Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,279
- 25,856
Mara kwa mara, vijana wa CCM wamekuwa wakifanya siasa za kilaghai na kitapeli. Kusema au kutenda uongo ni kulaghai na kutapeli.Siasa hizi zimekuwa zikinikera sana kwakuwa sipendi siasa za uongo na kutufanya watanzania hatuna akili. Leo nitawazungumzia hasa vijana wa CCM. Wakati wa sakata la Coco Beach, walijitokeza vijana wa CCM na kujipachika jina la 'Jukwaa la Wazalendo'
Hawa ni wana-CCM kwelikweli na si watu 'neutral' wanaoweza kujiita kama walivyojiita. Viongozi wa Jukwaa hilo ni Kijana Salum Ally Hapi na Kijana Mtela Mwampamba. Nani hajui kuwa hawa ni vijana wa CCM. Wamekuwa lini Jukwaa la Wazalendo,yaani wanaharakati? Katika mfumo wa kisiasa, wanaharakati hawapaswi kuwa na chama.
Jana, wamejitokeza Vijana wa CCM na kujiita 'Vijana wa CCM kutoka Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu nchini'. Vijana hawa walijitokeza katika kile kinachoonekana kama kumjibu Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe.Kiongozi na msemaji mkuu wa Shirikisho hilo ni yule yule Salum Ally Hapi.
Salum Ally Hapi namfahamu. Ni mdogo wangu hasa tulipokuwa UDSM kama wanafunzi. Nilimwacha chuoni mwaka wa pili wakati nilipohitimu. Kijana Hapi alimaliza chuo mwaka 2011. Alikuwa darasa moja na Mganda Odong Odwah.Tangu hapo hakuwa tena mwanachuo na hivyo hafai kuwa kwenye Shirikisho la Wanavyuo hata kama shirikisho hilo lipo.
Ni utapeli na ulaghai wa wazi kutumia mwamvuli batili au majina batili au hata watu batili. Kwanini Salum Ally Hapi,kijana wa CCM na wenzake wafanye ulaghai na utapeli kiasi hiki? Ndiyo yale yale ya mmoja wa wana-CCM kujiita Mwakilishi wa Walemavu Tanzania, nafasi ambayo haikuwahi kuwepo. Acheni siasa za kilaghai.