Vijana wa CCM ni jeshi la mbele,tusimame imara kuilinda tanzania, tukumbuke mahitaji yetu ni mawili tu, kuishi kwa kujitegemea na kupata mali halali

AUGUSTINO CHIWINGA

JF-Expert Member
Apr 23, 2017
220
689
Asalaam Aleykhum Macomrade wenzangu!

Nawasalimu katika jina lenye heri la Chama Cha Mapinduzi.
Ni vizuri tukatumia wasaa huu mchache katika kukumbushana masuala mtambuka ya msingi kwetu sisi Vijana tunaotokana na Chama Cha Mapinduzi. Kwanza napenda itambulike sisi ndio tunaoongoza kwa kuwa na moyo wa uzalendo katika kuilinda na kuitetea nchi yetu adhimu ya Tanzania.Amani iliyopo ni matunda ya uzalendo wetu huo tangu enzi za TANU Youth League mpaka sasa hivi UVCCM.

Kwa bahati mbaya ,Nchi yetu imeingiliwa na vibaraka wanaotumika kuipaka matope , nia zao ni ovu za kutaka nchi itetereke na Serikali ishindwe kufanya kazi. Vibaraka hao wanaonyonya mirija ya fedha chafu ni mahasidi, wazandiki, watu wasio maana wasiowapenda watu wa Tanzania ijpokua nao wanajiita eti ni Raia wa Tanzania.
Ni lazima tuwalaani na kuwakemea kwa nguvu na uwezo wetu wote.Katu tusikubali kuwakalia kimya, ni lazima tupambane nao kwa nguvu ya hoja kufa au kupona nao tena tukiwa mstari wa mbele bila uwoga wowote.

Tuwashtaki vibaraka kwa wananchi na mipango yao ya kishetani,vibaraka hawa ni watu hatari ni vimelea hatarishi kwa Taifa wanatumika kutaka kuitweza tunu yetu ya Uhuru na Umoja. Katu tusikubali watuchafulie nchi kama wao wameichoka Tanzania wana mambo mawili ya kufanya eidha wakae kimya au wakatafute nchi ya kwenda.

Hakuna Raia yoyote wa Tanzania ambaye atakaa na kuanza kupinga au kubeza mradi wa Stiegelers Gorge , SGR, ununuzi wa ndege au hatua ya ukamataji wa mchanga wa dhahabu kwa jina linguine mchanga wa Makinikia. Wanaopinga miradi hii ya maendeleo inayotekelezwa kwa kasi kubwa hapa Tanzania ipo haja ya kutilia mashaka Uraia wao.

Ni sisi vijana wa CCM ndio tunaotambua umuhimu maendeleo haya makubwa yanayofanyika hapa nchini na ni lazima tulize vinubi kwa nguvu mpaka masikio ya vibaraka na mabebeberu wao yapasuke na dunia ijue kwamba hii ni Tanzania mpya iliyodhamiria kupiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa kufanya siasa safi zenye za maendeleo zenye lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati.

Hatuna haja ya kuogopa au kuhofia chochote kwa sababu Serikali sikivu ya Wananchi ya CCM ina dhamira njema na inafanya kazi kwa kumtanguliza MUNGU mbele lakini pia kwa kuyatanguliza mbele maslahi mapana ya wale inaowatumikia yaani Wananchi.

Tuendelee kuulinda na kuutetea Ujamaa , tuishi kwa kujitegemea tusiwe kupe wa kuwanyonya wenzetu, lakini pia tuhakikishe mali tunazopata ni halali na zinatokana na fedha halali.
Ni aibu kwa kijana wa CCM kufanya mambo ya hovyo hovyo kama kupokea au kutoa rushwa, kuiba , kudhulumu watu ,kufanya ujangili au uhalifu wowote unaofanana na matendo hayo.Kijana wa CCM ukiaminiwa aminika.

Kijana wa CCM ni taswira kwa jamii inayomzunguka, kijana wa CCM ni kioo cha viongozi wa CCM lazima ahakikishe matendo yake hayatawafedhehesha viongozi wake wa Chama.

Mwisho kabisa kijana wa CCM anatakiwa kuwa na NIDHAMU. Nidhamu ndio msingi wa kujenga chama Imara, pia inafanya tupate Taifa bora lenye maadili na watu waadilifu. Bila ya nidhamu na utii chama chetu kitayumba tutawapa nafasi vibaraka kutushambulia.

Kidumu chama Cha Mapinduzi!
Augustino Chiwinga
Mtama-Lindi
0756 810 804
 
Sema vijana muitetee ccm na si Tanzania maana uvccm ndo mnaharibu tz I hope mna laana
 
Mimi kama mkuu wa vijana wa buku saba nimeona juhudi zako mzee sasa zawadi yetu kwako ni nguo hii maana tumeona tokea umeanza kutusifia haujabadilisha nguo hasa hilo shati
20190307_111148.jpeg

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Asalaam Aleykhum Macomrade wenzangu!

Nawasalimu katika jina lenye heri la Chama Cha Mapinduzi.
Ni vizuri tukatumia wasaa huu mchache katika kukumbushana masuala mtambuka ya msingi kwetu sisi Vijana tunaotokana na Chama Cha Mapinduzi. Kwanza napenda itambulike sisi ndio tunaoongoza kwa kuwa na moyo wa uzalendo katika kuilinda na kuitetea nchi yetu adhimu ya Tanzania.Amani iliyopo ni matunda ya uzalendo wetu huo tangu enzi za TANU Youth League mpaka sasa hivi UVCCM.

Kwa bahati mbaya ,Nchi yetu imeingiliwa na vibaraka wanaotumika kuipaka matope , nia zao ni ovu za kutaka nchi itetereke na Serikali ishindwe kufanya kazi. Vibaraka hao wanaonyonya mirija ya fedha chafu ni mahasidi, wazandiki, watu wasio maana wasiowapenda watu wa Tanzania ijpokua nao wanajiita eti ni Raia wa Tanzania.
Ni lazima tuwalaani na kuwakemea kwa nguvu na uwezo wetu wote.Katu tusikubali kuwakalia kimya, ni lazima tupambane nao kwa nguvu ya hoja kufa au kupona nao tena tukiwa mstari wa mbele bila uwoga wowote.

Tuwashtaki vibaraka kwa wananchi na mipango yao ya kishetani,vibaraka hawa ni watu hatari ni vimelea hatarishi kwa Taifa wanatumika kutaka kuitweza tunu yetu ya Uhuru na Umoja. Katu tusikubali watuchafulie nchi kama wao wameichoka Tanzania wana mambo mawili ya kufanya eidha wakae kimya au wakatafute nchi ya kwenda.

Hakuna Raia yoyote wa Tanzania ambaye atakaa na kuanza kupinga au kubeza mradi wa Stiegelers Gorge , SGR, ununuzi wa ndege au hatua ya ukamataji wa mchanga wa dhahabu kwa jina linguine mchanga wa Makinikia. Wanaopinga miradi hii ya maendeleo inayotekelezwa kwa kasi kubwa hapa Tanzania ipo haja ya kutilia mashaka Uraia wao.

Ni sisi vijana wa CCM ndio tunaotambua umuhimu maendeleo haya makubwa yanayofanyika hapa nchini na ni lazima tulize vinubi kwa nguvu mpaka masikio ya vibaraka na mabebeberu wao yapasuke na dunia ijue kwamba hii ni Tanzania mpya iliyodhamiria kupiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa kufanya siasa safi zenye za maendeleo zenye lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati.

Hatuna haja ya kuogopa au kuhofia chochote kwa sababu Serikali sikivu ya Wananchi ya CCM ina dhamira njema na inafanya kazi kwa kumtanguliza MUNGU mbele lakini pia kwa kuyatanguliza mbele maslahi mapana ya wale inaowatumikia yaani Wananchi.

Tuendelee kuulinda na kuutetea Ujamaa , tuishi kwa kujitegemea tusiwe kupe wa kuwanyonya wenzetu, lakini pia tuhakikishe mali tunazopata ni halali na zinatokana na fedha halali.
Ni aibu kwa kijana wa CCM kufanya mambo ya hovyo hovyo kama kupokea au kutoa rushwa, kuiba , kudhulumu watu ,kufanya ujangili au uhalifu wowote unaofanana na matendo hayo.Kijana wa CCM ukiaminiwa aminika.

Kijana wa CCM ni taswira kwa jamii inayomzunguka, kijana wa CCM ni kioo cha viongozi wa CCM lazima ahakikishe matendo yake hayatawafedhehesha viongozi wake wa Chama.

Mwisho kabisa kijana wa CCM anatakiwa kuwa na NIDHAMU. Nidhamu ndio msingi wa kujenga chama Imara, pia inafanya tupate Taifa bora lenye maadili na watu waadilifu. Bila ya nidhamu na utii chama chetu kitayumba tutawapa nafasi vibaraka kutushambulia.

Kidumu chama Cha Mapinduzi!
Augustino Chiwinga
Mtama-Lindi
0756 810 804
jipe jibu sasa ukiwa na akili timamu coz najua kipindi unaandika uzi huu njaa ndio ilikuwa inakusumbua
 
Back
Top Bottom