Vijana wa Tanzania na mustakabali wa taifa: Ushindi katika ujana

Tao

Member
Nov 10, 2018
95
157
Kijana ni nani?
Kijana ni mtu wa kike au wa kiume mwenye umri kati ya miaka 15 na 45.Hata hivyo katika dhana ya maendeleo ujana unaweza kuwa zaidi ya umri.

Maandiko matakatifu yamenena mambo mengi juu ya kijana, na baadhi ya hayo ni kuwa fahari ya kijana ipo katika nguvu zake (Mithali 20:29). Kijana ana nguvu nyingi, neno la Mungu linakaa ndani yake na kisha amemshinda shetani(1Yohana 2:14b).

Baada ya Yoshua kuchukua nafasi ya Musa, Mungu alimpa mikakati ya namna atakavyoweza kufikia lengo ambalo lilikuwa kuwafikisha Waisraeli katika nchi ya ahadi, Kanaani. Mikakati hiyo ni kama ifuatavyo:
1. Uwe hodari tu na ushujaa mwingi
2. Uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume au wa kushoto.(Yosh. 1.7).

”Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo…."(Yoshua 1:8)
Paulo alimwambia Timotheo hivi: “Usiache mtu yeyote audharau kamwe ujana wako. Badala yake, uwe kielelezo kwa waaminifu katika kusema, katika mwenendo, katika upendo, katika imani, katika usafi wa kiadili. . . . Endelea kufanya bidii katika kusoma mbele ya watu wote, katika kuhimiza, katika kufundisha. . . . Tafakari mambo haya; zama katika hayo, ili maendeleo yako yawe wazi kwa watu wote.” (1 Tim. 4:12-15)

Leo nimeamua kuleta mada hii ya vijana kwani nina uoga kuwa taifa hili linaweza kushindwa kufikia kwenye maendeleo makubwa yanayotarajiwa kutokana na aina ya vijana tulionao.Mada hii inaelezea kuwa yawezekana tuna laana ya kizazi kutokana na vijana wetu kutopikwa na kuandaliwa ipasavyo,mada inaeleza kinagaubaga kuwa vijana ndio ngao na silaha muhimu kwa taifa lolote hivyo vijana wasipoandaliwa ipasavyo taifa litaanguka.

Mwalimu Nyerere alitambua umuhimu wa kuandaa vijana hivyo pamoja na kuwapa elimu ya darasani aliwapeleka kwenye mafunzo ya JKT ili kuwafanya mashujaa,wakakamavu, majasiri,wajue historia ya Tanzania na zaidi ya yote ili wawe wazalendo.

Baada ya Mwalimu kung'atuka tawala zingine hazikutambua umuhimu huo na ndio ukawa mwanzo wa anguko letu.
Wakati ule vijana walishiriki mambo yote yanayohusu ujenzi wa taifa,hii dhana potofu kuwa vijana ni taifa la kesho haikuwepo,wazee na vijana waliketi pamoja kufanya maamuzi mazito ya taifa,walitambua maadui zetu na walishiriki kuwaburuza mafisadi na wahujumu uchumi,hii yote ilitokana na vijana kupikwa na kuokwa vyema.tofauti na kizazi cha sasa ambacho hakiwatambui maadui wa Tanzania,vijana wa sasa,si wazalendo,hawana maadili na si wacha Mungu,ni wahuni,mateja na hawajui kabisa taifa linahitaji nini ili liendelee na kibaya zaidi vijana wameungana na kundi la mafisadi,watu wenye hila na mikakati ovu dhidi ya taifa na vibaraka wa mabeberu.

JPM ni rais aliyejitoa mhanga kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua kubwa za maendeleo,anafumua mikataba mibovu kwenye sekta ya madini,anapambana na makundi haramu na ameinitiate miradi mikubwa ya kimkakati ili kurudisha heshima ya Tanzania iliyopotea na katika kufanikisha azma yake hii amewaamini vijana na kuwapa nafasi kubwa za uongozi lakini cha kushangaza baadhi ya vijana hawamuelewi kabisa na wanamdhihaki kwenye mitandao ya kijamii.

JPM anapofumua mikataba mibovu vijana badala ya kumuunga mkono wanadhihaki kuwa anapoteza muda kwani mabeberu yana nguvu kubwa,JPM anapochukua hatua kali dhidi ya mafisadi na wahujumu uchumi baadhi ya vijana wanadhihaki kuwa anawaonea na kuwa aheshimu haki za binadamu,hii inauma sana.

Natoa rai kwa wakuu wa taifa hili kuwa wachukue hatua za makusudi ili kuwaandaa na kuapika vijana,ADUI anaweza kupenya kirahisi hapa nchini kwani ANAJUA kuwa vijana wengi hawajitambui.
Mungu atukuzwe kupitia vijana wa Tanzania.
 
Laiti mwalimu Nyerere angefaulu Sera za ujamaa haya yote yasingeleta migogoro
 
Back
Top Bottom