Vijana wa ccm Zanzibar hawataki kupangiwa juu ya hatma ya nchi yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wa ccm Zanzibar hawataki kupangiwa juu ya hatma ya nchi yao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Aug 3, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  11 AN-NUUR
  RAMADHAN 1433, IJUMAA AGOSTI 3-9, 2012
  Makala
  VIJANA wa Umojawa Kitaifa Zanzibartumeshtushwa sanakufuatia matamshi/kaulina misimamo ya baadhiya viongozi na wafuasi waChama Cha Mapinduzi(CCM) yenye shabahaya kutumia vitisho namabavu katika kuzizimahoja za baadhi ya viongozi,wanachama na wafuasiwake wenye mawazombadala/tofauti.
  Hapa tunawakusudiaviongozi wa CCM waWilaya ya Mjini na AfisiKuu, Kisiwandui pamoja na baadhi ya viongozi wastaafuwa CCM ambao wanawatishana kuwashinikiza viongozikatika chama chao hususanWajumbe wa Baraza laWawakilishi la Wananchi waZanzibar waliochaguliwana wananchi wa Zanzibar wakiwa na wajibu wakuwatetea wananchi waZanzibar kwa mujibu wakatiba ya Zanzibar na ileya Jamhuri ya Muunganowakilindwa na kinga kwamujibu na kanuni za Barazana Sheria za nchi.Hao wenye kutoa vitishona kuweka shinikizowajue kuwa vitendo vyaohivyo ni kupora uhuru wawananchi na kuondoshauhalali wa zoezi zima lamarekebisho ya katiba.Vitendo vyao hivyo ni sawana kuwapangia wananchinini cha kusema na vitendokama hivyo ni uvunjifu wakatiba na sharia za nchi nani uporaji wa haki za msingikabisa za wananchi wote nani fedheha na aibu kubwakwa CCM.Ifahamike wazi kuwakupatikana kwa aina yamfumo wa muunganotunaoutaka utapatikana paletu ambapo wananchi wote bila ya kujali vyama vyaowatakuwa na uhuru usio namasharti ili waweze kutoamaoni yao vinginevyo zoezihili lote litapoteza maana nauhalali wake na hivyo kuwa batili.Katika hali kama hiitunamuomba MheshimiwaDk. Jakaya Mrisho Kikwetena Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohammed Sheinwaingilie kati ili kulindauhuru wa wanachama na sisiwananchi kwa ujumla wetu.Halikadhalika tunamuombaMwenyekiti wa Tume yaPamoja ya Marekebisho yaKatiba, Mheshimiwa Jaji
  Tamko la Indhari!
  Na, Vijana wa Umoja waKitaifa Zanzibar.
  PANDU Amir Kificho, Spika wa Baraza la Wawakilishi
  Joseph Warioba pamoja naMheshimiwa Pandu Ameir Kificho Spika wa Barazala Wawakilishi Zanzibar kutoa tamko juu ya kaulihizi za kushtusha za baadhiya viongozi hawa wa CCMili wananchi turidhike juuya uhuru wetu na uhalaliwetu wa kutoa maoni bilaya shinikizo la aina yoyotekutoka chama chochote.Kauli na misimamo hiyoinaonekana sio tu kwendakinyume na Azimio la Hakiza Binaadamu zinazothaminiuhuru na uwezo wa kilaraia kuwa na mawazo namaamuzi tofauti. Misimamona matamshi hayoyanapingana hata na kauliya Rais Jakaya Kikwete,Rais Ali Mohammed Sheinna Jaji Warioba ambao kwa pamoja walisema wazi kuwawananchi wako huru kuwana maoni tofauti juu yamchakato wa katiba na wawehuru katika kuyatoa mawazoyao. Aidha, Rais Kikwetealisema na tunamnukuu:“Kwa upande wa mchakatowa kupata katiba mpya,nawasihi Watanzaniatujiandae kwa maoni yakutoa. Tutofautiane bilakupigana”. Hata anayeitwaBaba wa Taifa, MwalimuJulius Kambarage Nyererealiwahi kusema katikahotuba aliyoitoa kwenyemkutano wa Uganda People’sCongress (UPC), tarehe 7Juni, 1968: “Chama kinauwezo kuiambia Serikalinini matilaba ya watu, nakwamba ni muhimu kuwekowanachama ndani ya chamawanaoweza kuhakikishakwamba Serikali na watuwanashirikiana kutekelezamatilaba ya watu”.Tunatanabahisha kuwatutofautiane katika fikra bila ya kubezana, kutishanawala kupigana. Aidha,tunatanabahisha kuwakauli kama hizi zilizoanzakutolewa zinazobebaagenda ya vitisho na kuivizademokrasia hazitavumiliwa. Ni busara kusoma alama zanyakati. Nchi hizi mbili za Zanzibar na Jamhuri ya Muunganowa Tanzania zimetokana naasili ya utawala wa chamakimoja cha siasa baada yamapinduzi ya Zanzibar na uhuru wa Tanganyika,na hatimaye kuwepo kwachama kimoja tu kwanchi zote mbili. Siasa yavyama vingi imeanza katikauchaguzi mkuu wa 1995,kiasi cha miaka kumi na sabailiyopita, tofauti na utawalawa chama kimoja wa miakazaidi ya thelathini.Kwa miaka hiyo thelathinina kitu, hakukuwa na tafautikubwa baina ya Chama naSerikali. Kwa mfano, Mkuuwa Mkoa alikuwa Katibu waMkoa wa Chama, viongoziwa Chama walikuwa nahadhi ya viongozi wa Serikalikama vile kusafiria pasi zakibalozi. Katika kila Wizara,Idara na Mashirika, kulikuwana ofisi za Chama chaMapinduzi, na Mwenyekitiwake, na bendera ya chamandio ilokuwa ikipepea. Hiiinaonesha wazi tutokapo na jinsi mfumo wa fikra za watu(mindsets) ulivyojengeka.Kutokana na hali hiisera za Chama na Serikalihazikuweza kuwa na tafautiyoyote. Sera zote za chamandio zilikuwa sera za serikali.Kwa maana hiyo sera yakuwa na Muungano waSerikali mbili iliyopo ndaniya Katiba ya Muunganondiyo ya Chama tawalacha wakati huo na ndiomaana bado kuna baadhiya viongozi (wahafidhina)wanaolalamika leo juu ya haya mabadilikotunayoyatarajia, na ndiomaana vilevile tunashuhudiawakikaripia na hata kupinga juu ya mabadiliko ya serahizo.Wakati umebadilika nanchi zetu zina vyama vingivya siasa, vyenye sera zaona wanachama wao ambaowote ni wananchi wenyehaki sawa juu ya maamuzimazito ya nchi kama katibazinavyoeleza. Zaidi yaChama tawala, hakuna hatachama kimoja chenye serayake ya muundo wa nchi,kwa sababu vinafahamukwamba sera hii haiwezikuwa ukiritimba wa chamakimoja, bali ni ridhaa yawananchi wote, hata waleambao siyo wanachama auwafuasi wa chama chochotecha siasa.Kwa hivyo huu utaratibuwa kukusanya na kuratibumaoni ya wananchi ni wakupongezwa. Hata hivyo,indhari ichukuliwe yakuhakikisha kwamba ukwelina uadilifu unatawala katikazoezi hili, na kwamba kilamwananchi apewe fursa yakutoa maoni huru bila yashinikizo la kuimba nyimboya sera za Chama chake. Hiiitakuwa kinyume kabisa nawanavyofanya baadhi yaviongozi na wanachamawa Chama cha Mapinduzi(CCM) kutaka kuwatishana kuwanyanyapaa baadhiya wanachama wake wenyefikra tofauti zinazokwendakwa mujibu wa hali yasiasa zilivyo hivi leo. Huuni wakati wa wananchikupingana bila ya kupiganana hii ndio demokrasiaitakayotuletea amani nausalama. Hapa elimu yauraia ndipo inapohitajika.Tunasisitiza kuwamatokeo ya zoezi hiliyaheshimiwe na wote.Tunajua kwambaMwenyekiti wa Tume yaMabadiliko ya Katiba nikiongozi mwandamizi waChama chake. Tunamuombakwamba asiyumbishwe nasera za Chama chake katikazoezi hili. Tume ni sualalinalojitegemea na maslahiya nchi na watu wake nimakubwa kuliko sera zavyama. Huu ni wakati wakusonga mbele si wakati tenawa kutazama nyuma. Wakatina mawimbi hayamsubirimtu.Tufanye kazi katikamaadili ya shabahayanayoheshimu mawazo,maoni na maamuzi yawananchi. Tuna wajibu wakusimama juu ya ukwelikama tunavyouona bila yakujali misingi na mirengoya vyama. Sote kwa ujumlawetu kuanzia vyama, Tumeya Mabadiliko ya Katibana Serikali zote mbili niwatumishi wa watu. Na watumishi hawanahaki wala mamlaka walanguvu zinazowazidimabwana zao ambao niwananchi kama Katiba zotembili zinavyolithamini hilo.Tunawajibika katika hilikutoa huduma ya kizalendona kwa sababu hiyoitakuwa huduma ya kwelina isiyosimamia misingi yavyama.Sisi Vijana wa Umoja waKitaifa ni waumini wenyekuheshimu uhuru wa mawazoya kila mwananchi; lakini pia tunabeba kauli mbiu(motto) isemayo: “Maslahiya wananchi ni makubwazaidi kuliko yale ya vyamavya siasa.” Historia itakujakutuhukumu.
  Nakala:-

  Mheshimiwa Jaji JosephWarioba, Mwenyekitiwa Tume ya Pamoja yaMarekebisho ya Katiba.Mheshimiwa PanduAmeir Kificho, Spika waBaraza la WawakilishiZanzibar
   
Loading...