Vijana wa Hai waliotangaza kutawala eneo lao wanaweza kushitakiwa kwa kuvunja Katiba Ibara ya 17

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Kwenye video zinazosambaa mitandaoni zikiwaonyesha vijana wa Wilaya ya Hai wakifanya fujo, pamoja na makosa mengine ya jinai, "kufanya fujo na kuharibu mali", wamesikika wakisema hawataruhusu mtu yeyote asiye mwana Hai kukanyaga eneo lao na kufanya siasa au jambo lolote lisilowahusu wana Hai.

Hili ni kosa kisheria kwa Sheria ya 1984 Na.15 ib.6. "Uhuru wa mtu kwenda atakako", vile vile wamevunja Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 17, "Haki ya Kuishi".

Ibara ya 17.-(1) Kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika Jamhuri ya Muungano na kuishi katika sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa kutoka katika Jamhuri ya Muungano.

Ni wito wangu kwa vyombo vya dola kuwatafuta vijana hawa na walio nyuma yao na kuwapeleka kwenye vyombo husika ili sheria ichukue mkondo wake.

Hali hii ikiachwa iendelee kuna siku watu wa eneo fulani watajitangazia mamlaka ya eneo lao ndani ya Jamhuri ya Tanzania.
 
Hayo ni mambo yaliyo achwa yaratibiwe na muhuni Ole Sabaya. Lengo kuu ni kumharasi Mbowe kama mpango rasmi ulioanzia juu.
Fujo za Jana zilisababisha vijana wa Sabaya wapokee kipigo, lakini kwa BAHATI MBAYA yule ambaye ilikuwa afe ili iwe fundisho kwa Sabaya hakufa. Sasa kuliko afe kijana anayefanya Fujo kwa 20,000/ zitokazo kwa Ole Sabaya bora afe mwenyewe na uteuzi mpya ufanyike.
 
Tatizo vyombo vyetu vya ulinzi vimesahau wajibu wao na kufanya kazi kwa kufuata matakwa ya wanasiasa (CCM)
 
Wanelushwa michembe na DJ mbowe,ngoja waonje joto la jiwe,ni kupoteza mmoja baada ya mwingine
 
Hiyo ndio speciality ya Sabaya, ndio maana muda wote amezungukwa na wahuni. Concern yangu ni kuwa hakuna wa kumfunga paka kengele. Doomed
 
Mambo yakijinga sana. Tunachekea ujinga wa hivi ila iko siku utatugharimu na tutakua tumechelewa.
 
Kwenye video zinazosambaa mitandaoni zikiwaonyesha vijana wa Wilaya ya Hai wakifanya fujo, pamoja na makosa mengine ya jinai, "kufanya fujo na kuharibu mali", wamesikika wakisema hawataruhusu mtu yeyote asiye mwana HAI kukanyaga eneo lao na kufanya siasa au jambo lolote lisilowahusu wana HAI...
Ambao walipaswa kuwachukulia hatua ndio waliowatuma na kuwalipa
 
Nimengalia vizuri hii clip wale ni mateja na jobless na baadhi ya vijana wenye matatatizo mbalimbali ya kimaisha yaliyotengenewa na ccm makusudi kisha wanageuza matatizo kuwa mtaji wa kisiasa ujinga mtupu yaan machalii wamekaririshwa name yakuongea ukiwaangali vizuri wako hoi kiafya wananjaa sura zimekosa nuru. Kinaja usikuba kutumika
 
Kwenye video zinazosambaa mitandaoni zikiwaonyesha vijana wa Wilaya ya Hai wakifanya fujo, pamoja na makosa mengine ya jinai, "kufanya fujo na kuharibu mali", wamesikika wakisema hawataruhusu mtu yeyote asiye mwana HAI kukanyaga eneo lao na kufanya siasa au jambo lolote lisilowahusu wana HAI..
Umwewahi kumwona Mgogo anamiliki shamba Hai, Bukoba, au Mbeya?

Sent from my XT1097 using JamiiForums mobile app
 
Vijana wa Hai komaeni hapohapo mlipowashika.Chenka ndo kidoogo alikua akipunguza spidi. Chenka keshatangulia mbele ya haki kwa sasa ni spana spana tu mwanzo mwisho.
 
Back
Top Bottom