Vijana wa CUF nao wamo kwenye "Ufisadi" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wa CUF nao wamo kwenye "Ufisadi"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Aug 17, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Monday, August 6, 2012

  JUVICUF waionya JUVICCM na BAVICHA kutotumikia matakwa ya Mafisadi wa vyama vyao.  [TABLE="class: tr-caption-container"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Naibu katibu Wa Jumuiya Ya Vijana
  CUF(JUVICUF)Bwana.Thomas Malima[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Jumuiya ya Vijana ya CUF-Chama Cha Wananchi (JUVICUF) inapenda kutoa mwito kwa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kufanya uchaguzi utakaozingatia matakwa ya vijana siyo ya watu Fulani. JUVICUF inatambua kuwa uchaguzi wa vijana ni changamoto katika taasisi za kisiasa kwani wanasiasa wakubwa hutambua kuwa Vijana ndio nguvukazi kubwa na wapiga kura wakubwa katika nchi yetu. Na ni vijana pia ndio wana matatizo makubwa hasa la ajira. Kwa hiyo hulazimika kuwapanga vijana katika mabaraza yao ili waingiapo madarakani waweze kuwatumia watakavyo.
  Hali hii husababisha Viongozi wengi wa Mabaraza ya Vijana ya vyama vya siasa hasa UVCCM na BAVICHA kuwa watumishi wa Viongozi wa vyama vyao badala ya kuwatumikia vijana walioko katika vyama vyao. Kwa sasa viongozi wa Jumuiya za vijana wamekuwa kama vipaza sauti vya Wazee badala ya kuwa vipaza sauti vya vijana.
   
 2. t

  thatha JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  JUVICUF inatambua kuwa RUSHWA ni adui wa haki ya kijana. Tunatambua kuwa endapo UVCCM watairuhusu rushwa kutembea wakati huu wa uchaguzi wao hakika watawapata viongozi wabovu wasiokidhi matakwa ya vijana.
  Vile vile JUVICUF inaamini kuwa kampeni chafu za kupakana matope, ni ishara ya uchanga wa Demokrasia.
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hakika ndoa ni nzuri hata majina yao yanafanana.JUVICUF=UVCCM
   
 4. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #4
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  JUVICUF inaishauri UVCCM kufanya uchaguzi usio na rushwa ili kupata VIONGOZI SHUPAVU wa kuwatumikia Vijana!??

  Jamani naomba kuelimishwa hii imekaajae?
   
 5. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #5
  Aug 17, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  title na contents haviendani!!!yani cuf wanataka ccm ipate viongozi bora?kweli cuf=ccm
  by the way mtatiro ana swaumu ramadhani hii au kobe?
   
Loading...