Vijana wa ' Dot Com ' hivi ' mmerogwa ' na nani hadi hamuigi nidhamu za Sisi tuliowatangulieni kuliona hili jua?

Na nitazipanda hadi Siku yangu ya Kufa Mkuu. Hivi wote tukiwa na Magari na Sisi tusiokuwa nayo ' tutachekwa ' na ' kudhihakiwa ' vipi na Matajiri na mlionayo kama Wewe / Nyie? Mimi GENTAMYCINE siyo tu kwamba napanda ' DalaDala ' kwakuwa sina Gari bali hata Hela / Pesa tu nazo sina na naishi tu ' Kimkandamkanda ' ila nashukuru kuwa napumua na nina Uhai huu.
Wahi Lumumba bukubuku zipo kibao mradi tafuta kapelo hata lililochakaa, haya yaliyochakaa mitaani yapo mengi tu, vaa, nakwambia hukosi kitu.
 
JANA KUNA VIBINTI VYA FORM TWO VILILAZIMISHWA KUNIPISHA SITI NA KONDA VILIONGEA NJIA NZIMA
 
nao watoto ni wakuhurumiwa.....mtu mzima nawe uwe mwenye huruma kwa wadogo.....muwaonyeshe upendo...mi nlisikiaga dar hakuna shikamoo so unaweza kusema shikamoo ukajibiwa poa mambo......vijana tuwapishe wale wenye uhitaji wa kusaidiwa ndio thawabu zenyewe...jili limekaa kiimani na utu wa mtu so sio kulazimishwa mana nae kalipa nauli kosa nila wewe uliyepanda ungali umeona siti zimejaa hivyo kupanda kwako umerizia kusimama ambapo pia kisheria n kosa......kijana hata mzazi wake mwenyewe hamuwezi vp wewe tuliokutana kwa daladala na huenda tusikutane tena labda akhera....Mjini huruma imekaa kushoto kila mtu anapambana na hali yake.Tamaduni nyingi zimevunjwa sio iyo tu ya huko daladalani kitaa pia kubovu...nawasilisha
 
Nyie mnaolilia kupishwa kwenye madaladala si mnunue magari yenu ebooo
 
Anayetakiwa kuachia siti ni denti tu kwa sababu analipa nauli ndogo. Ila abiria aliyelipa nauli kamili ana haki ya kukalia siti. Hiyo adabu unayoisema hata zamani haikuwepo kivile.

Sema kwa sasa hivi tatizo lipo kwenye Mwendokasi kwa kuwa hakuna kondakta wa kuwanyanyua, madentii huwa wanakaa tu huku tuliolipa nauli kamili tumesimama. Mi nikionaga denti jirani yangu amekaa namwambia, "Oya mwanafunzi pisha kiti."

Lakini abiria wengi hawako confrontational. Wanaogopa anaweza akasema hivyo halafu akajibiwa vibaya. Kwa hiyo inatakiwa kampuni ya Mwendokasi iweke audio recording ya kuwaagiza wanafunzi kuwapisha watu wazima iwe inaplay basi linapoondoka kwenye kila kituo.
 
Kwa hyo mwanafunz hapaswi kukaa?
 
Enzi zangu zipo o level azaboi nauli 50 na siti nakalia kama kawaida.....kuna watu wazima wengine ovyo sana unakuta mwanafunzi ananyanyaswa na konda yeye kajikausha kimya kisa amekaa mwengine anakwmbia ww acha ubishi panda gari nyingne.........kuna ile unampsha mtu situ hafu anaanza nyodo hatakwi kuguswa/kuegemewa hatk kuwasaidia mizigo abiria wengine yhn mwendo wa mikazo tena mm nakukazia sura hata sina haj ya kuzuga aibu utaona ww.
 
Kuna siku nilijaribu kumuuliza kijana mwenzangu,ili nione atatoa maoni gani kuhusu ili jambo alicho nijibu nilichoka,kwanza aliniambia kwamba wazee wa skuizi wanazingua wanachukua vibinti au vijana lika letu,na hii ndio ikaonekana sababu kubwa ya kuwawekea uso wa mbuzi wazee kwenye daladala.
Dah yaan kama uliona hili tukio langu!
Imetokea juzi natokea Chanika kuna Bi mkubwa nimepanda nae pale Taliani tena anaonekana ni mbovu wa miguu masikini ya Mungu, watoto wa kike na kiume wanamuangalia tu Bi mkubwa kashika bomba, ROHO ILINIUMA SANA!!! amekuja kupata siti tumefika Airport tena kwa kumuomba dada mmoja alikuwa akiiwahi ile siti nikamuomba amsaidie Bi mkubwa akae tafadhali, ndio kwa aibu akampisha, Dunia imebadilika sana hawa watoto wa sasa hivi hawana heshima wala adabu!!!
 
Ila ni kweli nimeshuhudia ili jambo mara nyingi sana.
Enzi zangu zipo o level azaboi nauli 50 na siti nakalia kama kawaida.....kuna watu wazima wengine ovyo sana unakuta mwanafunzi ananyanyaswa na konda yeye kajikausha kimya kisa amekaa mwengine anakwmbia ww acha ubishi panda gari nyingne.......
 
Kama kuna Mtu / Abiria wa ' DalaDala ' ambaye mara kwa mara huwa ' anagombana ' na Vijana na Mabinti wa Kizazi hiki ( mnakiita cha Dot Com ) kwa nidhamu zao ' mbovu ' za ama kutowaamkia Wakubwa zao au Kuwapisha Viti wakae basi ni Mimi.

Hamuwezi amini Mimi pamoja na ' Uhenga ' wangu huu wote nikiwa tu ndani ya ' DalaDala ' nikikutana tu na Mtu mzima Kwanza huwa nawahi Kumsalimu na kama nikiona Siti hakuna au zimejaa basi bila hiyana huwa nawapisha wakae.

Inasikitisha sana pale unapomwona Kijana / Binti akikutana tu na Mtu Mzima ndani ya Usafiri huo wa ' DalaDala ' wala hasalimii na kibaya zaidi hata mshipa wa aibu wa kuwapisha katika Viti huwa hawana na haraka haraka ili ' Kuzuga ' utawaona wengi wao wakizichomoa Simu zao za ' Smart ' na kuanza zao Kutiririka na Kuserereka kwa Kuchati na Kuperuzi.

Niwaombeni Watu wazima wenzangu hebu tusaidiane katika ' Kuwanyoosha ' hawa Wadogo zetu ili basi waweze ' Kutuiga ' Sisi Kaka / Dada zao ambao tumekuzwa na misingi mema ya Utu, Adabu, Utii na Nidhamu kubwa mno.

Kizazi cha ' Dot Com ' kinakera na kinaudhi sana hebu Kijitathmini na Kibadilike haraka. Sijui ni ' Sumu ' gani ambayo imetumika katika kuwatofautisha Wao na Sisi ambao tumeanza kuliona hili Jua kabla yao.

Nawasilisha.
Ww jamaa si ndiye unayetukanaga watu humu jf?
Sasa kipi kinakushangaza na wakati wanaiga kutoka kwa wakubwa zao?

Anyway, ni kawaida ya kizazi cha zamani kulaumu kizazi kipya hasa hasa linapokuja suala la maadili.

Tukibadilika na kuwa mifano bora kwa watoto ba wadogo zetu tutatengeneza kizazi chenye maadili.
 
Ashapigwa lifeban saiv,yupo na I'd nyingine
 
Kuna kitu kinakera kweli, kuna siku natoka makumbusho nenda zangu mbezi kupitia goba nimepanda gali na jamaa yangu kidogo kaingia mama kabeba mtoto sasa tukajiuliza uyu mama yupo hapa stendi gali zinapoanzia inakuwaje kapanda hali ya kuwa anaweza akasubili gali za nyuma apate siti huwezi amini watu walimkazia kinoma kwa bahati mbaya nilishuka tangi bovu sikujua kilichoendelea
 
Back
Top Bottom