Vijana wa kutembeza maandazi barabarani wanahitajika

Bac3

Senior Member
Apr 21, 2016
129
68
Natafuta vijana wanaohitaji shughuli ndogo ndogo!
Shughuli niliyonayo ni kuuza mandazi na chai kwa kutembeza!

MALIPO; Malipo ni sh .3000 kwa kila deli ukilimaliza kila siku. Ila ukiwa na uwezo wa kuuza madeli mawili unapat 6000
MAHALI PA KUISHI; tutaishi wote geto

MUDA WA KAZI; Ni kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi mpaka ukimaliza mzigo wako

ANGALIZO!!!! mimi naishi geto tu,kwa hiyo hamna starehe ni kukomaa kiume ili mradi unatafuta maisha! Pia kazi hii inahitaji uipende kwa sababu usipofanya hivo itakushinda unatumia mda mwingi barabarani na jua hili usipojituma utashindwa kazi.kumbuka unalipwa kulingana na ulivofanya kazi na siku utakazofanya kazi.tunafanya kazi wote kwa hiyo hamna kulala

MAWASILIANO; Kama kuna mtu ana ndugu yake anaweza fanya kazi hii basi anitafute kwa hii namba 0689569883

MAHALI NINAPOISHI; Dar es salaam,Temeke
 
Tabia mbaya kuwatumikisha wasiokuwa ndugu zako.nenda kawachukue wakubwa na wadogo zako uje uwape kazi za mateso
Inaonekana haujaelewa umekurupuka.nani kakwambia ni kazi ya mateso?mbona na mimi naifanya? Afu nimesema siwalipi? Afu unafikiri kila kazi ni madogo eh? Mbona mimi ni mkubwa na nina degree yangu ila nafanya hii kazi? Wake up inaonekana bado umelala!
MJINI UKIWA NA AIBU HUWEZI ISHI!
 
Kawachukue ndugu zako tu ndiyo uje uwatembeze juani wale vumbi.wiki tu wanaumwa halafu uwatose.na wakishikwa na mgambo wa jiji uwakane
 
Kawachukue watoto wa Mjomba kijijini kwenu

Vijana mnaokula ugali wa wazazi bure au mlioko vyuoni mna mtazamo tofauti kabisa kwenye haya maisha

Acheni kubeza ,nyie kama elfu sita mnaiona ndogo kuna watu wanaihitaji
Tabia mbaya kuwatumikisha wasiokuwa ndugu zako.nenda kawachukue wakubwa na wadogo zako uje uwape kazi za mateso

Kawachukue ndugu zako tu ndiyo uje uwatembeze juani wale vumbi.wiki tu wanaumwa halafu uwatose.na wakishikwa na mgambo wa jiji uwakane
 
Ndiyo elf sita nyingi sana. Ni bora uchukue ndugu zako wanufaike na kukusujudia kuwa wanafanya kazi kwa ndugu
Mkuu tusianzishe ligi,kila mtu anajua maisha yake yakoje na ndoto zake zikoje.kuna mtu anataman apate hata elfu moja tu kwa siku.wewe kama uko vizuri basi kaa kimya!
Pia kuhusu ndugu nilionao sio lazima kufanya nao maana kazi ni mtu yeyote yule ili mradi analipwa.
Mbona mimi siumwi? Naenda asubuhi narudi jioni nyumbani,
Nina 26 yrs, nimesoma chuo uhasibu ila mbona nafanya hii kazi? Na nimesomea hapahapa Dsm! Ukijielewa kazi ni kazi ili mradi ikutimizie mahitaji yako.
Ujasiriamali sio kitu rahisi,we kama umeajiriwa huko au una hela zako ni vizuri na sisi tunaanzia hukuhuku chini tutakutana mbele ya safari.
Pia sio kwamba hii kazi inafanywa na vijana wadogo kama unavodhani. Ni yeyote yule hata kama ni mkubwa au una status gani.mbona kuna wadada wazuri wanatembeza juice na uji n wanauza vizuri tu!!!
Anyway,sio kosa lako nisikulaumu!
Mimi nimesema atakayehitaji au kama mtu ana rafiki,ndugu n.k anaona anatafuta kazi tunaweza tukaja tukaungana n nikamlipa kulingana na mauzo.ni hayo tu
 
Wazo lako ni zuri sana, hongera kwa wazo hilo ila umetumia lugha ngumu na yenye dharau kwa vijana hao unaowahitaji.

Kumbuka vijana hao hawatumii mitandao kama hii, sasa ndugu zao wakiona lugha unayotumia inakuwa ngumu kuwapata.

Umenikumbusha jamaa mmoja aliwaajiri vijana 5,wakutembeza karanga. Aliwapangishia chumba chao akawawekea na TV, duh madogo walikuwa wanashindana kumaliza mzigo mapema. Maana anayewahi kumaliza ndiyo anarudi geto kucheck movie na mambo mengine.
 
Back
Top Bottom