Kwenye video zinazosambaa mitandaoni zikiwaonyesha vijana wa Wilaya ya Hai wakifanya fujo, pamoja na makosa mengine ya jinai, "kufanya fujo na kuharibu mali", wamesikika wakisema hawataruhusu mtu yeyote asiye mwana Hai kukanyaga eneo lao na kufanya siasa au jambo lolote lisilowahusu wana Hai.
Hili ni kosa kisheria kwa Sheria ya 1984 Na.15 ib.6. "Uhuru wa mtu kwenda atakako", vile vile wamevunja Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 17, "Haki ya Kuishi".
Ibara ya 17.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.
Ni wito wangu kwa vyombo vya dola kuwatafuta vijana hawa na walio nyuma yao na kuwapeleka kwenye vyombo husika ili sheria ichukue mkondo wake.
Hali hii ikiachwa iendelee kuna siku watu wa eneo fulani watajitangazia mamlaka ya eneo lao ndani ya Jamhuri ya Tanzania.