Naomba sana mleta uzi aisome hii comment.

No offense ila mkuu nabid uelewe nyie wanawake mko too quick to judge, hasa pale mnapoona hakuna kitu kinafanyika wakati huo.
Kingine hua ni wepesi kuamin katika kitu kinachoonekana wakati huo kwa mtu flani kuliko kitu ambacho mtu anafanya for the sake of 10-20 years na bado hakijaanza kuonekana au kuleta matunda.
Elewa hili Mama, mipango ya mwanaume na mwanamke haijawah kua sawa.
With women, wao ni rahisi kujiengage na petty jobs na wakaonekana wapambanaji kwa sababu mwisho wa siku wao sio providers (in nature), at the end of the day anajua tu kuna mwanaume atakuja kutake responsibilities za muhimu zaidi.
Few women pekee ndo hua hawamtegemei mwanaume kwenye issue za maana na zinazohitaji attention kubwa.
Mwanaume anapopanga mipango yake lazima aangalie miaka isiyopungua mi5 mbele.
Cause sooner or later atakua provider.
Graduate or not, ndivyo mwanaume alivyo.
Soo sisi tunapoweka malengo au mipango hua inachelewa sana kuonyesha/kuleta matunda cause we only have us, ourselves to get shit done, unlike nyie wanawake, kutusua ni mara mmoja cause hua mnakutana na huruma za hapa na pale za wanaume kuwafanya mtoboe mapema plus mna kitega uchumi binafsi.
Lakin ukweli usemwe, ni very few women wana hustle ila hustle from 0 bila msaada au favors zozote na wakatoboa.
Sisi hua hatupati hizo.
Soo huyu dogo, usione anaamka saa 5 na akaonekana hafanyi kitu ukamdharau, hujui kichwan mwake ameweka malengo gan au ni kitu gan anaplan kukifanya ambacho bado/kimtachukua muda mpaka aone/uyaone matunda yake.
Tena mbaya zaidi usiombe awe anafanya mishe zake kimyakimya, tena zile ambazo hazikupi clue, unamuona boya tu. Be very afraid Madam. He's keeping records from how everyone is treating him through these hard times.
Wanasemaga mwanaume halali njaa ila anachelewa tu kula.
Simply becuase huyo dogo haoneshi hustles zozote now haimaanishi ni mzembe au anaplan ya kua hivyo forever. Never.
Be kind to him, give him time, and let him be.
10 years down the road, utakuja kuelewa na itamake much sense.
Usimhukum kwa hapo alipo, ni transition tu hio anapitia.
Shukuru tu kua umebarikiwa kua part ya his transition, you'll be rewarded accordingly siku mmoja kwa ukarimu wako kwake, kama ni mtu anayejielewa.
Narudia, usimjudge. Let him be.
 
Yani Huyo Mdogo Wako Cjui Shangazi Yako Ndo Iwe Njia Ya Kutoa Mashambulizi? Umekurupuka Na Inaonekana Ww Akili Yako Inafanya Kazi Kwa Hisia. Wote Tuna Macho Na Tunaona Tunavotoka Jasho Kutafuta Mkate Wetu Wa Kila Siku.

Ulitakiwa Uje Na Mada Kumsema Huyo Mdogo Wako, Unamdekeza Mwenyewe Halafu Unabweka Huku Shenzi Taip
 
Hivi ndio namna tunatakiwa tuishi na hawa vijana wenzetu! Sasa unakuta dume zima lina support malaya ila kumpa ramani mwanaume mwenzie anaona uchawi ila kwenye thread humu anashupaza koromeo ooh vijana wavivu! Watu wapo tayari kuwajibika ila kazi ziko wapi sasa?

Haingii akilini graduate ukurupuke tu kubeba jiko la kahawa na kashata! Mzazi wako anaweza kuona umeshadata ukamuua kwa presha esp. kama ndiye jembe lake analolitegemea!

Well said Chief eti ukurupuke tu kubeba jiko la kahawa umeniacha hoi sana hapo
 
Habari za jumapili wana Jamii Forum

Leo naomba nizungumze kidogo na hawa wenzetu upande wa Kiume mana miaka ijayo kuna hatari ya kupoteza nguvu kazi

Siku izi ni kawaida kabisa kukuta mdada anauza matunda, anatembeza mtumba, anachoma mandazi ubuyu na juice na mengine mengi ya kuingiza kipato, huko kwenye vikoba ndo usiseme wanawake wameamua kutafuta hasa tofauti na zamani

Lakini upande wa pili kuna uvivu na kujisahau ambapo trend ikiendelea hivi kuna hatari kubwa mbeleni
Wanaume hasa hawa wanaojiita graduate mnapotea kaka zangu, najua mmesoma bodaboda mnaona si hadhi zenu tena, saidia fundi pia siyo hadhi yenu kuuza matunda siyo hadhi yenu mmebaki mnatembea na bahasha kutwa kutafuta kazi, ebu ndugu zangu acheni u brazamen wa kishamba, jichanganyeni hakuna pesa inakuja kukugongea mlango lazima tu uitolee jasho kidogo, mbona wadada wazuri tu wanajishughulisha??

Kuna mtoto wa ndugu yangu alifikia kwangu ili aende interview jamani anaamka saa tano akiamka anaamka na laptop na muvi, anakunywa chai anaendelea na muvi mchana anakula anaendelea na muvi narudi nyumbani nipo hoi bin taaban yeye hata kuoga ajaoga,saa mbili na nusu tunakula dinner ndo anamwambia dada akampashie maji ya kuoga hivi huyu mtu hata akipata kazi si mzigo huu??????

Huu ni mfano lakini wanaume wa aina hii ni wengi sana

Wakati ambapo dunia ipo busy kuimpower mtoto wa kike hebu Wazazi wekeni juhudi kidogo na kwa watoto wa kiume, wajitambue na kuwafundisha kufanya kazi kwa mikono yao wenyewe.

Ni aibu sana

Baba yetu alikuwa mkoloni kweli yani ukichelewa kuamka asubuhi tu ilikuwa kuamka ni Saa kumi na mbili asubuhi ata siku za wiki endi, sasa siku Moja kaka yetu alichelewa kuamka, akalala mpaka Saa Moja asubuh baba akamfungia mlango na ufunguo na kuondoka na funguo wa chumba kaka alikaa chumban kuanzia asubuh mpka Saa nne usiku,, bila kunywa maji wala kula chakula, sisi tukawa tuna mchingulia tu dirishai, daaah wazee wa zamani walikuwa wakoloni kwel.
 
Naomba sana mleta uzi aisome hii comment.

No offense ila mkuu nabid uelewe nyie wanawake mko too quick to judge, hasa pale mnapoona hakuna kitu kinafanyika wakati huo.
Kingine hua ni wepesi kuamin katika kitu kinachoonekana wakati huo kwa mtu flani kuliko kitu ambacho mtu anafanya for the sake of 10-20 years na bado hakijaanza kuonekana au kuleta matunda.
Elewa hili Mama, mipango ya mwanaume na mwanamke haijawah kua sawa.
With women, wao ni rahisi kujiengage na petty jobs na wakaonekana wapambanaji kwa sababu mwisho wa siku wao sio providers (in nature), at the end of the day anajua tu kuna mwanaume atakuja kutake responsibilities za muhimu zaidi.
Few women pekee ndo hua hawamtegemei mwanaume kwenye issue za maana na zinazohitaji attention kubwa.
Mwanaume anapopanga mipango yake lazima aangalie miaka isiyopungua mi5 mbele.
Cause sooner or later atakua provider.
Graduate or not, ndivyo mwanaume alivyo.
Soo sisi tunapoweka malengo au mipango hua inachelewa sana kuonyesha/kuleta matunda cause we only have us, ourselves to get shit done, unlike nyie wanawake, kutusua ni mara mmoja cause hua mnakutana na huruma za hapa na pale za wanaume kuwafanya mtoboe mapema plus mna kitega uchumi binafsi.
Lakin ukweli usemwe, ni very few women wana hustle ila hustle from 0 bila msaada au favors zozote na wakatoboa.
Sisi hua hatupati hizo.
Soo huyu dogo, usione anaamka saa 5 na akaonekana hafanyi kitu ukamdharau, hujui kichwan mwake ameweka malengo gan au ni kitu gan anaplan kukifanya ambacho bado/kimtachukua muda mpaka aone/uyaone matunda yake.
Tena mbaya zaidi usiombe awe anafanya mishe zake kimyakimya, tena zile ambazo hazikupi clue, unamuona boya tu. Be very afraid Madam. He's keeping records from how everyone is treating him through these hard times.
Wanasemaga mwanaume halali njaa ila anachelewa tu kula.
Simply becuase huyo dogo haoneshi hustles zozote now haimaanishi ni mzembe au anaplan ya kua hivyo forever. Never.
Be kind to him, give him time, and let him be.
10 years down the road, utakuja kuelewa na itamake much sense.
Usimhukum kwa hapo alipo, ni transition tu hio anapitia.
Shukuru tu kua umebarikiwa kua part ya his transition, you'll be rewarded accordingly siku mmoja kwa ukarimu wako kwake, kama ni mtu anayejielewa.
Narudia, usimjudge. Let him be.
Mkuu, hakuna maajabu sisi wenyewe tuko mtaani humu humu tunaona.

Huko vyuoni tumesoma na vijana wa nchi hii tunajuana.

Kitu pekee ambacho bado kinatusaidia wabongo ni roho ya ujamaa tuliyonayo.

Huna hata mia, lakini unaweza kwenda kukaa kwa ndugu, kupiga vizinga washkaji, kula bure, kuoga.

Lakini kila mtu akikaza, hakika nakwambia utapambana kivyovyote uweze kuishi.

Na hii ndio sababu watu hasa wa Dar ni ngumu kutoka nyumbani. Being used to comfort zones.
 
Baba yetu alikuwa mkoloni kweli yani ukichelewa kuamka asubuhi tu ilikuwa kuamka ni Saa kumi na mbili asubuhi ata siku za wiki endi, sasa siku Moja kaka yetu alichelewa kuamka, akalala mpaka Saa Moja asubuh baba akamfungia mlango na ufunguo na kuondoka na funguo wa chumba kaka alikaa chumban kuanzia asubuh mpka Saa nne usiku,, bila kunywa maji wala kula chakula, sisi tukawa tuna mchingulia tu dirishai, daaah wazee wa zamani walikuwa wakoloni kwel.
Yaani kuna wazee wa zamani ukishakua mtu mzima: siyo mwanafunzi tena, linakufukuza kwake🤣

Linakwambia unakaa kwangu mkmi siku nikishindwa hapa nikimbilie wapi, katafute na wewe.

Na wale wazee wenye ng'ombe ukishatahiriwa tu ukapona, kifuatacho ni wewe kwenda kujenga huko porini na unaozeshwa na kupewa ng'ombe wa kuanzia.
 
Huu ndio mfumo ambao unatumiwa na wazee hata wakisasa ili kuwaandalia future watoto wao! Kama ni biashara basi baada ya shule unakaa dukani unaelekezwa nini cha kufanya. Mzigo tunanunua wapi na tunauzaje. Hizi ndio basics ndio maana watoto wa wafanyabiashara hawana maisha magumu baada ya kumaliza vyuo!

Shida ni kwa wazazi ambao wao elimu ya mkoloni ndio iliwatoa wanaamini kuwa elimu ndio mkombozi wa maisha! Stigmatization kuwa ukiwa nje ya professional industry wewe ni kiazi hio ndio imemaliza graduates kabisa!
 
FACT!!!
 
Kule Jei Kei Tii vipi hakujasaidia vijana wetu graduates kujiajiri si walikuwa wanafanya kazi ngumu ngumu amaaa!?

Ila wakuu pooltable na mashine ya mchna vinayo hela acheni kabisa
 
Nyinyi mnaongelea wavulana na si wanaume,umeshaambiwa mwisho wa usharobaro ni majukumu,unachokosea wanaume unawafananisha na vijana
 
Mtoa mada ,mtoa mada umeangalia kwa makini au umeandika andika tu?, umeshawai kumuona mwanamke akiuza ice cleam za bakhresa kwa vile vibaiskeli? Umekwenda pale buguruni ukute vijana wangapi wa kiume wanafanya kazi za kupakia ngano , ushawai kukuta gari za pespi ,koka, au za kusambaza maji wanapakia au kushusha wanawake. Ushawai unajua waendesha bajaji asilimia kubwa ni wanaume, unajua boda boda wengi wanaume ,unajua makondacta na madeleva wa daladala wengi wanaume, ukija na hoja fanya tasmini kwanza sio unakuja kubwabwajatu, kama ulikuwa hujui mwaka huu ndio tumepata rais nwanamama huko kote tulikuwa na marais wa wanume

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwanamke akishapata visenti anaona wanaume kama mgambo
 
Naomba sana mleta uzi aisome hii comment.

No offense ila mkuu nabid uelewe nyie wanawake mko too quick to judge, hasa pale mnapoona hakuna kitu kinafanyika wakati huo.
Kingine hua ni wepesi kuamin katika kitu kinachoonekana wakati huo kwa mtu flani kuliko kitu ambacho mtu anafanya for the sake of 10-20 years na bado hakijaanza kuonekana au kuleta matunda.
Elewa hili Mama, mipango ya mwanaume na mwanamke haijawah kua sawa.
With women, wao ni rahisi kujiengage na petty jobs na wakaonekana wapambanaji kwa sababu mwisho wa siku wao sio providers (in nature), at the end of the day anajua tu kuna mwanaume atakuja kutake responsibilities za muhimu zaidi.
Few women pekee ndo hua hawamtegemei mwanaume kwenye issue za maana na zinazohitaji attention kubwa.
Mwanaume anapopanga mipango yake lazima aangalie miaka isiyopungua mi5 mbele.
Cause sooner or later atakua provider.
Graduate or not, ndivyo mwanaume alivyo.
Soo sisi tunapoweka malengo au mipango hua inachelewa sana kuonyesha/kuleta matunda cause we only have us, ourselves to get shit done, unlike nyie wanawake, kutusua ni mara mmoja cause hua mnakutana na huruma za hapa na pale za wanaume kuwafanya mtoboe mapema plus mna kitega uchumi binafsi.
Lakin ukweli usemwe, ni very few women wana hustle ila hustle from 0 bila msaada au favors zozote na wakatoboa.
Sisi hua hatupati hizo.
Soo huyu dogo, usione anaamka saa 5 na akaonekana hafanyi kitu ukamdharau, hujui kichwan mwake ameweka malengo gan au ni kitu gan anaplan kukifanya ambacho bado/kimtachukua muda mpaka aone/uyaone matunda yake.
Tena mbaya zaidi usiombe awe anafanya mishe zake kimyakimya, tena zile ambazo hazikupi clue, unamuona boya tu. Be very afraid Madam. He's keeping records from how everyone is treating him through these hard times.
Wanasemaga mwanaume halali njaa ila anachelewa tu kula.
Simply becuase huyo dogo haoneshi hustles zozote now haimaanishi ni mzembe au anaplan ya kua hivyo forever. Never.
Be kind to him, give him time, and let him be.
10 years down the road, utakuja kuelewa na itamake much sense.
Usimhukum kwa hapo alipo, ni transition tu hio anapitia.
Shukuru tu kua umebarikiwa kua part ya his transition, you'll be rewarded accordingly siku mmoja kwa ukarimu wako kwake, kama ni mtu anayejielewa.
Narudia, usimjudge. Let him be.
 
Tatizo kubwa lipo kwenye jamii sio vijana.. yani kijana akimaliza chuo akaendesha bodaboda au kufanya Kazi ya saidia fundi watu wengi huanza kusema vibaya kumchukulia kama kitendo cha kwenda shule alipoteza muda.. na hakuna maarifa aliyo yapata ya ziada tofauti na walio baki mtaani hii kitu sio kizuri kwenye jamii yetu, na ndo kimefanya vijana wengi wajifungie majumbani.

Yani ili nchi iendelee inatakiwa tujifunze kuwasifia watu wanao kujituma kufanya Kazi kwa bidii hata kama ikiwa ni Kazi ya kuzibua choo.. na kingine pia tujifunze kwa nchi zilizo endelea.

Jamii yetu inaona kama mtu ukimaliza kusomea Uhandisi ukaenda kulima au kujiajiri katika fani tofauti unakuwa umepotea.. kwa mtazamo wangu kitu kikubwa kinacho kwamisha vijana ni majungu kutoka kwenye jamii.

Mfano niulize tu.. ni wazazi wangapi wataruhu mwanao aliesomeshwa kwa gharama mpaka chuo akawe bodaboda,saidia fundi, au hata kuwa mpishi mgahawani?? Wazazi kama mpo humu naomba mjibu kwa uwazi kabisa
Hakika umenijibia. ila ushauri wa dada vijana tumeupokea.
 
Habari za jumapili wana Jamii Forum

Leo naomba nizungumze kidogo na hawa wenzetu upande wa Kiume mana miaka ijayo kuna hatari ya kupoteza nguvu kazi

Siku izi ni kawaida kabisa kukuta mdada anauza matunda, anatembeza mtumba, anachoma mandazi ubuyu na juice na mengine mengi ya kuingiza kipato, huko kwenye vikoba ndo usiseme wanawake wameamua kutafuta hasa tofauti na zamani

Lakini upande wa pili kuna uvivu na kujisahau ambapo trend ikiendelea hivi kuna hatari kubwa mbeleni
Wanaume hasa hawa wanaojiita graduate mnapotea kaka zangu, najua mmesoma bodaboda mnaona si hadhi zenu tena, saidia fundi pia siyo hadhi yenu kuuza matunda siyo hadhi yenu mmebaki mnatembea na bahasha kutwa kutafuta kazi, ebu ndugu zangu acheni u brazamen wa kishamba, jichanganyeni hakuna pesa inakuja kukugongea mlango lazima tu uitolee jasho kidogo, mbona wadada wazuri tu wanajishughulisha??

Kuna mtoto wa ndugu yangu alifikia kwangu ili aende interview jamani anaamka saa tano akiamka anaamka na laptop na muvi, anakunywa chai anaendelea na muvi mchana anakula anaendelea na muvi narudi nyumbani nipo hoi bin taaban yeye hata kuoga ajaoga,saa mbili na nusu tunakula dinner ndo anamwambia dada akampashie maji ya kuoga hivi huyu mtu hata akipata kazi si mzigo huu??????

Huu ni mfano lakini wanaume wa aina hii ni wengi sana

Wakati ambapo dunia ipo busy kuimpower mtoto wa kike hebu Wazazi wekeni juhudi kidogo na kwa watoto wa kiume, wajitambue na kuwafundisha kufanya kazi kwa mikono yao wenyewe.

Ni aibu sana

Fimbo zirudi.
 
hata hapa wapo wengi sana,, na wako busy kupost upuuzi...mie nlipomaliza chuo nakumbuka niweka vyeti kabatini nikatoka kutafuta vibarua....tena vile vya kuvizia kwa gate.....nyapara linakuja linachagua kama 5 mnaingia ndani...ukibahatika unaambiwa kesho uingie...na kitamburo unapewa.......nilisota pale wiki.......aiseee Mungu sio athumani.....pale mimi ndio nilitoka direct......conection initik inside, kuleta vyeti nikaambiwa wewe utaenda kuwa manager wa branch mpya dsm.......hawa vijana ukiwaambia wanaona ni zuga....kubet,,,uchambuzi wasoka ....akirudi nyumbani ...ni bora kuku atataga ule yai....brake ya kwanza jikoni....duh....ila wazazi ndio tumewafikisha hapo
 
Back
Top Bottom