Mr pianoman
JF-Expert Member
- May 22, 2019
- 2,548
- 6,102
Kwako mheshimiwa Rais Mama Samia ni muda sasa na huu upande wa majeshi nao ukumbukwe kupewa ajira ambazo moja kwa moja zinawahusu hawa vijana wetu walio jitolea huko jeshi la kujenga taifa (jkt) kwa miaka isiyo pungua mitatu.
Vijana wamejitolea na wengine bado wanaendelea kujitolea wapewe na wao ajira kama wapewavyo walimu kila kukicha kwani bila kificho majeshi mengi yanaupungufu wa askari kwa kiasi kikubwa sana kwani tunaona kila siku majeshi tofauti tofauti yakiomba ajira mpya.
Imefika wakati sasa sisi wananchi tunaambiwa tuanze kujilinda kupambana na wezi na majambazi kwa sababu askari polisi hawatoshi hii imekaaje wakati tuna vijana wengi tu ambao kila kukicha wanarudishwa nyumbani kutoka JKT?
Mwananchi leo katoka kwenye shughuli zake mchana kutwa amerudi nyumbani badala apumzike kwa majukumu ya kesho inambidi tena akeshe doria usiku kupambana na wezi, vibaka na majambazi sisi taaluma hiyo hatuna mheshimiwa Rais.
Au nyie wananchi mnasemaje tutoke kwenye majukumu ya kutwa nzima kisha usiku tuingie doria au vijana wetu waajiriwe ili sisi tuendelee kulipa kodi?