Vijana wa CCM wawacharanga mapanga wafuasi wa Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wa CCM wawacharanga mapanga wafuasi wa Chadema

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mtaka Haki, Oct 14, 2010.

 1. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  NI MUHIMU RAISI JAKAYA MRISHO KIKWETE AKACHUKUA HATUA YA HARAKA JUU YA HALI HII INAYOJITOKEZA YA WAFUASI WA CCM. NAOMBA WATANZANIA TUMHIMIZE RAIS WETU KATIKA HILI.
  SOMA HABARI HII HAPA CHINI. NINA HAKIKA KAMA MH KIKWETE ATAKEMEA WAFUASII WAKE KATIKA KILA KAMPENI ZAKE NA WAGOMBEA WOTE NAO WAKAKEMEA WAFUASI WAO BASI HILI LITAKOMA.
  NA WAANDISHI WETU
  13th October 2010
  B-pepe
  Chapa
  Maoni

  Rehema Malima (15) ambaye ni mmoja ya watu waliokatwa mapanga wakati wa vurugu lilizotokea kati ya wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) nawa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Musoma, akionyesha vidole vilivyokatwa kwa mapanga.
  Watu wanaosadikiwa kuwa wafuasi na viongozi wa CCM jimbo la Musoma mjini, wamewakatakata mapanga na kuwajeruhi vibaya watu wanaodhaniwa ni wafuasi wa Chadema.
  Tukio hilo lilitokea juzi usiku na jana subuhi katika kata ya Kigera mjini hapa.
  Wakizungumza na Nipashe juzi usiku katika Hospitali ya Serikali ya Mkoa wa Mara, mmoja wa majeruhi hao, Seleman Mwita, alidai alishambvuliwa na kundi la vijana wa CCM wakiwa na viongozi wa tawi la Kigera Bondeni.
  Alisema wakati akitokea katika mkutano za Chadema kata ya Buhare alikutana na kundi la vijana hao walikuwa wamevalia sara za CCM walimtaka kueleza sababu za kukishabikia Chadema, lakini wakati akijieleza walianza kumkata na mmoja wapo kuchomoa panga na kumkata kichwani.
  Hata hivyo, alisema wakati akifanyiwa kitendo hicho walikuwepo viongozi wengine wa CCM ambao walionekana kushabikia hivyo wananchi wa eneo hilo walianza kupiga kelele kwa lengo la kumuokoa.
  “Wakati nikiokolewa na wananchi kidogo likatokea gari la mgombea wa Chadema, Vicent Nyerere, ambalo lilinichukua na kunipeleka polisi kupata fomu namba tatu ya polisi kisha kunipeleka hospitalini,” aliongeza.
  Alisema wakati madaktari wakijaribu kuokoa maisha yake, ghafla baadhi ya wananchi walimfikisha majeruhi mwingine Mapambano Malima akiwa amekatwa vibaya na panga sehemu ya kichwani na usoni.
  “Nilikuwa natokea gengeni nikiwa na vijana wenzangu sasa wakati nikiondoka kwenda nyumbani nikakutana na kundi hilo ambao wengi nawafahamu wakanihoji ni kwanini navaa beji ya Nyerere (Vicent) kabla ya kujibu walianza kunishambulia,” alisema.
  Kadhalika, jana asubuhi, baadhi ya vijana hao walivamia nyumbani kwa mama Tatu William katika eneo la Kigera Bondeni na kumtaka ashushe bendera ya Chadema iliyokuwa juu ya nyumba yake, lakini wakati wakizidi kubishana walichomoa panga na kushambulia mototo wake wa kike, Rahab Malima(15) kwa kumkata vidole vya mkono wa kulia.
  Alisema pamoja na mtoto huyo kushambuliwa, pia walimchoma na chuma chenye ncha kali.
  Kamanda wa polisi mkoani hapa, Robert Boazi, alithibitisha kutokea kwa matukio hayo.
  Boaz alisema matukio hayo yalitokea baada ya ugomvi uliotokea wakati viongozi wa CCM wa kata ya Kigera walipokuwa wakitembea nyumba kwa nyumba wakiomba kura, kitendo ambacho kinadaiwa kuwachukiza wananchi wa eneo hilo na kuzua vurugu hizo.
  Waliojeruhiwa ni Kapuru Charlesi(44), Sele Mwita (27) na Mapambano Malima (30), wote wakazi wa Kigera Migombani.
  Boaz alisema polisi inawashikilia watu watano kwa mahojiano.
  Mgombea ubunge wa Chadema, Vicent Nyerere na Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Musoma mjini, Charles Kayele, walisema kuwa kitendo kilichofanywa na vijana wa CCM kinatokana na vyombo vya dola kufumbia macho malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa dhidi ya CCM kwa kuendesha mafunzo ya kijeshi kwa vijana wake.
  Katibu wa CCM wilaya ya Musoma, Haula Kachwamba, alisema kuwa suala hilo ni la polisi.
  CHANZO: NIPASHE
  0 Maoni | Kuwa wa kwanza kutoa maoni
   
 2. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtaka haki hii habari tumejadili toka juzi/jana kuna thread nyingine mkuu, ahsante lakini kwa kutoa maoni yako.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,316
  Trophy Points: 280
  JK na Chama cha mafisadi wanataka kuendelea kutuongoza kwa mtutu wa bunduki lakini safari hii hatutamwogopa mwanadamu
   
Loading...