Vijana wa Mwalimu Nyerere sasa wameamua kusimama na kusema imetosha!!!

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
4,296
Points
2,000

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
4,296 2,000
Wakati mwalimu anatamka maneno kuwa anataka katika nchi hii vijana jeuri, watakaosimama na kumwambia bwana mkubwa kuwa hapana hatuko tayari kutii na kuvumilia mambo ambayo si ya Kitanzania ilikuwa ni miaka ya 70 mwanzoni.

Vijana hao wakati huo ni hawa akina Butiku, Warioba, Jakaya, Msekwa, Membe Akina marehemu mzee Sitta na wengineo wengi.

Wakati huo yule Mpangaji wa magogoni alikuwa bado shule ya msingi akisoma kwa hisani ya UPE (halafu leo anasimama anadai eti mbona wenzie hawakununua ndege yeye kanunua, kituko!!)

Vijana hawa wa wakati huo ni watu ambao tunaweza kusema wanamjua Mwalimu, kila mmoja kwa namna yake ana upako wa mwalimu.

Butiku alikuja kuwa katibu wa mwalimu, Warioba alikuja kuwa mwanasheria mkuu wa serikali ya mwalimu, Jakaya alikuwa kijana wake aliyekwenda kuijenga CCM Zanzibar baada baada ya kuunganika ASP na TANU

Membe alikuwa kijana wa mwalimu hapo ikulu Dar

Hawa ni vijana ambao wakati mwalimu anatoa meseji yake ya kutaka vijana jeuri, kimsingi HAO NDO WALIKUWA walengwa haswaa wa meseji hiyo!

Sasa vijana wale wa zamani LEO Wameamua kuuonyesha moto uliomo ndani ya vifua vyao kwamba wao bado ni JEURI, hawaogopi, hawatishiki na kwamba Itakapobidi kwa manufaa ya TAIFA hili JEURI yao wataionyesha.

Kama coordination hivi, Vijana hao katika siku chache hizi Wameunguruma kwa sauti nzito, Sauti ambayo mwangwi wake unatikisa mizizi dhaifu ya Udikteta na Uungumtu ambao unajaribu kujikita.

Alisema mzee Butiku juu ya haja ya kuheshimu utawala bora

Msekwa kasema, Tunahitaji katiba bora

Warioba akafuata akasema Hii inayoitwa kupambana na Ufisadi mbona inawagusa wafanyabiashara na watumishi wa umma lakini hakuna kiongozi hata mmoja?

Leo kaja Jakaya, akapiga cruise missile utadhani tomahawk ya wamarekani, Jakaya kasema UKIWA KIONGOZI HUNA HAJA YA KUJIMWAMBAFAI MWAMBAFAI, Maadam wewe ni kiongozi tekeleza tu yakupasayo usiwadunishe watu!

Lakini kabla hili halijapoa, Kijana Mwingine Jeuri wa enzi za Mwalimu, Bernad Cammillius Membe akapiga za Chembe kabisaa kwa kuandika waraka kwa baba askofu kuwa HATISHIKI NA WALA HATAABUDU MUUNGU

Hawa ni wale vijana jeuri wa mwalimu wamesimama vifua mbele kulinda Heshima ya Taifa, Tunu zake na maadili yake

Hii Coordination na combination ni kali
na nimepata faraja kubwa kumbe Hata zile ndoto za Mtu fulani kutaka kung'ang'ania kitini kama Gundi haitofanikiwa, Azma yake haitofanikiwa, Tunao makamanda Vijana Jeuri wa mwalimu nyuma yetu, na sisi Jeshi la vijana wa sasa tuliokuwa tunataka uongozi, kwa pamoja tutashinda jeshi lolote lile litakalojaribu kuvunja Katiba ya nchi yetu, kutetea uvunjifu wa katiba ya nchi yetu, tutashinda jeshi lolote lile litakalojaribu kutetea tabia za uungu mtu, kutoheshimu wananchi na kuruin maisha ya wananchi kwa kisingizio chochote kile

HIMAAAAA HIMAAA TANZANIAAAAA
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
4,296
Points
2,000

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
4,296 2,000
Nyerere hana vijana wanaondekeza ufisadi
Acha magufuli awanyooshe

Ukiona wanalia ujue maslahi yao yameguswa

Walizoea kula wao tu
Sasa Magufuli amefanya raslimali zetu ni kwa kila Mtanzania wameanza kununa

Magufuli usiyumbe Baba
Hao hawakugawa nyumba za serikali kwa mchepuko au ndugu kama njugu!

Jiwe ni fisadi nyangumi!!!
 

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Messages
3,850
Points
2,000

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2019
3,850 2,000
Yaani sasa shetani ajue imetosha, ameumiza wengi sana, yaani huyu kila mtu kwa nafasi yake amwambie imetosha, afuate sheria, katiba na atende haki na aliowaonea wote awaombe msamaha na awalipe wale aliowafukuza kazi kwa kuwaonea na kuwabomolea nyumba zao, bila kusahau aliowabambika kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha.
 

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Messages
3,850
Points
2,000

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2019
3,850 2,000
Nyerere hana vijana wanaondekeza ufisadi
Acha magufuli awanyooshe

Ukiona wanalia ujue maslahi yao yameguswa

Walizoea kula wao tu
Sasa Magufuli amefanya raslimali zetu ni kwa kila Mtanzania wameanza kununa

Magufuli usiyumbe Baba
Wao ndio walionunua kivuko kibovu? Unaweza kunyoosha nchi kwa kutofuata sheria na katiba?
 

Mkomavu

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2016
Messages
9,178
Points
2,000

Mkomavu

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2016
9,178 2,000
Nyerere hana vijana wanaondekeza ufisadi
Acha magufuli awanyooshe

Ukiona wanalia ujue maslahi yao yameguswa

Walizoea kula wao tu
Sasa Magufuli amefanya raslimali zetu ni kwa kila Mtanzania wameanza kununa

Magufuli usiyumbe Baba
Fisadi aliuza nyumba na kuhonga nyumba kwa vimada may be wewe ndiye uliyehongwa,na alinunua kivuko kibovu
 

Mgg3

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2018
Messages
404
Points
1,000

Mgg3

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2018
404 1,000
Shida ya ccm wa sasa wanafikiri ccm ilianza mwaka 2015 kipindi cha magu. Haya tunayoona yameletwa na wanaccm naona pia wanajitahidi sana kuzoea kinyesi chao. Watu walihaidiwa maji mwaka 1961 na wameletewa 2019 mwezi 9 na bado vijiji vingine hawana ndoto za kupata maji. Lakini wananchi wanaruka ruka na kushangilia, wameshasahau miaka kadhaa walihaidiwa na mbunge wa ccm wateletewa maji.

Watanzania wengi hawana elimu ya kung'amua mambo vichwani mwao. Ukiwa na elimu ya darasa la 7 ukikutana na mwalimu mkuu anakuwa kama maskini kakutana na tajiri. Elimu inasadia sana, inafuta ujinga na inaondoa hofu.

Kwangu haina kitu cha kuweza kunishawishi kuwa kwa sasa CCM inachapa kazi. Utasikia siku hizi mafisadi wanakiona cha mtema kuni. Huo ufisadi uliletwa na nani kama siyo ccm? Ajira wamefuta lakini kila siku wanaimba mapambao ya kusifu. Hali ni mbaya ajira hakuna.
 

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Messages
6,763
Points
2,000

Bams

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2010
6,763 2,000
Nyerere hana vijana wanaondekeza ufisadi
Acha magufuli awanyooshe

Ukiona wanalia ujue maslahi yao yameguswa

Walizoea kula wao tu
Sasa Magufuli amefanya raslimali zetu ni kwa kila Mtanzania wameanza kununa

Magufuli usiyumbe Baba
Hizo lugha za kusema kuna mafisadi halafu hao mafisadi wenyewe hakuna anayepelekwa mahakamani akathibitika kuwa ni fisadi ni kauli za kiwendawazimu maalum kwaajili ya watu waliopungukiwa uelewa.
 

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Messages
13,145
Points
2,000

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Joined Aug 8, 2015
13,145 2,000
Nyerere hana vijana wanaondekeza ufisadi
Acha magufuli awanyooshe

Ukiona wanalia ujue maslahi yao yameguswa

Walizoea kula wao tu
Sasa Magufuli amefanya raslimali zetu ni kwa kila Mtanzania wameanza kununa

Magufuli usiyumbe Baba
Siku magu akianza kumsema atakayekua kwenye madaraka kipindi hicho wewe unayemsifia sasa hivi utalipwa buku saba za kitanzania ukamtusi na kumwita fisadi wa 1.5Trillion, kivuko kibovu, tena utaweka chumvi na kusema magu alihonga nyumba kwa kimada wake!!

Tena kipindi hicho utaenda mbele zaidi na kusema alinunua mandege mabovu kifisadi na alifanya maisha ya watanzania kuwa magumu!!

Hizi ndio akili za uvccm!! mpe buku 7 umemaliza akili yooote!

Kwa lugha rahisi ni kwamba unatumika NA UTAKUJA KUTUMIKA TENA KUMTUSI MAGU AKISTAAFU!!
 

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Messages
6,763
Points
2,000

Bams

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2010
6,763 2,000
Bila kupepesa wala kuremba, utawala wa awamu hii ni wa kimabavu na uonevu. Kuna watu wengi wameumizwa bila makosa. Na hawa kuna siku Mungu atawajibia na kuwalipia kisasi kwa waliowaonea.

Viongozi wengi awamu hii wamekosa busara na hekima.
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
11,072
Points
2,000

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
11,072 2,000
Unaweza utajenga hoja kulingana na fikra zako kwa jinsi unavyopenda ili tu kutibu matamanio yako!

Neno ''vijana wa Mwl. Nyerere'' unaweza kuliweka sehemu yoyote ile ili tu upitishe hoja yako hasa kwa watu wasiojua historia ya taifa ambalo kwa sasa linaitwa Tanzania!

Hao hao unaowaita kwa sasa ''vijana wa Mwl. Nyerere'', kesho utaibuka tena na kuwaita wanafiki kwa sababu tu walichokifanya ni kinyume na jinsi ulivyotafsiri maneno yao ili kukidhi matamanio yako.

Kibaya zaidi, unachofanya ni kuicheza ngoma ya CCM huku ukiwaalika wanaojiita ''wapinzani'' wakushangilie bila kujua kuwa CCM huonyesha makucha, nguvu na umoja wakati wa kutafuta dola.
 

An Eagle

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
1,481
Points
2,000

An Eagle

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
1,481 2,000
Acha ' Kuwagombanisha ' na ' Kuwafitinisha ' Wazee waliokuwa ' Wasaidizi Waandamizi ' wa Hayati Baba wa Taifa kuanzia hawa uliowataja hapa na wengine ambao yawezekana ukawa huwajui au umewasahau pia dhidi ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano hii yake Ndugu Dkt. John Pombe Magufuli eti kwakuwa tu leo hii Rais wenu Mstaafu Kikwete ' yamemtoka ' maneno ambayo nyie ' Wanafiki ' na Watu wenye ' Chuki ' mnalazimisha ' Kutuaminisha ' na ' Kuwaaminisha ' Watu kuwa kwa 100% amemlenga / alikuwa anamlenga Rais Dkt. Magufuli.

Sasa labda tu leo hii nikusaidie kama kuna Rais ambaye aliwachukia tena wazi wazi hao Wazee wako tajwa hapo ( waliokuwa Wasaidizi Waandamizi wa Hayati Baba wa Taifa ) na hata hakuipenda Taasisi yenyewe ya MNF sema alilazimika tu Kuihudumia kwakuwa aliona Aibu kuwa kwanini asiisaidie wakati akina Museveni, Kagame, Rais wa China na hata Serikali ya Afrika Kusini zinaisaidia na kuilea mno hiyo Taasisi alikuwa ni huyu huyu Kikwete wenu ambaye leo hii ' Kiunafiki ' kabisa mnajifanya Kumuona Mtu muhimu Kwenu wakati ' Kiuchambuzi ' Yeye ndiyo amechangia ' Kuiharibu ' kabisa Tanzania hii kiasi cha hadi kumpa wakati mgumu Rais Dkt. Magufuli wakati wa Kampeni mwaka 2015 kwani kila alikokuwa akipita alikuta akiambiwa kuwa CCM haitakiwi na ndiyo maana kuna muda aliamua kubadili upepo na kusema kuwa Chagua Magufuli na akaiacha kwa muda ile ' Slogan ' ya Chagua CCM kitu ambacho kilimsaidia Kuaminika na Kukubalika na Watanzania wengi hasa ikizingatiwa kuwa rekodi yake ya Kiutendaji katika Wizara alizopita zilikuwa ni nzuri na alikuwa ni Mtu Mchapakazi kweli kama alivyo sasa kama Rais wetu Kipenzi kabisa.

Na kwa usichokijua sasa ni kwamba hakuna Watu ambao Ushauri wao unasikilizwa vyema hadi kwa haraka na Rais wa sasa JPM kama hao Wazee akina Joseph Butiku, Jaji Mstaafu Joseph Warioba, Mama Maria Nyerere na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mzee Benjamin William Mkapa bila kuwasahau na wengineo ambao kwa pamoja walipata kuwa Watu Waaminifu kabisa na Wasaidizi wazuri wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Na ni juhudi za hawa hawa Wazee ( Pro Mwalimu Nyerere ) ndizo zilimfanya Rais JPM afanikiwe kule Mkutanoni Dodoma hasa baada ya Kugundua ' Janja ' ya Kikwete na Genge lake la ' Wanamtandao ' na ' Mafisadi ' ambao waliitaka hii nchi ili waendeleze ' Uhuni ' na ' Uswahili ' wao lakini alishindwa na hao Wazee wachache tu ila wenye Akili, Mbinu, Mikakati na Maarifa mengi huku pia baadhi yao wakiwa wameiva vyema ' Kiujasusi ' na si tu kwamba wanasifika bali pia wanaogopeka kwa hiyo Fani.

Ngoja niishie hapa ili nikuache uendelee Kuwadanganya Watu hapa Mtandaoni na ' Propaganda ' zako za ' Kipuuzi ' sana.
 

kurlzawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2018
Messages
7,762
Points
2,000

kurlzawa

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2018
7,762 2,000
Nyerere hana vijana wanaondekeza ufisadi
Acha magufuli awanyooshe

Ukiona wanalia ujue maslahi yao yameguswa

Walizoea kula wao tu
Sasa Magufuli amefanya raslimali zetu ni kwa kila Mtanzania wameanza kununa

Magufuli usiyumbe Baba
nyumba zakugawia malaya kumbe sio ufisadi na kununua ndege midoli sio ufisadi?
 

Forum statistics

Threads 1,343,525
Members 515,078
Posts 32,787,439
Top