana na uwezo wa lugha yenyewe.

  Kazi kwelikweli na kiswahili chetu,tunakizungumza vizuri tunakiandika ovyo basi shida tupu.Na yote hii ni kuwa unasoma Kiswahili shule ya msingi ikifika sekondari unaagana na kiswahili na kuingia kwenye lugha ya watu ya kigeni,ambayo nayo ni kichomi pia kwa wengi wetu.
   
Loading...