Vijana wa CCM, acheni KUTUKANA wazee WENU.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wa CCM, acheni KUTUKANA wazee WENU..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eng. Y. Bihagaze, Jul 16, 2012.

 1. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Sidhani
  Nimesoma mabandiko humu ndani, na Kwenye vyombo mbalimbalivya habari juu ya Matamshi ya wazi wazi waliyoyoyatoa na wanayoyatoa baadhi yawanachama wa CCM juu ya mageuzi ya kisiasa yanayoendelea ndani ya Chama hichona pilika za kujikwamua kwa kile kinachodhaniwa ni kupoteza kwa mvuto wa Chamambele ya jamii.

  Wanachama hao ambao pia ni kada ya Uongozi wa CCM, wakiwemoWatoto wa waliokuwa wanasiasa mashuhuri , William Malecela, Moses Nauye ,January Makamba na wengineo, kwa namnamoja au nyingine wamekuwa mstari wa mbele kwa kile kinachotafsirika kwamba nijuhudi za kukinusuru Chama.

  William kwa nyakati tofauti amemnanga katibu mkuu wa CCM- W.Mukama kwamba ni mtu aliyepitwa na kasi ya mabadiliko ya Kisiasa Inayoendelea. Nakwa Mara kadhaa amemsifia Katibu mwenezi wa CCM Taifa Nape Nauye, kwamba ni mtuawezaye kutambua tatizo na kulichukulia maamuzi pasipo kumshirikisha Mwenyekitiwake.

  Kwa nafasi hiyo, nadhani kwenye jamii yetu, mbali na wingiwa mitazamo ya kisiasa hata kiuchumi miongoni mwetu Vijana wa taifa hili, nadhaniBado tuna weledi kamili wa kushauriana. Vijana Hawa Lazima wajue kwamba siutaratibu wa jamii yetu ya Kitanzania Kutowaheshimu wazee wetu, na pia siutanzania Kumchamba au kumvua nguo mtu mzima mbele ya mboni za jamii. Ketendo chavijana hawa kuwashambulia wazee wa Chama kinatafisiriwa kama kuwavua Nguo wazeehawa ambao Hata kama Taifa au Chama hakiwaheshimu lakini Familia na watoto waobado wanawaheshimu.

  Vijana hawa HAWAWEZI kulazimisha Chama kiende kama waoWatakavyo, Chama kina miiko, kanuni, na taratibu. Na kabla ya kujiunga na Chamachochote Lazima Ujue Miiko yao na kipi unapaswa Utende na Kipi Usitende na siKukurupuka na kuanza kutumia vyombo vya Habari kukandamiza udhaifu wa wazee wetu ambao tunawaheshimu.

  Vijana hawa wa Chama lazima wajue Wanaposhutumiana wao kwawao wasisahau kila mmoja hapo amewekwa na Mamlaka Hiyo moja, na Mamlaka Hiyondiyo yenye maamuzi ya kujua nani mzembe imuondoe na nani abaki. Na kama wotewamewekwa na mamlaka Moja, ni mamlaka Hiyo hiyo moja inayotakiwa kuwaadabisha,na kama mamlaka husika inashuhudiaUgomvi huo na yenyewe imekaa kimya basi tatizo kubwa liko kwenye mamlaka Hiyokwa udhaifu mkubwa wa kutowawajibisha watendaji wake. Hata ndani ya Familia baba asipoisimamiafamilia yake vyema Lazima watoto watapotea kimaadili.
  Vyama vya kisiasa ni kama Dini, Kama imani yako haiendani naDini au dhehebu uliloko, huna sababu ya kuikashifu dini/dhehebu hilo uliloko,kimyakimya unajiondoa na kutafuta pale unapodhani panafaa imani yako na sikuleta matapishi kwenye ustaarabu wa wengine..

  Kama Vijana Hawa wanadhani CCM ni Chama legelege, chama ‘slow' na hakimudu kasi ya vugivugu lakisiasa nchini kwa sasa, hakuna aliyewabatiza wawe waumini wa CCM wa milele. Nawashaurikuliko kuendelea kuwakosea adabu wazee hawa ni vema wakaangalia kulewanakodhani wao kuna kasi wanayoitaka ya kisiasa na wajiunge huko.

  Mimi si mwanachama wa CCM lakini pia si mwanachama waKutukana wazee.. nacholenga hapa ni kuwahakikishia wazee wetu wote kwamba sivijana wote wa taifa hili wanaafiki mkumbo wa majibizano haya ndani ya Chama,na jamii kwa ujumla
   
Loading...