Paparazi Muwazi
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 310
- 80
WE MNYIKA ACHANA KUFUKUZANA NA WAMACHINGA, NJOO HAPA JF UJIBU MASWALI YA MWENYEKITI WAKO MBOWE!
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
VIJANA WA CHADEMA KUKUTANA NA WAMACHINGA WA MKOA WA DAR ES SALAAM
Kuzindua ripoti ya uchunguzi kuhusu hali na changamoto za wafanyabiashara ndogo ndogo
Kutoa zawadi kwa washindi wa kuandika michanganuo ya miradi ya wafanyabiashara ndogo ndogo
Wanachama wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) watafanya mkutano na wafanyabiashara ndogondogo wa jijini Dar es salaam katika maeneo ya Kigogo Sambusa siku ya jumapili tarehe 16 Machi, 2008 kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 9 alasiri. Mgeni rasmi katika uzinduzi huo ni Ndugu Mhonga Said Ruhanywa, Mbunge wa Viti Maalum(CHADEMA) ambaye pia ni mmoja wa wadhamini wa uchunguzi huo.
Mkutano huo ni mahususi kwa ajili ya kuzindua ripoti ya uchunguzi wa mwenendo wa wafanyabiashara ndogondogo jijini Dar Es Salaam pamoja na kutoa zawadi kwa washindi wa kuandika mchangunuo wa biashara ndogo kwa vijana. Pia mkutano utatoa fursa ya washiriki kujadili masuala ya wafanyabiashara ndogo ndogo na ujasiriamali.
Kadhalika katika mkutano huo washindi wa shindano maalumu la kuandika mchanganuo kwa wafanyabiashara ndogo ndogo wa Kinondoni lililoratibiwa na kurugenzi ya vijana wa CHADEMA watapatiwa zawadi zao.
Itakumbukwa kwamba tangu awamu ya kwanza ya serikali ya CCM kumekuwepo na tatizo kubwa la wafanya biashara ndogondogo kuingia katika mivutano ya mara kwa mara dhidi ya serikali iliyopo madarakani. Aidha kwa upande wake, serikali imekuwa ikiwaondoa wafanya biashara hao kwa madai kuwa wanaharibu mandhari ya jiji na kwamba ni budi ama warudi vijijini, au wafanye biashara katika maeneo ambayo yamepangwa na serikali.
Pamoja na hoja hizo, bado kumekuwepo na hali ya mvutano isiyokwisha baina ya wafanya biashara ndogondogo maarufu kama wamachinga , kiasi cha kupelekea uvunjifu wa amani ikiwa ni pamoja na mauaji, uharibifu wa mali za wafanyabiashara hao, na mapigano baina ya askari kwa niaba ya serikali dhidi ya wafanya biashara hao. Vijana wa CHADEMA tuliamini kuwa kujirudia kwa mivutano na mapambano haya kila wakati ni kielelezo kuwa kuna tatizo la msingi ambalo serikali ya CCM bado ama haijalichunguza au kama limechunguzwa basi halijawekwa bayana.
Katika muktadha huo CHADEMA ikiwa ni chama mbadala kinachoamini katika misingi ya amani, na ufumbuzi wa matatizo kisayansi hatuoni sababu ya watanzania kuendelea kuvutana kiasi cha kuhatarisha hali ya amani na utengamano kwa mambo ambayo yanaweza kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa njia za kistaarabu.
Hivyo tuliamua kufanya uchunguzi wa takribani miezi sita katika kipindi cha mwaka 2007 kwenye maeneo husika ili kubainisha njia mbadala kwa mustakabali mwema wa wafanya biashara ndogondogo ambao wengi ni vijana. Aidha uchunguzi huo ulifanywa na vijana wa CHADEMA kutoka taasisi za elimu ya juu, kwa kushirikiana na wafanya biashara ndogondogo. Kamati maalumu ya uchunguzi ya vijana watano iliundwa kuratibu mchakato huu.
Lengo likiwa ni kupata hoja za kuboresha mazingira ya wafanyabiashara ndogo ndogo kwa kutambua mchango wao katika ongezeko la ajira na kukua kwa uchumi wa taifa.
Uchunguzi huu ulihusisha kutembelea maeneo yaliyotengwa kuangalia hali ya mazingira ilivyo sambamba na kuzungumza na wafanyabiashara ndogondogo. Pia uchunguzi ulihusisha kukutana na baadhi ya viongozi wa serikali kupata taarifa mbalimbali za msingi na kufanya uchambuzi wa mwelekeo wa mipango iliyopo. Mchakato huu ulihusisha pia kuwatembelea wahanga wa bomoa bomoa ya wakati uliopita pamoja baadhi ya maeneo yaliyofanyiwa bomoa bomoa katika hatua ya awali kujua hali ilivyo hadi wakati uchunguzi ulipofanyika. Uchunguzi huu ulihusisha pia kutembelea baadhi ya wadau wengine mathalani mashirika yasiyo ya kiserikali kupata maoni yao kuhusu njia bora za kukukabiliana na changamoto za wamachinga. Kwa upande mwingine mchakato huu ulihusisha pia kupitia nyaraka zilizopo ikiwemo zile zilizoandaliwa na taasisi mbalimbali za utafiti zinazozungumzia changamoto zinahusiana na biashara ndogondogo nchini. Kadhalika uchunguzi ulihusisha kupata uzoefu wa baadhi ya nchi nyingine duniani zinavyoshughulikia suala la wafanyabiashara ndogondogo katika nchi zao.
Tunapenda kusisitiza kuwa: Tunathamini na kutambua haja ya miji yetu kuwa safi, lakini tunathamini na kutambua zaidi maisha ya watu kabla ya chochote.Tunaamni jumuiya ya wafanya biashara ndogondogo, taasisi za serikali na zisizo za kiserikali za kitaifa na kimataifa zitatuunga mkono matokeo ya uchunguzi huu na kuzifuatulia changamoto ambazo tutazianisha , kwa maslahi ya wafanyabiashara ndogondogo na Taifa kwa ujumla.
Punde baada ya matokeo ya uchunguzi huo kutangazwa, hapo kesho , tutayapeleka kwenye taasisi na wadau wote muhimu ili kujadili na kuanza mchakato wa kuishinikiza serikali juu ya namna bora na ya kistaarabu ya kukabiliana na changamoto za wamachinga Tanzania
Imetolewa 15/3/2008:
John John Mnyika
Mkurugenzi wa vijana
0754 694 553
mnyika@chadema.net
www.chadema.net