Vijana wa CCM: Tusikubali mafundisho ya kusifia tuu mtu na chama chetu, bali tupokee yale yenye kutia "UBUNIFU" wa kuijenga nchi kisayansi zaidi.

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,791
3,360
Ninamsifu na ninamshukuru baba yangu mzazi kwa :-

1. Kuandaa mazingira ya kumwoa mama hatimaye nikawa duniani.

2. Kujenga nyumba ya tope na bati, na kutulelea humo, wakati huo majirani wote walikuwa na nyumba za makuti.

3. Kuishi kwa kutegemea kilimo na ufugaji ndani ya shamba la baba ; mahindi tulipata gunia 6 kwa ekari kwa kutumia mbegu za kienyeji. Yalitutosha mwaka mzima na ziada tuliuza. Hatukuwahi kuombaomba chakula.

4. baba kuwa na elimu ya middle school, na mimi ni akanisomesha hadi form six na zaidi na kujiajiri. Sasa ninajiandaa kuanza maisha ikiwa ni pamoja na kuoa,kujenga kulea familia nk.

Je, wewe kama great thinker,unanishaurije kuhusu namna ya kufanikisha maisha kama baba alivyofanikisha?

- Niendelee kumsifia kwa kuwa wa kwanza kuwa na nyumba ya bati, nami nijenge kama ile ile?

- Niwe na shamba kama baba, nilime,nipate gunia 6 kwa ekari ili familia isiathirike kwa njaa?

Ndugu wanaJF na wapenzi wa ujenzi wa nchi yetu, mimi ni mdau wa mabadiliko.
Nimesikiliza mafundisho ya Comrade Polepole kwa vijana wetu wa UDSM ya kukuza uelewa wa Itikadi ya Chama Cha Mapinduzi.

Nikaona nami kama Mzazi (Mwana CCM) mpenda mabadiliko hasa ya kiuchumi nitoe kasoro nilizoziona kama ifuatavyo:-

1. Mh. Comrade Polepole alipwaya sana kama mwezeshaji wa mhadhara ule. Kimsingi huyu Comrade hajui vizuri Itikadi na Siasa ya CCM,tulikotoka,tuliko na tunakoenda. Aliishia kuweka mipasho,mawazo yake, kubeza upinzani, kusifia, kutukuza miradi ambayo ni michanga au inajengwa na haijafikia kutoa matokeo chanya.

Itikadi ya Chama ni imani inayopelekea kufikia malengo fulani hasa ya Kisiasa,Kijamii au Kiuchumi. Itikadi ya CCM bado ndiyo ileile iliyokuwa ya TANU na kwa kiasi ASP kuwa Chama kitajenga nchi yenye kufuata Uchumi kwa Siasa Ujamaa na Kujitegemea. Vijana wetu wanatakiwa kujua je, bado tunafuata kindakindaki itikadi hiyo ya baba au babu zao?

Wanatakiwa kujua kama kuna mabadiliko, ni lini yalifanyika, ni yepi na faida zake! Lengo ni ili tuwape nafasi waijadili kwa kina kama inafaa au la kulingana na mazingira ya sasa.

Hiki kipengele hakikuelezwa vilivyo! Na ukiangalia yanayoendelea hapa nchini kwenye sera za Uchumi,siyo yale yaliyoainishwa kama matokeo ya Itikadi iliyo kwenye Katiba ya CCM.

Hakuna nchi ya Kijamaa Duniani inayobinafsisha njia Kuu za Uchumi. Njia kuu za uchumi zinahodhiwa na Serikali au Umma. Sasa tunaona sekta binafsi ikipewa kipaumbele kwa kutumia neno "uwekezaji" .

Hii Mh, Polepole hajaieleza imekaaje na inaoanishwaje na Itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea. Hapo,tulitarajia kupata mbegu mpya za vijana wabunifu na wanamapinduzi ya kweli kama kina Castro Ruz, Hayati Nyerere nk.

Watajenga ghorofa badala nyumba za tope na bati kama ile ya baba, watalima na kuvuna gunia 50 za mahindi kwa ekari na siyo 6 kama za baba.

Tunapowapa mafundisho ya
Kuwafungia kwa kuwataka wasifu tuu, wawaone wanaopinga ni wasaliti,wasijadili au kuhoji,tunajenga kizazi cha ajabu cha kutawaliwa tuu bila kufikiri!!?

Ninaamini,vijana wetu na wasomi wa CCM wana yao mazuri pengine kuliko tunayofikiri sisi kina Comrade Polepole ni mazuri zaidi.

Kuna vijana wengi ndani ya chama chetu wanaogopa kutoa mawazo yao kulingana na mfumo unaojengenga sasa wa kubana fursa au jukwaa la kutoa maoni.

Wamebakia watazamaji. Hii ni hatari ukizingatia ushindani unaoukua siku hadi siku wa kisera ,kiitikadi, kitechnologia,kiuchumi nk Afrika na Duniani kote.

Tuwajenge vijana wetu katika misingi ya utaifa zaidi kwa kuwapa fursa za kubuni njia bora zaidi za kufikia maendeleo makubwa zaidi ya nchi yetu ndani ya Chama au vyama vyao .

Tuwaweke pamoja proposers na opposers wadebate hatma ya nchi yetu,waende mbele zaidi ya kusifia tuu yale ya baba kujenga bati kwa nyumba ya tope huku tukifungia yao ya kujenga ghorofa nk.
 
Bora hamkuishi maisha ya kusadikika ama ya kupiga ramli kwasasa tunaishi maisha kwakutumia Sera za nyuma ya mikamela 'policy of uncertainties' biashara zimekufa na zinaendelea kufa huwezi kupanga bila Sera zinazo dumu 'you can't plan with policy of uncertainties'

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha mleta Mada nimekuelewa ,binafsi nilimsikiliza siku hy pale shekilango ubungo , jamaa alikua ana wakaririsha hao mnaita vijana wasomi wa ccm

MTC | 101|
 
Sera kuu ya CCM kwasasa n Uzushi na unafiki.

Hakuna mikakati ya maana kulijenga Taifa nikuzusha na kupotosha.

Elimu ya hovyohovyo......haina ubora, ccm insifia kinafiki na uzushi

Afya ya hovyohovyo ....ccm nikusifia tuuu

Uchumi.....ndio kabisa, vyelehani 4 kinaitwa kiwanda, mfuga kuku wa nyama 50 kinaitwa kiwanda , msaga unga lishe kilo 100 kwa siku eti kiwanda

Katiba inaruhusu siasa, ccm wanatumia polisi wao wanafanya siasa wengine hapana

Ccm chama cha unafiki na ukandamizaji hakina lolote zaidi ya kuendesha Taifa kiujanjaujanja

No strategies
No projections
No planning
Something blindly floating

Polepole anajuwa vizuri

Bao la mkono ....Nape

Uchaguzi ukiwa huru na haki .....ccm ijiandae kukabidhi Ikulu......polepole
 
Mkuu, tusichoke kutoa maoni pale panapostahili.
 
Polepole &CO, Magufuli anawaita WAPUMBAVU wake, hakuna watachosema wala kufanya zaidi ya kuwa WAPUMBAVU wa Magufuli.
Kazi ni moja tu: kuabudu na kusifia, fullstop.

Wewe nani mpaka ubishe. Utatimuliwa.
 
Back
Top Bottom