Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,498
- 51,092
Wakati mwalimu anatamka maneno kuwa anataka katika nchi hii vijana jeuri, watakaosimama na kumwambia bwana mkubwa kuwa hapana hatuko tayari kutii na kuvumilia mambo ambayo si ya Kitanzania ilikuwa ni miaka ya 70 mwanzoni.
Vijana hao wakati huo ni hawa akina Butiku, Warioba, Jakaya, Msekwa, Membe Akina marehemu mzee Sitta na wengineo wengi.
Wakati huo yule Mpangaji wa magogoni alikuwa bado shule ya msingi akisoma kwa hisani ya UPE (halafu leo anasimama anadai eti mbona wenzie hawakununua ndege yeye kanunua, kituko!!)
Vijana hawa wa wakati huo ni watu ambao tunaweza kusema wanamjua Mwalimu, kila mmoja kwa namna yake ana upako wa mwalimu.
Butiku alikuja kuwa katibu wa mwalimu, Warioba alikuja kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya mwalimu, Jakaya alikuwa kijana wake aliyekwenda kuijenga CCM Zanzibar baada baada ya kuunganika ASP na TANU
Membe alikuwa kijana wa mwalimu hapo ikulu Dar
Hawa ni vijana ambao wakati mwalimu anatoa meseji yake ya kutaka vijana jeuri, kimsingi HAO NDO WALIKUWA walengwa haswaa wa meseji hiyo!
Sasa vijana wale wa zamani LEO Wameamua kuuonyesha moto uliomo ndani ya vifua vyao kwamba wao bado ni JEURI, hawaogopi, hawatishiki na kwamba Itakapobidi kwa manufaa ya TAIFA hili JEURI yao wataionyesha.
Kama coordination hivi, Vijana hao katika siku chache hizi Wameunguruma kwa sauti nzito, Sauti ambayo mwangwi wake unatikisa mizizi dhaifu ya Udikteta na Uungumtu ambao unajaribu kujikita.
Alisema mzee Butiku juu ya haja ya kuheshimu utawala bora
Msekwa kasema, Tunahitaji katiba bora
Warioba akafuata akasema Hii inayoitwa kupambana na Ufisadi mbona inawagusa wafanyabiashara na watumishi wa umma lakini hakuna kiongozi hata mmoja?
Leo kaja Jakaya, akapiga cruise missile utadhani tomahawk ya wamarekani, Jakaya kasema UKIWA KIONGOZI HUNA HAJA YA KUJIMWAMBAFAI MWAMBAFAI, Maadam wewe ni kiongozi tekeleza tu yakupasayo usiwadunishe watu!
Lakini kabla hili halijapoa, Kijana Mwingine Jeuri wa enzi za Mwalimu, Bernad Cammillius Membe akapiga za Chembe kabisaa kwa kuandika waraka kwa baba askofu kuwa HATISHIKI NA WALA HATAABUDU MUUNGU
Hawa ni wale vijana jeuri wa mwalimu wamesimama vifua mbele kulinda Heshima ya Taifa, Tunu zake na maadili yake
Hii Coordination na combination ni kali
na nimepata faraja kubwa kumbe Hata zile ndoto za Mtu fulani kutaka kung'ang'ania kitini kama Gundi haitofanikiwa, Azma yake haitofanikiwa, Tunao makamanda Vijana Jeuri wa mwalimu nyuma yetu, na sisi Jeshi la vijana wa sasa tuliokuwa tunataka uongozi, kwa pamoja tutashinda jeshi lolote lile litakalojaribu kuvunja Katiba ya nchi yetu, kutetea uvunjifu wa katiba ya nchi yetu, tutashinda jeshi lolote lile litakalojaribu kutetea tabia za uungu mtu, kutoheshimu wananchi na kuruin maisha ya wananchi kwa kisingizio chochote kile
HIMAAAAA HIMAAA TANZANIAAAAA