Vijana wa kiume kwa mfumo huu uliopo nchini chukueni maamuzi magumu

Wamepigika sana hao wanawake/wasichana kwa HONGO TENDO.. yaani kwa rushwa ya ngono na sisi sisi wanaume tuliokuwaga madarakani na vijisecta fulani kwa kudai tendo ili tuwape kazi wameshika kijiti sasa ..waacheni
Kazi ipo
 
Vijana tegemezi wa kiume ambao ni graduates wanaongezeka sababu kazi zao zimeshikwa na dada zao wanaobebwa na mfumo wa Huyu ni Mwanamke, tumpe nafasi mwanamke, Haki sawa, Usishindane na mwanamke n.k.

Mabinti graduate wanapata kazi mapema kuliko vijana wa kiume, matokeo yake hata waoaji wanapungua kwa sababu ya uoga wa maisha ya majukumu ya ndoa na kuoa binti mwenye ajira aliyesoma.

USHAURI:
Vijana hakuna jinsi, tafuteni system nzuri ya kuingia mashambani. Serikali haiwezi kutoa ajira kwa wingi uliopo halafu binti wa kike anapewa kipaumbele kwenye ajira chache zilizopo. Huku mtaani hali ni mbaya. Vijana wengi ninaokutana nao wanahitaji msaada na si rahisi kuwasaidia wote.
Anayejua kuhusu ukweli wa Mr. Kuku farmers
 
Ukimuajiri mwanaume mmoja ni sawa na umesaidia familia tatu ila mwanamke anakuwa anajifikiria yy kama yy.
 
Ni kweli vijana wa kiume wajipage! Amasivyo hali yao itakuwa tete zaidi hapo mbele!!
 
Huko shambani kuna visingizio vingi sana mfano, mvua, sehemu ya kulima, mtaji na mwingine anaenda mbali na kusema hakuna soko la uhakika.

Ukisikia mwenye afadhali atakwambia yaani nina PhD nikalime!.
 
"vijana wa kiume!" ina maana huwa pia kuna "vijana wa kike"? mimi sijawahi kuwasikia...au ndio mabinti...basi mimi huwa nafikiri vijana ni mascuiline term.
 
Vijana tegemezi wa kiume ambao ni graduates wanaongezeka sababu kazi zao zimeshikwa na dada zao wanaobebwa na mfumo wa Huyu ni Mwanamke, tumpe nafasi mwanamke, Haki sawa, Usishindane na mwanamke n.k.

Mabinti graduate wanapata kazi mapema kuliko vijana wa kiume, matokeo yake hata waoaji wanapungua kwa sababu ya uoga wa maisha ya majukumu ya ndoa na kuoa binti mwenye ajira aliyesoma.

USHAURI:
Vijana hakuna jinsi, tafuteni system nzuri ya kuingia mashambani. Serikali haiwezi kutoa ajira kwa wingi uliopo halafu binti wa kike anapewa kipaumbele kwenye ajira chache zilizopo. Huku mtaani hali ni mbaya. Vijana wengi ninaokutana nao wanahitaji msaada na si rahisi kuwasaidia wote.
Ulichokiwaza wewe ata Mimi miaka miwili ilopita nlikiwaza ,,ila huu ni mpango maalumu uliosukwa muda mrefu Wa kuondoa mfumo dume ili huko mbeleni mwanamme ili aishi lazima apewe masharti Fulani Na wengi wao wataangukia ushoga ili wapate uafadhali Wa kujikimu
 
yani vijana hawa hawa ambao wanagombania poda na lip stick na dada zao? ama unamaanisha vinaja wa namna gani, taifa limepigwa na kitu kizito yaani vijana wanashindana na dada zao nani katokelezea sijui ili iwe nini anyway ngoja tuone , kimsingi tumepigwa
 
"vijana wa kiume!" ina maana huwa pia kuna "vijana wa kike"? mimi sijawahi kuwasikia...au ndio mabinti...basi mimi huwa nafikiri vijana ni mascuiline term.
Vijana limekaa kirika zaidi..vijana wakiume vijana wakike.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom