Vijana wa kiume huumizwa na mapenzi pia

affinitytz

JF-Expert Member
Feb 10, 2020
206
976
Anasimulia mdau,

Naandika uzi huu takribani miaka nane tangu nilipopokea ushauri huu kutoka kwa huyu jamaa ambaye nilikuwa nikimuita braza aliyekuwa amepanga karibu kabisa na nyumbani.

Ipo hivi, miaka fulani huko nyuma nikiwa chuoni mwaka wa tatu nilimtongoza binti fulani ambaye alikuwa akiishi jirani kabisa na nyumbani kwetu. Binti alielewa somo na kwa kweli nikaanza kula mema ya nchi bila hiyana.

Wakati huo binti ndio alikuwa amemaliza kidato cha sita na harakati za kujiunga chuoni zikaanza na mimi ndio nikawa kinara wa kutoa maelekezo na ushauri juu ya masuala ya kielimu kwa binti.

Binti akafanikiwa kupata chuo hapa hapa Dar na tuliamua apange nje ya chuo ili walau tuendelee kujinafasi na mapenzi yetu. Nikiri kwamba nilichangia sehemu kubwa ya malipo ya kodi ya awali.

Wakati huo mimi naelekea kumaliza mwaka wa nne, hivyo sikuwa na ratiba inayobana sana shuleni kwa semester ya kwanza na semester ya pili ni dissertation tu. Hivyo ilikuwa muda mwingi nipo chumbani kwa huyu binti yeye akiwa mwaka wa kwanza.

Hatimaye nikamaliza chuo huku mapenzi na binti yakiwa motomoto mpaka kuwekeana ahadi za ndoa.

Mambo yanaanza kubadilika.

Miezi kadhaa baada ya kumaliza chuo nikapa kazi ya temporary mkoani, kazi ilikuwa inalipa vizuri hivyo nikaanza kufanya mipango yangu huku nikimsapoti huyu binti kwa pesa za hapa na pale.

Baada ya muda nilipokuwa ninarudi kusalimia wazazi huyu binti akawa kama ananikwepa na kusema kwamba yupo tight sana na ratiba za shuleni.

Napata ushauri

Siku nikiwa nimerudi nyumbani kutoka mkoani na yeye akawa amekuja kusalimia wazazi wake, hatukuwa tumeonana kwa kipindi cha miezi miwili, nikiri kwamba alikuwa amenawiri na amevaa vizuri sana. Hata simu aliyokuwa anatumia wakati huo Nokia N90 ilinifanya niwaze mara mbilimbili.

Basi tukapata muda wa kukaa mahali(Baa ya jirani na nyumbani), nikaanza kumuuliza mbona kama amebadilika hivi na hauonyeshi kama ana thamini mahusiano yetu? Binti alikuwa anajibu kwa kifupi sana kwamba kila kitu kipo sawa. Nikamuomba kama tunaweza kwenda kulala kwenye kile chumba chake, binti akajibu kuwa hilo haliwezekani, nikamshawishi lakini ikashindikana.Muda wote alikuwa yupo bize na simu yake, hakuonyesha hayta cheme ya kuthamini kile nilichokuwa naongea.

Baadaye aliniaga kuwa kuna mahali anataka kwenda hivyo anaondoka. Hakuwa yule binti niliyeanza naye mahusiano akiwa bikra, mpole na mwenye staha, alikuwa amebadilika sana.

Alipoondoka wakati namalizia Seven Up yangu mezani ndipo huyu braza akasogea mezani kwangu na kuanza kuzungumza nami. Jamaa moja kwa moja akaniambia ‘’ mdogo wangu pale mapenzi yameshaisha’’ , nikamuuliza kwa nini, ndipo aliponiambia, ninawajua wewe na yule msichana jinsi mapenzi yenu yalivyokuwa moto lakini leo kwa namna mlivyokuwa mnaongea ni wazi kuwa binti ameshapata mtu mwingine ambaye inawezekana ana pesa kukuzidi.
Kabla sijaongea chochote braza akaendelea kusema, kwa sasa unaweza kufanya jambo moja tu japo ni ngumu sana, jaribu kum-ignore( kumpuuza), usimtafute kwenye simu, na ikitokea amekupigia usianze kujilalamisha wala kumuuliza maswali juu ya mahusiano yenu. Jamaa alinisisitiza kuwa kwa muda huo mimi nikomae na maisha yangu kwa kuwa wanawake wapo tu.

Sikuwa namuelewa.

Nikiri wazi wakati wote huu, nilikuwa nahisi uchungu sana moyoni, nikikumbuka mambo niliyofanya na huyu binti halafu leo amenigeuka namna hii. Braza akapigilia msumari wa mwisho kwa kusema ameshuhudia mara kadhaa huyu binti akiletwa kwao anapokuja kusalimia kwa gari. Na jamaa anayemleta huwa anakaa kwenye baa mpaka muda binti anapoaga kurudi chuoni.

Baada ya mazungumzo na braza nikarudi nyumbani huku nikihisi kuchanganyikiwa, niliwaza mengi sana lakini mwishoni nikaona nimpigie simu binti ili walau nimuulize kama ana bwana ili walau nimwambie kwamba mimi na yeye basi( kosa namba moja).

Nikapiga simu, ikaita na haikupokelewa kabisa. Nikaona ngoja niandike meseji ‘’ Mimi na wewe naomba tuachane maana sikuelewi’’ hazikupita sekunde tano nikapokea meseji fupi iliyosomeka ‘’ok’’. Nilisoma meseji ile zaidi ya mara tano, nikahisi baridi na kichwa kikaanza kuuma. Nikiwa nimeduaa, machozi yalianza kutirirka, nilibaki chumbani kwambu mpaka majira ya saa mbili ambapo nilitoka ili kula pamoja na familia.

Niliamka asubuhi na kurudi Mkoani kuendelea na kazi, ilikuwa safari ndefu sana maana kila wakati sura ya huyu binti ilinijia.

Nikiwa mkoani nikaamua niingie kwenye ukurasa wa facebook wa huyu binti, kweli jamaa alikuwa akimpa maisha ambayo sikuwahi kumpa, mara amepost wanakula kwenye migahawa yenye hadhi mjini, nakumbuka picha aliyopiga wakiwa wanakula pale Lemon Tree Restaurant nadhani Quality Centre ilipokuwa kwenye ubora wake, nmara wapo Fairly Delight pale mlimani city. Nikafikia hitimisho kuwa jamaa ananizidi hela na binti amefanya maamuzi ili afurahie maisha.

Tatizo namba mbili lilikuwa rafiki zangu ambao walikuwa wanajua kuwa mimi na binti tulikuwa na mahusiano. Nilipewa maneno mengi ya kejeli na dharau, iliniuma sana.

Naamua kuzingatia ushauri wa braza

Miezi kadhaa baadaye wakati bado nikiwa na uchungu moyoni nikaamua kutaka kumsahau kabisa huyu mwanamke. Haikuwa kazi rahisi, lakini nilijiangalia mimi mwenyewe pamona na wazazi wangu waliokuwa wananitegemea. Nikaapa kwamba mimi sitakaa tena kuhuzunika kwa mahusiano yaliyovunjika na huyu binti.

Nikaacha kabisa namna yoyote ya mawasiliano na kufuatilia ukurasa wake wa facebook.
Nikachoma picha, kadi na chochote ambacho kingenikumbusha huyu binti
Nikaanza rasmi kutafuta mchumba ili nioe

Mama yangu aligundua nilichokua napitia, nakumbuka siku moja usiku akanipigia simu na kuniambia, pole sana mtoto wangu, lakini ndio ukubwa huo, vumilia maana ipo siku utasahau, tafadhali usifanye jambo lolote la kijinga.

Kufupisha stori;
Hatimaye nikaoa mwaka mmoja baadaye na maisha yakaendelea.

Yule binti mwaka jana akahamia karibu kabisa na ninapoishi, ameolewa pia lakini sio na yule jamaa bali na mtu mwingine.
Nieleze wazi sina uadui na huyu binti kwa sababu amefanya nimepata mke bora sana.

Lengo la kuandika yote haya ni;-

1. Wanaume pia tunaumizwa sana na mahusiano japo huwa tunakomaa kimya kimya
2. Huna haja ya kujenga uadui na mpenzi wako wa zamani hata kama alikucha kwa nyodo.
3. Wazazi wetu huwa wanajua tunachopitia na huwa wanaumia pamoja nasi.
Mahusiano yakifika mwisho kubali usilazimishe.
4. Dada kama umeona kijana wa watu sio kiwango chako, walau mwambie tu ili muachane kwa usalama.
5. Usiwekeze muda na mali kwa mpenzi, kijana wa kiume jenga maisha yako kwanza.
 
Nmekuelewa sana,, ila ambaye hajawahi kuumizwa hawezi kukuelewa hata kidogo.

Kuumia ni sehemu ya mapenz na yanakomaza sana akili kuingia utu uzima,,
 
Niseme tu pole mkuu, niliyapitia na kuyaishi maisha hayo ya kumpenda mtu then akapata mwingine na wewe kuonekana kama boya tu, hakika inauma sana,
Ila ajabu na kweli wanawake hao hao hurudi na kupiga magoti wakiomba msamaha,
Zaidi katika msamaha huwa najibu, ngoja nifikirie kwanza nitakujibu, na sasa ni zaidi ya mwaka wa sita huwa akinikumbuka na kuuliza namwambia bado nafikiria,,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom