Vijana wa CCM tupinge mwenendo mbaya wa dola kwa nguvu zetu zote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wa CCM tupinge mwenendo mbaya wa dola kwa nguvu zetu zote

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nyundo, Nov 9, 2011.

 1. n

  nyundo Senior Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 13, 2007
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ningependa kutoa msimamo wangu juu ya matukio yanayotoke huko Arusha kama kijana Mtanzania, mpenda nchi yangu na watu wake, pia kama kijana kiongozi ndani ya UVCCM.

  Siridhishwi na hali inayoendelea huko Mkoani Arusha na jinsi suala hilo linavyoshughulikiwa.

  Siridhishwi na namna ya dola inavyowabagua vijana wa arusha kutokana na kutofautiana kiitikadi na chama tawala, na hivyo kuwa ni tiketi ya kuwafanyia unyanyasaji, udhalilishaji na uonevu wa kila hali. Vijana ndio wanaoshiriki kudai kile wanachokidai, hawsikilizwi, badala yake wanakumbana na kikwazo cha vitisho, mabomu, risasi za moto, kufunguliwa mashitaka pamoja na kudhalilishwa mbele ya raia.

  Vijana wa CCM tunabeza haya, tunafurahia, tumesimama pembeni tukiwa tunaangali kinachoendelea. Ila tukumbuke, nje ya itikadi zetu za vyama, vijana wote ni wamoja, vijana wote ndio tutakalolijenga taifa hili sasa na hapo baadaye.

  Katika kujenga taifa haihitaji nguvu ya itikadi moja, bali ni nguvu ya pamoja. Kama katika hili vijana wa ccm tutakuwa tunajitenga nalo basi tujue tunajitengenezea au tunatengenezewa mwanzo mbaya wa kutokuja shirikiana hapo baadaye kuijenga nchi yetu kwa umoja uliokuwepo hapo zamani.

  Ningependa kutoa nasaha kwa serikali yangu ya CCM, watambue kwamba Arusha ni zaidi ya siasa, Arusha ni sehemu muhimu sana kwa uchumi wetu, sekta ya utalii ni ya pili katika kuchangia pato la taifa. Hakuna utalii bila kujumuisha mji wa arusha. Arusha ndio serengeti. Arusha ndio manyara, arusha ndio mlima kilimanjaro na arusha ndio Tanzanite. Pia Arusha ni kituo kikubwa kwa diplomasia ya kimataifa na mahusiano ya masuala mbalimbali ya kijumuiya na mashirikiano ya kikanda.

  Si sahihi kuacha tunu yote hiyo ipotee kwa maslahi madogo ya kisiasa na matakwa ya kundi ama hisia za kiitikadi. Chadema imefanya makosa, CCM imefanya makosa.

  Lakini CCM imefanya makosa makubwa zaidi kwakuwa wao baada ya kushika dola mgogoro uliozaliwa kwenye siasa wakauhamishia kwenye dola na chadema kubaki na wanasiasa, hivyo dola kupitia jeshi la polisi wanapambana na ugomvi ambao haukutakiwa ufike kwao. Na sasa tunaona madhara yake.

  Wanasiasa waliohusika na yanayotokea Arusha warudi nyuma, waache ubabe kwa kuwa wao wana dola, wana nguvu ya majeshi na kauli za kuamrisha chochote.

  Ikumbukwe wakati tunapigania uhuru hatukumwaga damu. Ila sasa tunagombania madaraka tunamwaga damu, tunauwana wenyewe kwa wenyewe, hii sio maana ya uhuru tulioutaka.

  Vijana wa CCM tukiacha unyanyasaji huu kwa vijana na viongozi wa upinzani basi dhambi hii haitaishia hapo, itajirudia. Itafika wakati vijana ambao wamo ndani ya CCM lakini wanapingana kimtazamo na kiongozi fulani ambaye ana ushawishi kuwaambia polisi washughulikie kundi fulani kwenye ccm itakuwa hivyo.

  Daima mwisho wa yote, manyanyaso, mateso na dhulma haki ndiyo mshindi na daima ukweli ndio utamuweka mtu huru. Kama viongozi wa serikali yangu ya CCM wakaona hakuna busara inayohitajika kusikiliza malalamiko wanayodai wapinzani basi dhana ya kuchagua viongozi kwa kuzingatia busara zao utakuwa haukufuatwa, kwani busara tungependa kuiona kwenye masuala kama haya.

  Vijana tunatakiwa tukatae matumizi ya nguvu dhidi ya wananchi bila kujali itikadi zetu, kwani hili ni jukumu letu kama katiba ya ccm inavyosema. Lakini pia tunajukumu la kusimamia na kutilia mkazo juu ya kutendeka kwa haki za msingi za kikatiba ili tanzania iwe sehemu huru kwa maisha ya kila mmoja!

  "Tujisahihishe"

  M. Nyundo.
  Mjumbe, Baraza kuu UVCCM (M)
   
 2. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,971
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kijana wa ccm aongee hivi? Inanipa mashaka mengi kukuamini mkuu. Ccm HAKUNA anayeweza kuongelea umoja wa kitaifa akaacha maslahi ya chama chao pembeni.
   
 3. n

  nyundo Senior Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 13, 2007
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuwa ccm sio maana yake ukubaliane na kila ambalo linaonekana si sahihi! Ccm hairuhu ukandamizaji wa haki za raia! Mkuu mimi ni ccm na ni kiongozi! Lakini kwa hili nimetoa msimamo wangu binafsi na si kama nimeisemea jumuiya!
  M.Nyundo
   
 4. m

  makaptula Senior Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 157
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Segere hawaliwezi hao watuachie wenyewe tulicheze.
   
 5. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​
  mkuu kunaukweli? ccm kufilisika kiasi hicho inakuweje uwe mtanashati mitaani ndani kwako kuchafu sawa na dampo
   
 6. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​​vijana ccm msewe kama maboya kesho ilisha pita naweni uso kumekucha
   
 7. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 7,440
  Likes Received: 9,090
  Trophy Points: 280
  Mkuu, umenikuna Sana, binafsi sina kadi ya chama chochote cha kisiasa ila kwa jinsi ulivyofunguka ni dhahiri kuwa CCM HAPAKUFAI... Mawazo yako yanafanana sana na yale ya barua ya Lema.. Ukitaka kuamini kama huko siyo kwako ngoja wanamagamba watapokuita ktk vikao vya ndani, unaweza kuonekana unataka utengeneze kundi lako nakati in reality you fightng for your fellow Tanzania's.. So TOKA HUKO ULIKO, HAMIA KWA WANABADILIKO WAKWELI ambao hawajawahi kuwalipa watu wahudhurie ktk mikutano yao.. Ambao wamekua tayari kudhalilishwa ktk kuhakikisha angalau na sisi wa chini tunakumbukwa! TOKA HUKO ULIKO, TUNAHITAJI SANA MSAADA WAKO
   
 8. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ataambiwa ni Muhaini.
   
 9. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #9
  Nov 9, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  nyundo pola kiongozi kazi ngumu sana unayofanya hawa watu pesa kwanza.ila we ni vijana zaidi nn?.mi nakushauri kama ni kweli upo kwa ajili ya wtz vema sana ila kama umetumwa unajidhalilisia hawa watu hawana shukrani watakutumia kama kondo.. Wakishapata wanakutupa
   
 10. n

  nyundo Senior Member

  #10
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 13, 2007
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks Mkuu, ila ningependa kukuhakikishia ya kwamba ni kweli nimetumwa, nimetumwa na dhamira ya kweli ya kusimamia ukweli na haki, nimetumwa na dhana ya ukweli kwamba watanzania wamechoka kusikia kila kukicha wanasikia serikali yao inashughulika na mambo ambayo hayana + impact na dhamira yao ya kuichagua na matarajio yao na hivyo kuanza kukata tamaa na maisha yao! Mkuu tafuta historia yangu, mimi sijawahi na haitotokea kununuliwa hata siku moja!
   
 11. A

  AzimiolaArusha Senior Member

  #11
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45

  mbona ccm tuko wengi tu jamani tusiofurahishwa na mienendo ya hii serikali yetu na wajibu wetu ni kuwakumbusha na kuwaambia pia na pengine hata kuwakemea!! Kaka Nyundo hongera sana, tuko pamoja na tutalifanyia kazi suala lako!!!
   
 12. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Si hivyo tu, vjana wa CCM wakumbuke kuwa kuna uwezekano mkubwa wa wao kuja kuwa kwenye chama cha upinzani siku za usoni. Je, wangependa watendewe kama hivi?
   
 13. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #13
  Nov 9, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  mimi sina shaka nae kabisa, ninaamini wako wengi katika ccm ambao hawakubaliani na upumbafu na maamuzi ya kishenzi yafanywayo na viongozi wa chama na nchi, inabidi wabaki huko kwa sababu za kiintelejensia, wakitoka wote tutakosa mengi,

  MAPAMBANO YANAENDELEA
   
 14. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #14
  Nov 9, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Bado kuna watu especially vijana wenye akili zao ndani ya CCM ambao wamekataa ama kununuliwa au kufuata mkumbo, Wafundisheni hao wazee wenu waache upu##i. Mambo ya ajabu kabisa, sisi tunataka amani, na usawa kwenye rasilimali zetu na si vinginevyo. Imetulia
   
 15. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #15
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hongera kwa dhamira safi juu wtza, wote kwa ujumla ktk kulinda na kutekeleza swala zima la utawala wa sheria kwa maendeleo ya nchi! Nakupa hongera lkn najiuliza mengi juu ya uanachama wako kwa ccm! Je ni hili tu la Arusha ndolinakuamusha na kuona udhalimu wa CCM kwa watz?
   
 16. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #16
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Nimeipenda hii ukweli ndio huo lazima haki itashinda mwisho wasiku!!!!!!!! Mtenda akumbuke na yeye kutendewa vile vile!!!!!!!!! CCM wanachekea manyanyaso ngoja zamu yao!!!!!!!!!
   
 17. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #17
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Napongeza kijana Nyundo,inaonyesha wewe ni mzalendo na kwasababu ni kijana unayetambua kwamba siasa za kunyanyasa wapinzani ni za kizee na kizamani. Nafarijika ninaposoma maoni kama haya kutoka kwako na vijana wengine kama Benno Malisa na James Millya. Inaonyesha ndani ya CCM kuna vijana wenye busara kuliko viongozi na wazee wao.
   
 18. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #18
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Kama Kweli uyasemayo uko tayari kuyasimamia, basi hongera sana. Nafurahi kuona kuwa hata CCM wenyewe wanatambua uonevu huo unaofanywa.
  Karibu katika mapambano na Mungu Akubariki sana
   
 19. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #19
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,398
  Likes Received: 1,523
  Trophy Points: 280
  ............saaafi sana, ikifikia wakati tukaachana na siasa za kutumia matumbo kufikiri, itapendeza sana, thread hii ya Nyundo sio ya bahati mbaya, anajua siku moja nao (CCM) watakuwa chama cha upinzani, BRAVO Nyundo.
   
 20. Chilipamwao

  Chilipamwao JF-Expert Member

  #20
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35

  Hakika umenena, inanipa shida kuamini kuwa nawe upo CCM. Natamani message yako hii iwafikie viongozi wenzako wote.
   
Loading...