Vijana wa CCM mnazeekea kwenye corridor za Lumumba. Vijana wa upinzani wanazidi kulamba vyeo. Mpo?

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,567
50,393
Inauma, inauma Sana! Umeanza kuipenda CCM tangu utoto, ukashiriki chipukizi kisha ukaingia UVCCM.

Umesaka mpk vyeti vya elimu ya juu ili uwe na sifa zote za kupewa nafasi ndani ya chama ulichokipambania tangu utoto wako lkn unaishia kusugua benchi kwenye korido za Lumumba.

Kuna siku jpm aliwahi kumpa sifa msomi (wa phd) fulani ndani ya ccm kwamba amekuwa akilipwa laki 5 kwa miaka kibao akisubiri uteuzi.

Lkn vijana toka upinzani wamekuwa wakipiga purukushani za miaka michache tu kisha huonwa na kupewa vyeo.

Ndiyo maana wakinga wanasema:- Joining opposition wing is a short, simple and quick method of securing a post in the government led by CCM.

Sonje wa Songwe alilalamika hadharani juu ya hili. Hoja yake ikazimwa na JPM halafu wanaccm kindakindaki mkaufayata.

Mifano hii hapa:
Shonza, Gekul, Waitara, Silinde, Dr. Slaa, KAFULILA, Mkumbo, Katambi, Mghwira, Mtatiro, Mollel, na wengine wengi Sana.

Sasa wewe gamba endelea kukodoa macho huko CCM. Wenzako wameanzia upinzani ili soon walambe vyeo.
 
Unatumia vibaya haki yako ya kutoa maoni .Yaani unavuka mipaka,tukisema tuwajibu mnakimbulia kwa mods eti "nipigwe ban" huo ni uzandiki na undezi. Haya wewe unafaidika nini na Ruzuku aliyovuta mbowe tar 27 Nov 2020??🤔
 
Vijana wa CCM kwenye Corridor za Lumumba!😁
263823765.jpg
 
Hao uliowataja hapo wengi ni CCM walioenda upinzani kwa mkopo tu then wamerudi walikotoka.

Mwanampotevu akirudi nyumbani hukirimiwa kuliko watoto wengine.
 
Back
Top Bottom