Vijana wa chama cha CUF na wa upinzani kwa ujumla, kuandamana January 12 kuunga mkono Azimio la Zanzibar

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,013
144,371
Naona kuna kila dalili ya watu kupania kutekeleza Azimio la Zanzibari ambalo lilifikiwa hivi karibuni na viongozi wa vyama vya upinzani.

Katika kutekeleza azimio hilo,vijana wa CUF kwa kuwaalika vijana kutoka vyama vingine vya upinzani, wamepanga kufanya maandamano January 12 mwaka 2019, yakiwa ni maandamano ya kuunga mkono Azimio hilo la Zanzibar.

Fungua hii link hapa chini uone video ya vijana wa CUF wanaokusudia kuandamana siku hiyo ya tarehe 12/01/2019.

Vijana CUF kuandamana Januari 12

My take:

Ni wazi wapinzani wamekusudia jambo zito maana naona Halima Mdee ame-tweet maneno: "nguvu ya umma is coming soon" huku Zitto kupitia gazeti la Mwananchi la leo akikaririwa kusema kwamba mwaka 2019 utakuwa mwaka mgumu ambao hatujawahi kuushudia kwa miaka 20 iliyopita.

Zitto: Kuanzia kesho Watanzania tegeni masikio

Naona watu wameishiwa uvumilivu na wahusika wakikosa busara,hasa bwana wakubwa,basi tunaweza kushuhudia majanga mengine kama ilivyowahi kutokea huko nyuma.
 
Naona kuna kila dalili ya watu kupania kutekeleza Azimio la Zanzibari ambalo lilifikiwa hivi karibuni na viongozi wa vyama vya upinzani.

Katika kutekeleza azimio hilo,vijana wa CUF kwa kuwaalika vijana kutoka vyama vingine vya upinzani, wamrpanga kufanya maandamano January 12 mwaka wa 2019 yakiwa ni maandamano ya kuunga mkono Azimio hilo la Zanzibar.

Fungua hii link hapa chini uone video ya vijana wa CUF wanaokusudia kuandamana siku hiyo ya tarehe 12/01/2019.

Vijana CUF kuandamana Januari 12

My take:

Ni wazi wapinzani wamekusudia jambo zito maana naona Halima Mdee ame-tweet maneno: "nguvu ya umma is coming soon" huku Zitto kupitia gazeti la Mwananchi la leo akikaririwa kusema kwamba mwaka 2019 utakuwa mwaka mgumu ambao hatujawahi kuushudia kwa miaka 20 iliyopita.

Zitto: Kuanzia kesho Watanzania tegeni masikio

Naona watu wameishiwa uvumilivu na wahusika wakikosa busara,hasa bwana wakubwa,basi tunaweza kushuhudia majanga mengine kama ilivyowahi kutokea huko nyuma.
Mungu wabariki vijana
 
Tangu Wazanzibari walivyochinjwa Kama Kuku Januari 2001 chini ya Baba yake Fatma Karume Na Mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema Fredrick Sumaye ,

Halafu Seif akaja kutafuna Kuku Na Mzee Kingunge Ng'ombale Mwiru Kwenye Muafaka pale New Africa Hotel 2003 Na hoja kubwa ikawa Mafao ya Seif Ya Uwaziri Kiongozi , Wa znz waliapa hawatoandamana Tena Hata 2015 Maalim alitamani Waandamane Baada ya Jemedari Jecha kuzima Uasi wa October 2015 lakin akajua watapuuza
 
Inaonyesha Jinsi CCM walivyo wauwaji
Yani unachinja Binadamu kama kuku bila kosa halafu unajisifu!!!
 
Katika maandamano yao wasiache kumpongeza mhe Ester Bulaya kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuwatetea watumishi wa umma waliokuwa wadhulumiwe na serekali ya CCM,pia wasiache kumpongeza jiwe kwa kujitenga na wazee wa ndiyooo na kujiunga na wapinzani kwa kufanya kile ambacho kilikuwa kinapiganiwa na wapinzani kabla muswada binafsi wa Ester haujapelekwa bungeni.
 
Zitto: Kuanzia kesho Watanzania tegeni masikio
huyu bado sana kwanza chama chake kichanga sana na hakitaweza -kuna mikoa hakijulikani kabisaa anajulikana yeye tu Zito sio ACT. Afikirie chama cha kujiunga nacho aidha chadema au CUF

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom