Vijana wa Lumumba, ni nani Kawadanganya Marekani kuna vyama viwili vya siasa?

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,581
11,658
KWA wasiofuatilia vyema siasa za Marekani wanaweza wakadhani kuna vyama viwili tu vya siasa nchini humo; Democratic kinachotawala sasa na hasimu wake Republican, kumbe sivyo.

Taifa hilo lina vyama vingi ukiondoa hivyo viwili vinavyotawala kwa kupokeza, huku vyama maarufu zaidi vikiwa Libertarian, Kijani (Green Party) na Kikatiba (Constitutional Party).

Libertarian ni chama kinachopigania uhuru wa mawazo, dini, kufikiri na kutenda, ukombozi wa kiraia na kupinga vita.

Chama cha Kijani huendekeza siasa za mazingira, ukombozi wa kiraia na kupinga vita huku Chama cha Kikatiba kikiwa cha sera za uhafidhina wa kijamii na haki za kidini.
Lakini pia kuna vyama vingine vya siasa ambavyo vimeishia katika ngazi za majimbo, au ambavyo havina lengo la urais. Vyama vya aina hii si makusudio ya makala haya!

Hivyo basi, vyama hivyo katika umoja wao vinajulikana kama ‘Chama cha Tatu’ yaani baada ya Democratic na Republican na wagombea wake hujulikana kama wagombea wa ‘Chama cha Tatu’ bila kujali kama wanatokea vyama tofauti.

Kwa sababu hiyo wagombea kutoka vyama hivyo vidogo kwa kawaida huwa hawana athari kubwa katika chaguzi za urais nchini humo. sihusishi zile za majimbo!.

Hata Marekani ilikuwapo ‘CCM’, ikafa

Hata kama vyama vya siasa vinakuwa kwenye midomo ya watu kwa vipindi virefu vikilinda na kusisitiza masuala yaleyale, misingi ileile, takwimu ya idadi ya watu na kuungwa mkono, baadaye huchukiwa kutokana na sera mbovu au zilizopitwa na wakati na hupumzishwa. Hivyo ndivyo vyama vya ukombozi katika nchi za Kenya, Zambia, Malawi, Uganda, Rwanda, Burundi, Nigeria, India na kwingineko vilipumzishwa.

je, wajua kuwa kuna vyama vya siasa Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na kwingineko duniani viliwahi kushamiri na kutoa ama marais au waziri mkuu au chansela, lakini baadaye vilikataliwa na wananchi na vikafa?

Tutazame Marekani. Marekani hakukuwa na vyama vya siasa kama ilivyo leo.

Historia inaonyesha Rais wa kwanza George Washington hakuwa mwanachama wa chama chochote, akiamini kuwa nchi inaweza kutawaliwa bila vyama vya siasa na alikuwa akihofia vyama kukwamisha mabadiliko aliyokusudia.

Hata hivyo, vyama vilianza enzi za utawala wake. Kati ya mwaka 1789–1797 aliyekuwa Waziri wa Fedha, Alexander Hamilton alianzisha chama cha Federalist, ilhali James Madison na Thomas Jefferson walijibu kwa kuanzisha chama cha Democratic-Republican. Rais Washington alishabikia Federalist.
Federalist ilipata wafuasi wengi waliounga mkono Katiba iliyoandikwa.

Pia, wafanyabiashara na maofisa wa mabenki waliunga mkono sera za uchumi za chama hicho, na madaraka kurundikwa katika serikali kuu.

Federalist ilitoa rais mara moja tu, John Adams (1797 – 1801) na iliondolewa na chama cha Democratic-Republican kilichotumia sera ya kupeleka madaraka majimboni.

Jefferson aliwania urais akashinda mwaka 1801 na 1804; Madison aliongoza mwaka 1808 na 1812; James Monroe akatawala 1816 na 1820.

Baada ya Federalist kuanguka iliibuka migogoro iliyosababisha kifo chake mwaka 1824.

Migogoro mingine iliibuka na kusababisha minyukano katika chama pinzani cha Democratic-Republican na kufikia mwaka 1828 kikagawanyika; kipande kimoja kikajiita Demoratic Party ambacho kipo hadi leo na kingine kilichoongozwa na John Quincy Adams na Henry Clay kikaitwa National Republicans na baadaye kikabatizwa jina la Whig.

mr mkiki.

Wapinzani ni watoa elimu.

Wanalumumba mmenipata.
 
Pumbavu Sana wewe ,Sema asichojua ni nini?
kakosea kitu kimoja tu kwenye uzi wake, Republican ndo wanaongoza US kwa sasa na siyo Democratic.
Nyie hata mwenyekiti wenu ni zero tu ije kuwa Nyie fans wake si ndo mende kabisa Nyie.
Yani ndio watu wakutuletea viwanda hao?
 
US kuna vyama viwili tu vya siasa. Wengine ni Independents.
hivyo vyama ulivyovitaja nobody cares about them, nobody talks about them.
Vyama vipo viwili tu, na Independents are not organized ni independents.
 
KWA wasiofuatilia vyema siasa za Marekani wanaweza wakadhani kuna vyama viwili tu vya siasa nchini humo; Democratic kinachotawala sasa na hasimu wake Republican, kumbe sivyo.

Taifa hilo lina vyama vingi ukiondoa hivyo viwili vinavyotawala kwa kupokeza, huku vyama maarufu zaidi vikiwa Libertarian, Kijani (Green Party) na Kikatiba (Constitutional Party).

Libertarian ni chama kinachopigania uhuru wa mawazo, dini, kufikiri na kutenda, ukombozi wa kiraia na kupinga vita.

Chama cha Kijani huendekeza siasa za mazingira, ukombozi wa kiraia na kupinga vita huku Chama cha Kikatiba kikiwa cha sera za uhafidhina wa kijamii na haki za kidini.
Lakini pia kuna vyama vingine vya siasa ambavyo vimeishia katika ngazi za majimbo, au ambavyo havina lengo la urais. Vyama vya aina hii si makusudio ya makala haya!

Hivyo basi, vyama hivyo katika umoja wao vinajulikana kama ‘Chama cha Tatu’ yaani baada ya Democratic na Republican na wagombea wake hujulikana kama wagombea wa ‘Chama cha Tatu’ bila kujali kama wanatokea vyama tofauti.

Kwa sababu hiyo wagombea kutoka vyama hivyo vidogo kwa kawaida huwa hawana athari kubwa katika chaguzi za urais nchini humo. sihusishi zile za majimbo!.

Hata Marekani ilikuwapo ‘CCM’, ikafa

Hata kama vyama vya siasa vinakuwa kwenye midomo ya watu kwa vipindi virefu vikilinda na kusisitiza masuala yaleyale, misingi ileile, takwimu ya idadi ya watu na kuungwa mkono, baadaye huchukiwa kutokana na sera mbovu au zilizopitwa na wakati na hupumzishwa. Hivyo ndivyo vyama vya ukombozi katika nchi za Kenya, Zambia, Malawi, Uganda, Rwanda, Burundi, Nigeria, India na kwingineko vilipumzishwa.

je, wajua kuwa kuna vyama vya siasa Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na kwingineko duniani viliwahi kushamiri na kutoa ama marais au waziri mkuu au chansela, lakini baadaye vilikataliwa na wananchi na vikafa?

Hata kama vyama vya siasa vinakuwa kwenye midomo ya watu kwa vipindi virefu vikilinda na kusisitiza masuala yaleyale, misingi ileile, takwimu ya idadi ya watu na kuungwa mkono, baadaye huchukiwa kutokana na sera mbovu au zilizopitwa na wakati na hupumzishwa. Hivyo ndivyo vyama vya ukombozi katika nchi za Kenya, Zambia, Malawi, Uganda, Rwanda, Burundi, Nigeria, India na kwingineko vilipumzishwa.

Tutazame Marekani. Marekani hakukuwa na vyama vya siasa kama ilivyo leo.

Historia inaonyesha Rais wa kwanza George Washington hakuwa mwanachama wa chama chochote, akiamini kuwa nchi inaweza kutawaliwa bila vyama vya siasa na alikuwa akihofia vyama kukwamisha mabadiliko aliyokusudia.

Hata hivyo, vyama vilianza enzi za utawala wake. Kati ya mwaka 1789–1797 aliyekuwa Waziri wa Fedha, Alexander Hamilton alianzisha chama cha Federalist, ilhali James Madison na Thomas Jefferson walijibu kwa kuanzisha chama cha Democratic-Republican. Rais Washington alishabikia Federalist.
Federalist ilipata wafuasi wengi waliounga mkono Katiba iliyoandikwa.

Pia, wafanyabiashara na maofisa wa mabenki waliunga mkono sera za uchumi za chama hicho, na madaraka kurundikwa katika serikali kuu.

Federalist ilitoa rais mara moja tu, John Adams (1797 – 1801) na iliondolewa na chama cha Democratic-Republican kilichotumia sera ya kupeleka madaraka majimboni.

Jefferson aliwania urais akashinda mwaka 1801 na 1804; Madison aliongoza mwaka 1808 na 1812; James Monroe akatawala 1816 na 1820.

Baada ya Federalist kuanguka iliibuka migogoro iliyosababisha kifo chake mwaka 1824.

Migogoro mingine iliibuka na kusababisha minyukano katika chama pinzani cha Democratic-Republican na kufikia mwaka 1828 kikagawanyika; kipande kimoja kikajiita Demoratic Party ambacho kipo hadi leo na kingine kilichoongozwa na John Quincy Adams na Henry Clay kikaitwa National Republicans na baadaye kikabatizwa jina la Whig.

mr mkiki.

Wapinzani ni watoa elimu.

Wanalumumba mmenipata.
Umekosea; chama kinachotawala kwasasa ni Republican na si Democrat
 
Weee bwege jingalao ulieanzisha uzi kwamba Marekani kuna vyama viwili tu vya siasa njoo huku unavuliwa nguo upo mtupu kabisa.
Ukiwa mtu pale Lumumba lazima kichwani kuwe hamnazo.
Mkuu,tunapojaaliwa watoto tuwe makini kuwapa majina.Na vilevile,tuwakanye watoto wetu kujipa majina hata kama ya utani,yasiwe yanaakisi uhayawani.Maneno au majina huumba uhalisia.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom