Vijana wa CCM, acheni KUTUKANA wazee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wa CCM, acheni KUTUKANA wazee

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eng. Y. Bihagaze, Jul 16, 2012.

 1. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Sidhani
  Nimesoma mabandiko humu ndani, na Kwenye vyombo mbalimbalivya habari juu ya Matamshi ya wazi wazi waliyoyatoa na wanayoendelea kuyatoa baadhi yawanachama wa CCM juu ya mageuzi ya kisiasa yanayoendelea ndani ya Chama hicho na pilika za kujikwamua kwa kile kinachodhaniwa ni kupotea kwa mvuto wa Chama mbele ya jamii.

  Wanachama hao ambao pia ni kada ya Uongozi wa CCM, wakiwemo watoto wa waliokuwa wanasiasa mashuhuri , William Malecela, Moses Nauye ,January Makamba na wengineo, kwa namna moja au nyingine wamekuwa mstari wa mbele kwa kile kinachotafsirika kwamba ni juhudi za kukinusuru Chama.

  William kwa nyakati tofauti amemnanga katibu mkuu wa CCM- W.Mukama kwamba ni mtu aliyepitwa na kasi ya mabadiliko ya Kisiasa Inayoendelea. Nakwa Mara kadhaa amemsifia Katibu mwenezi wa CCM Taifa Nape Nauye, kwamba ni mtu awezaye kutambua tatizo na kulichukulia maamuzi pasipo kumshirikisha au kusubiri ushauri kutoka kwa Mwenyekiti wake.

  Kwa nafasi hiyo, nadhani kwenye jamii yetu, mbali na wingi wa mitazamo ya kisiasa hata kiuchumi miongoni mwetu Vijana wa taifa hili, nadhani Bado tuna weledi kamili kushauriana. Vijana Hawa Lazima wajue kwamba si utaratibu wa jamii yetu ya Kitanzania Kutowaheshimu wazee wetu, na pia si-utanzania Kumchamba au kumvua nguo mtu mzima mbele ya mboni za jamii. Ketendo cha vijana hawa kuwashambulia wazee wa Chama kinatafisiriwa kama kuwavua Nguo wazee hawa ambao Hata kama Taifa au Chama hakiwaheshimu lakini Familia na watoto wao bado wanawaheshimu.

  Vijana hawa HAWAWEZI kulazimisha Chama kiende kama wao WATAKAVYO Chama kina miiko, kanuni, na taratibu. Na kabla ya kujiunga na Chama chochote Lazima Ujue Miiko yao na kipi unapaswa Utende na Kipi Usitende na si Kukurupuka na kuanza kutumia vyombo vya Habari kukandamizia udhaifu wa wazee wa chama.

  Vijana hawa wa Chama lazima wajue Wanaposhutumiana, wasisahau kila mmoja hapo amewekwa na Mamlaka Hiyo moja, na Mamlaka Hiyon ndiyo yenye maamuzi ya kujua nani mzembe imuondoe na nani abaki. Na kama wote wamewekwa na mamlaka Moja, ni mamlaka Hiyo hiyo moja inayotakiwa kuwaadabisha,na kama mamlaka husika inashuhudiaUgomvi huo na yenyewe imekaa kimya basi tatizo kubwa liko kwenye mamlaka Hiyo kwa udhaifu mkubwa wa kutowawajibisha watendaji wake. Hata ndani ya Familia baba asipoisimamia familia yake vyema Lazima watoto watapotea kimaadili.

  Vyama vya kisiasa ni kama Dini, Kama imani yako haiendani na Dini au dhehebu uliloko, huna sababu ya kuikashifu dini/dhehebu hilo uliloko,kimyakimya unajiondoa na kutafuta pale unapodhani panafaa imani yako na sikuleta matapishi kwenye ustaarabu wa wengine..

  Kama Vijana Hawa wanadhani CCM ni Chama legelege, chama ‘slow' na hakimudu kasi ya vuguvugu la kisiasa nchini kwa sasa, hakuna aliyewabatiza wawe waumini wa CCM wa milele. Nawashauri kuliko kuendelea kuwakosea adabu wazee hawa ni vema wakaangalia kule wanakodhani wao kuna kasi wanayoitaka ya kisiasa na wajiunge huko.

  Mimi si mwanachama wa CCM lakini pia si mwanachama wa Kutukana wazee.. nacholenga hapa ni kuwahakikishia wazee wetu wote kwamba si-vijana wote wa taifa hili wanaafiki mkumbo wa majibizano haya ndani ya Chama,na jamii kwa ujumla

   
 2. T

  Twigwe Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sipati picha!!! wala mvuto wa hii!!
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Pilipili usioila inakuwashia nini?
   
 4. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ugonjwa Wa mwenzio Leo ni wako kesho..
   
 5. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  wazee ndio wanaokwamisha maendeleo ya nchi hii! aaarrrggghhhh!
   
 6. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  ..
  Soma Kati ya mistari.. Utaelewa labda!!
   
 7. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Chama kikishatumbukia kwenye ufisadi, hapo hakuna kijana wala mzee. Wote lao moja. Kufisadi. Mzee anataka na kijana anataka. Heshima sio kigezo hapa. Hakuna ustaarabu hapa. Mambo ni tukana, vunja,bomoa,ua,angamiza nk. Achana nao hao wameshapotea njia. Sidhani kwamba watapokea ushauri wako.
   
 8. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Kama ndio walio kwamisha sasa kwanini vijana Kama hawa waendelee kuwakumbatia... Na kuwatukana . Basi tatizo si wazee hawa ni ugonjwa Wa vijana wasiopima Upepo Wa mabadiliko..

  Kama Chama kimedhoofu mnawaachia wenye nacho mnaangalia ustaarabu mwingine..
   
 9. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Watoto hao wanaamini kuwa chama ni chao na ndio wenye dhamana ya kushika uongozi wowote wa nchi hii kwa sababu tu eti wazazi wao waliwahi kuwa viongozi wa chama hicho. We angalia safu hizi alafu ulinganishe na kauli niliyoitoa.
  1. William Malecela ni mtoto wa Mzee John S.Malecela aliyepata kuwa waziri mkuu
  2. Livingstone Lusinde ni mtoto wa kada wa zamani wa ccm mzee Job Lusinde.
  3. January Makamba ni mtoto wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar na katibu mkuu wa ccm.
  4. Mathayo David Mathayo ni mtoto wa Mzee Cleopa David Msuya aliyewahi kuwa gavana na waziri mkuu.
  5. Nape Nnauye ni mtoto wa kada wa zamani wa ccm na pia jeshi Mzee Mosses Nnauye.
  6. Jakaya Kikwete baba yake ni mmoja wa waasisi wa Tanu na baadaye ccm.
  7. Emanuel Nchimbi naye baba yake ni mmoja wa waliowahi kuwa viongozi wa nchi hii na kada wa ccm.
  8. Adam Malima ni mtoto wa aliyewahi kuwa waziri wa fedha ndugu Kigoma Ally Malima.
  9. Husein Mwinyi ni mtoto wa aliyekuwa rais wa tz. ndugu Ally Hassan Mwinyi.
  10. Juma Khamis Kagasheki ni mkwe wa Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi.
  11. Zainabu Rashid Kawawa (Mbunge) ni mtoto wa aliyekuwa waziri Mkuu Rashid Mfaume Kawawa.
  12. Vita Rashid Mfaume Kawawa (mbunge) naye ni mtoto wa Rashid Mfaume Kawawa.

  Hao ni baadhi tu ya ambao mimi ninawafahamu. Kina Nape na wenzake hao wanahisi kuwa wao na wazazi wao walizaliwa ili kuwa viongozi wa nchi hii (Wao ni tabaka la watawala na wengine wote wasiokuwa na wazazi viongozi wabaki kuwa watawaliwa) na ndio chanzo kikubwa cha wao kuhodhi madaraka yote ndani ya chama chao. Ni kama Ridhiwani alivyo na nguvu kubwa kubwa ya maamuzi ndani ya ccm kwa kuwa tu baba yake ndiye mwenyekiti wa ccm.
   
 10. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Jisachi
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wewe Mwigulu,

  Hoja yako hii ya kuwatafuta UCHAWI baadhi ya vijana wa CCM wenye fikra huru ni bora ukatundike madai yako hayo kuleeee Lumumba mlikozoea KUPAKANA MAFUTA MGONGO WA CHUPA huku mkifichana ukweli.

  Huwezi kutarajia mabadiliko ndani ya chama chenu kwa kuendekeza TABIA TUICHUKIAYO KUFA YA KUITA BELESHI KUWA NI 'KIJIKO KIKUBWA'.
   
 12. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Chama wakishapewa wakina NAPE kwishne , wananchama wote waliobaki watageuka Oil chafu.
   
 13. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini haya watoto wanaharibu chama chetu kweli!
  Limekuwa pango la majambazi na mijizi, mkama ameshindwa kubadilisha chama sijui kwanini hajiudhuru tuu!
   
 14. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,491
  Trophy Points: 280
  hawa vijana wa ccm wamepitia wapi hadi kufika kwenye uongozi wengi wamebebwa kutokana na nyazifa walizokuwa nazo hawajui kijana kweli wa Tanzania anaishi vipi na kwa sababu wazazi wao walikuwa viongozi wanaamini hakuna mtu mwingine zaidi ya wao anayeweza kuongoza nchi vizuri.
  Tatizo la nchi yetu kiongozi halihusiani na wazee au vijana bali ni kuvunjwa kwa maadili ya uongozi kwani hata hao wazee tunaowalaumu ndio vijana waliokuwa wanaamini wakipewa nchi watafanya vizuri ni hoja dhaifu kuamini kuwa kundi fulani ndicho chanzo cha matatizo yetu hao vijana ndio walishiriki kiasi kikubwa kumchafua aliyekuwa Katibu mkuu wa Un ambaye bila ubishi alikuwa na ubora mkubwa kuliko kiongozi aliyechaguliwa katika nafasi hiyo
  tuache kutafuta visingizio tuwe na maadli ya uongozi,tuipe katiba kinga anayeivunja ashugulikiwe na mahakama tukiwa na katiba bora hata rais bila kujali umri au jinsia atatekeleza kile ambacho watanzania wanataka
   
Loading...