Vijana wa CHADEMA Arusha wagoma kushiriki maandamano kuhusu suala la Mbowe

mitigator

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
5,119
2,000
CHADEMA ARUSHA YA LAZIMISHA VIJANA KUSHIRIKI MAANDAMANO, VIJANA WAGOMA WATOA MSIMAMO MKALI KUHUSU SUALA LA MBOWE

Mkoani Arusha.

Moja ya mikakati mikubwa inayoendelea kufanywa na CHADEMA nchini ni pamoja na kuendelea kuratibu zoezi kubwa la maandamano kwenda mahakamani kwa ajili ya kuishinikiza mahakama kumuachia huru mwenyekiti wa chama hicho anayekabiliwa na kesi mbaya ya Ugaidi nchini yenye mikakati ovu dhidi ya viongozi wa nchi na raslimali za umma kwa mjibu wa mkuu wa jeshi la polisi nchini kamanda Saimon Sirro ambaye alisikika akizungumza katika mahojiano ya televisheni hivi juzi

Mara baada ya vijana hao kuzungumza na waandishi wa habari hapa jijini Arusha vijana ambao waligusia suala zima la kesi ya mwenyekiti Mbowe pamoja na mchakato mzima wa katiba mpya inayopiganiwa na viongozi wa chama hicho, vijana hao walisema kuwa ili kuweza kufanya vizuri katika jambo hilo basi waanze kujitathimini wao kwanza ndipo waende katika suala la kupigania masilahi ya nchi mzima.

"Leo hii kuna viongozi wetu wapo nje ya nchi wana andika twita tu kuwa tuandamane kwa mfano Godbless Lema tumempigania hapa Arusha kwa kipindi chake chote cha ubunge halafu mwakajana alipokosa akakimbilia Canada akatuacha huku, mgombea urais Tundu Lisu baada ya uchaguzi akakimbilia Ubelgiji akatuacha huku halafu leo wanatwiti kwenye mitandao eti tuandamane ni jambo la ajabu sana kwakweli wao wapo nje halafu sisi tuingie barabarani hilo suala hatukubaliani nalo na vijana wa Arusha kwa kuungana na wale wa Iringa, Mbeya na Dar es salaam hatupo tayari kwa maandamano hayo" walisema vijana hao kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha

Vilevile vijana hao walitoa mikakati ambayo wao kama chadema waliipanga ili kufanikisha michakato yao kufanyika kwa njia isiyo sahihi na kuhatarisha usalama wa raia na mali zao

"Kuna mikakati ambayo ilitolewa na viongozi wetu ambayo kiukweli sisi kama vijana baada ya kuitafakari tumeona haina tija zaidi ya kuleta athari hasi kwa watanzania, kiufupi sisi hatuwezi kuandamana kwa masilahi ya mtu binafsi yaani leo tuonekana tunapambana kwa ajiri ya Mbowe, tupigwe na kuumizwa kama ilivyotokea mwaka 2015 hapa damu zilimwagika kwa ajiri ya mtu ambaye hana hata shukrani na bado anaendelea kutuweka matatizoni sisi hatutakubali hilo litokee tena"

Moja kati ya mikakati iliyoazimiwa na vijana hao wa chadema ni kwamba mabaraza yatoe tamko zito juu ya mwenyekiti wetu ili kila mtu ajue kuwa tuna mpigania kisawa sawa. Ni kweli kama mtakuwa mliona ukimya fulani wa matamko tangu mwenyekiti akae ndani na hivi juzi na jana ndo akina Pambalu walijitokeza kuanza kutoa kauli zenye utata hii ni kutokana na kikao hicho cha kimkakati ambacho ndo kilimuibua kiongozi huyo wa vijana taifa chadema

Lakini vilevile mikakati hiyo iliendelea kusisitiza viongozi wote wa ngazi ya kamati Kuu watimkie ughaibuni wakaongeze sauti za huko nje ili Mama mh Rais Samia Suluhu Hassan asipate misaada ashindwe kuongoza serikal hivyo vikao waviendeshe online kutokea umoja wa mataifa bila hivyo wapo watakao ongezwa kwenye mashitaka ya mh mwenyekiti Mbowe, kwa jinsi hali inavoendelea unaweza kuona jana kuna kiongozi wa maswala ya kigeni kutokea Marekani alifanya kikao na viongozi wa vyama vya upinzani nchini na kusisitiza kuwa Marekani ipo tayari kuendelea kusaidia vyama vinavyopambania haki za msingi

Sasa unaweza kujiuliza ni haki zipi ambazo wanazipigania katika taifa hili ambalo linaongoza kwa amani kidunia na Afrika kwa ujumla? Hivyo sisi kama vijana tunaojielewa hatutaki kusikia habari hizi unapokwamisha misaada katika taifa anayeumia si Rais wa nchi Bali anayetaabika ni mwananchi wa chini kabisa anayehitaji mwanae asome, apate matibabu na kupata mahitaji yake ya msingi sasa mikakati kama hii sisi vijana hatupo tayari kuona inafanyika na kukwamisha maendeleo ya watanzania.

Mkakati mwingine ulikuwa ni lazima mwenyekiti wa vijana avunje ukimya, akaseme walipokamatwa walipigwa kutishwa sana walizuiwa kufanya siasa na walionywa sana. Hii afanye kuwasingizia ili huko nje wavimbe kisawasawa. nae atimkie ng'ambo kwo unaweza kuona jinsi ambavyo wanatumia njia za udanganyifu kuuhudaa umma wa watanzania ili tujue ni kweli kumbe ni uongo mkubwa sasa sisi kama vijana wazalendo wa nchi hii tunakubalije utoto huu?? siwezi kulisaliti taifa langu ingawaje mimi natokea CHADEMA na ni mwanachama wao lakini siwezi kukubali upuuzi huu kufanyika mbele ya macho yetu.

Halafu mkakati mwingine ni kwamba kamati kuu itayokuwa imetimkia nje ya nchi iendelee kutoa maagizo ya wananchi kutekeleza maagizo yatakayofanya nchi kuendelea kuwa ya moto mfano kuamsha maandamano makali ya kuitaka serikali kumuachia Mbowe

Najua tumetoa haya yote na isitoshe tutafukuzwa uanachama lakini potelea mbali tupo tayari kwa adhabu hiyo lakini ukweli tumeusema na umma wa watanzania wamejua kinachoendelea ndani ya chama chetu walisema vijana hao mbele ya waandishi wa habari mkoani Arusha

Sisi vijana wa Arusha hatuwezi tukawa tunapokea maagizo na waliopo nje ya nchi yetu wakitushinikiza tuandamane halafu wao hawaonekani hivyo wanapenda familia zetu ziwe zinalia kila siku ili wao wapate ajenda ya kuihujumu nchi yetu kimataifa yaani hatutakubali na hatupo tayari kwa maagizo yao hewa wakati wao wameficha familia zao mahala salama huko nje.

Halafu kuna propaganda zinaendelea eti za kubandika mabango kwenye miji wakisema umma ndo unaofanya hivyo mimi naomba niwaambieni huo ni utoto wa akina Pambalu na kagenge kake wanalipa vijana mateja ndo wanabandika hivyo vikaratasi nchi hii si ya kuchezewa na siasa uchwara chadema kuna mahali tumekosea tunapaswa kurudi na kujisahihisha tuachane na hizi siasa nyepesi zisizokuwa na tija.

View attachment 1881084 View attachment 1881085 View attachment 1881086
Rubbish.Vuvuzera za Lumumba hizo
 
zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
4,063
2,000
Wapenda amani kote nchini na wazalendo wa nchi popote pale walipo kamwe tusikubali hawa wahuni wachache wanao jifanya wanadai haki kwa kuvunja sheria watuharibie Amani ya nchi yetu.
tuchukue hatua za kuwafichua na kuwa ripoti popote pale walipo.
sio wafuasi wote wa chadema wanafurahia uhuni huu bali wapo wahuni wachache wenye chembe chembe za Ugaidi/uhalifu/ujanbazi/wizi ndio wanafanya vitendo hivi vya kihuni ili wapate sababu.
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
10,164

Wangekuwa wanachadema halisi jeshi la polisi lisingewapa muda wa kujipiga selfie, wangesambalatishwa kama wafanyiwavyo wanachadema kama ilivyotokea Dar, Mbeya, Mwanza, Kagera na Didoma, ni wakati jeshi la polisi likiratibiwa na CCM wabadili mbinu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom