Vijana wa Dar es Salaam mmekuwaje? Hii ni aibu kwa taifa

KJ07

JF-Expert Member
Dec 17, 2021
2,243
4,989
Kwa muda wa takribani wiki mbili tangia niingie Dar es salaam nimejikuta na duwaa kwa kuwashangaa vijana na wanaume wanaovaa vipensi vifupi vinavyoonyesha mapaja.
Je?
Msingi wa jambo hili ni nini maana kimaadili halijakaa sawa.
Hivi ni kweli vijana hawa hawaishi na watu wazima ambao wanaweza kuwa wasimamizi wa maadili.
Hii ni aibu kwa taifa hasa ukizingatia jiji hili linapokea watu wa aina mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali.
Vijana tuache ulimbukeni kwani si kila jambo linalozuka ulimwenguni ni la kuiga mengine yanatushushia heshima hasa katika jamii inayotuzunguka .
Sisi watu wa vijijini tumekua tukiambia dar kuna wajanja kama huu ndo ujanja wenyewe nibaki kuwa mshamba milele na wala sitadhurika na ushamba na wala sio huu ujinya.
Sisi ndo tunatakiwa tuwe mfano bora wa kuigwa kwa watoto wanaokuwa kwa sasa.
Haya si maadili wala mila zetu.
NB:najua wahusika mtakuja kunishambulia kwa fujo ila ukweli ndio huo
 
20220528_143114.jpg
Nikija dar nitawapiga ukuni nitaanza na huyu.
 
Kwa hiyo hawa mademu wanaovaa vikaptura wewe hawakustui kabisa unakuja kushangaa mwanaume kuvaa kaptura?

Kun tatizo sehemu
 
Kwa muda wa takribani wiki mbili tangia niingie Dar es salaam nimejikuta na duwaa kwa kuwashangaa vijana na wanaume wanaovaa vipensi vifupi vinavyoonyesha mapaja.
Je?
Msingi wa jambo hili ni nini maana kimaadili halijakaa sawa.
Hivi ni kweli vijana hawa hawaishi na watu wazima ambao wanaweza kuwa wasimamizi wa maadili.
Hii ni aibu kwa taifa hasa ukizingatia jiji hili linapokea watu wa aina mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali.
Vijana tuache ulimbukeni kwani si kila jambo linalozuka ulimwenguni ni la kuiga mengine yanatushushia heshima hasa katika jamii inayotuzunguka .
Sisi ndo tunatakiwa tuwe mfano bora wa kuigwa kwa watoto wanaokuwa kwa sasa.
Haya si maadili wala mila zetu.
NB:najua wahusika mtakuja kunishambulia kwa fujo ila ukweli ndio huo
Kuna tajiri mmoja alikavaa kamoja hivi mbele ya maelfu wapenda SOKA kwa Mkapa halafu akakunama.Muda ukapita wahuni wakapita naye ,akakaa huko siku kadhaa,alipopatikana akadai alivalishwa kanga.
 
Back
Top Bottom