Vijana wa Bara Wapewa Vitambulisho Vya Ukaazi Z'bar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wa Bara Wapewa Vitambulisho Vya Ukaazi Z'bar?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Aug 3, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mpoki Bukuku, Pemba na Salim Said

  CHAMA cha wananchi (CUF) kimedai vitambulisho vya ukaazi vinatolewa kwa vijana wa bara ili waweze kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwakani.

  Akizungumza Mjini Wete, mbunge wa viti maalum wa chama hicho, Riziki Omar Juma, alidai kwa sasa baadhi ya vijana wameshapatiwa vitambulisho kwajili yakujiandikisha kupiga kura mwakani na wengine wanatarajiwa kuingia Zanzibar wakati wa mbio za mwenge.

  "Sasa umefika wakati wa kuwashughulikia watu hawa kwani wapemba wakiwa na chao wanatoa kwa hiari si kwa nguvu," alisema na kuongeza kuwa vijana wajihadhari wakati wa mbio za mwenge kwani vijana wengi wataletwa na kusambazwa sehemu mbalimbali.

  Akizungumzia suala hilo Katibu Mkuu wa CUF, alisema kuwa wabara wengi wamekuwa wakipewa vitambulishio hivyo na Wapemba wakiachwa bila ya kitu kinachowasababisha kupoteza haki ya kupiga kura.

  Alitoa mfano wa baadhi ya mikoa ambako kuna mvuto kwa chama cha CUF ambako maelfu ya wananchi wamezuiwa kupata fomu za vitambulisho hivyo kwa madai kuwa hawana sifa, lakini maeneo mengine ya CCM kila mtu anapatiwa.

  Wakati huo huo wazee wanaotetea kujitenga kwa kisiwa cha Pemba, wameitaka Jumuiya ya Umoja wa Mataifa (UN) kuingilia kati zoezi la uboreshaji wa daftari la wapigakura kisiwani humo, ili kuepusha maafa makubwa ambayo yanaweza kusababishwa na zoezi hilo.

  Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Msemaji wa wazee hao Hamad Ali Mussa alisema, tayari wameiandikia UN barua (nakala tunayo) wakiitaka kuingilia kati zoezi hilo na kwamba waliifikisha ofisi za UN jijini hapa siku ya Julai 30 mwaka huu.

  Alisema, UN kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) iliahidi kubeba jukumu la kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar mwakani utakuwa huru na wa haki na haitavumilia Taasisi yoyote itakayoonekana kwamba inataka kuhatarisha amani kwa kuchafua uchaguzi huo.

  "Usajili wa wapigakura ni hatua muhimu ya mchakato wa uchaguzi mkuu, tayari kuna ushahidi wa kutosha kwamba mchakato huu umeshavurugwa na unaendelea kuvurugwa vibaya," alisema na Mussa na kusisitiza:

  "Kwa hivyo tunaiomba mamlaka ya UN kuingilia kati zoezi hilo katika hatua hii ya awali ambapo ni muda mzuri bado, ikitokea juhudi za UN kusimamia uchaguzi visiwani Zanzibar kushindwa, tunaiomba kutumia nguvu zake kuizuia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kufanya uchaguzi mkuu mwakani hadi hapo madai yao yatakapotekelezwa".

  Alisema, unyama wote unaofanywa na SMZ katika usajili wa wapigakura unafadhiliwa na UN kupitia UNDP na kwamba mabaya yoyote yaliyotokea, yanayotokea na yatakayoendelea kutokea lawama zake zitabebwa na Umoja huo.

  "UN ikae ikijua kwamba damu ya kwanza kumwagika kwa ajili ya kutetea demokrasia ya vyama vingi nchini ni ya Kisiwa cha Pemba, hivyo kama inapuuzia hilo basi ituachie sisi tuliwe na samaki na hao wachache watakaobakia itakuja kuwabwagia 'vibiskuti' na mahema," alisema kwa uchungu Mussa.

  Kwa upande wake Katibu wa wazee hao Ali Makame alisema kwa sasa hawako tayari kuvumilia kuona haki yoyote ya watu wa kisiwa hicho ikidhulumiwa na utawala wa SMZ.

  Alisema, kinachofanywa Pemba hivi sasa katika zoezi la kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura ni unyama na uvunjaji wa katiba ambao matokeo yake ni kutoweka kwa utulivu na amani ya kisiwa hicho.


  SOURCE: MWANANCHI.
   
  Last edited by a moderator: Aug 3, 2009
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Wajitayarishe kuuwawa kwa tairi na petroli kama vibaka, Tumechoka!
   
 3. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  unamaana watu wa TANGANYIKA washaanza kuvamia kule visiwa vidogo vidogo?

  tatizo la wa Tanganyika wanasahau sana historia ya kule visiwani ambako watu wanavumilia wee baadae wakichoka damu inaanza kumwagwa
   
 4. K

  Kitoto Akisa Member

  #4
  Aug 3, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo la wa Tanganyika wanasahau sana historia ya kule visiwani ambako watu wanavumilia wee baadae wakichoka damu inaanza kumwagwa[/QUOTE]

  Game wabara wanasahau pia kuwa chokochoko mchokoze pweza, binadamu hutamuweza! linakuja hilo
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na onyo ndo limeshatolewa mara hii hao mamluki wakishapiga kura tu, tairi na nimedokezewa kuwa kuna "vibabu" vimekasirika sana vinasema kila kituo watahakikisha wanaweka "zindiko la nguvu" kwa kuwa watu woootea wanajuwana akionekana mgeni tu "zindiko" litamuandama mpaka anakokwenda, atakuwa baradhuli maisha yake, kwa hivyo mkiona baada ya uchanguzi mkuu wa 2010 mabaradhuli wameongezeka mjini ndo hivyo tena.
   
 6. BabaBabuu

  BabaBabuu Member

  #6
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  huku bara hakuna kabisa wazanzibari, ndo maana watanganyika hawalalamiki kabisa. ama kweli mdebwedo kwa malalamiko, ndoa mwaipenda talaka mwaitaka arrrrrggggh
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Nyani!!??
   
 8. C

  Calipso JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kwa kweli inauma tena inauma saana lkn lenye mwanzo halikosi mwisho,kama hivo vibaraka vishazowea kupewa vijisenti na hao ccm safari hii zitzwatokea puani,waanze kuangalia hivi sasa watu walivokuwa na jazba huko,asiesikia la mkuu huvunjika guu, waznz wamechoka na hawatavumilia kabisa safari hii,ngoma itakavopigwa ndivo itakavochezwa.. waambieni ndugu zenu watanganyika watakuja kuuta safari hii..
   
 9. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Siyo siasa za kichawi ww chukuwa hicho kitambulisho cha ukaazi halafu njoo zako Pemba kule ukapige kura yako ya kimamluki kisha shwari urejee zako nyumbani ukipunga mkono wanaume wakushughulikie, utajuwa kama siasa za uchawi zipo au hapana, mm nimedokezwa kuwa vibabu vilevile vilivyo kwenda kuwachokonoa "mapopo bawa uvundo" yakashikisha adabu kwelikweli, nafikiri mnakumbuka yule kijana wa Kipemba aleyetapeliwa mamilioni na vijana wa Mbagala kule alivyofanya, alikwenda kwao kwa vibabu vile kuomba msaada wa "kitaalamu" na "mapopo bawa" unajuwa yalivyoshikisha adabu kule Mbagala.
  Kama hujasahau utakuwa unakumbuka rais Mstaafu Mkapa(fisadi papa No.6) alivyoteguliwa kiuno na vibabu vile. Shauri yako,
   
 10. BabaBabuu

  BabaBabuu Member

  #10
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  nyani mzee wa bara ahahahahahaha. weye wa wapi, unguja? Sylva Sylvarum
   
 11. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  CUF wameshajichokea sasa wanataka huruma ya wananchi.
  Hivi wabara hawaruhusiwi kuishi Zanzibar?
   
 12. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ifahamu nukta hii katika muktadha huu kuwa vitambulisho hivyo vinatolewa si kwa malengo kama ya sheria inavyosema kuwa kila mwenye sifa na haki apewe, bali kwakuwa vimeingizwa katika mchakato wa uchaguzi inaonekana hata wasiokuwa na sifa na haki watapewa mradi tu watakipigia kura chama tawala, si hao tu kutoka bara kuna Wakenya wanafanya kazi mahotelini huko wameshatayarishwa kupiga kura mpaka katika kambi za vikosi vya SMZ ambako wao siyo askari kabisaaaa lakini watapewa vitambulisho hivyo kwa mintarafu hiyo, utasema na hawa hawana haki ya ukaazi?
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Naomba niendelee kuamini kuwa haya ni madai tu mpaka yatakapothibitishwa pasi na shaka
   
 14. M

  Mvutakamba Member

  #14
  Aug 3, 2009
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama madai haya ni ya kweli basi nashauri wagunga akina Mwiba wakomae na hawa wasaliti kwa sana ili watu wapige kura na si kulazimisha kuchahua Chama .
   
 15. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Matters of allegetion are proved on balance of probability, and that is what CUF has already done.
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Aug 3, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Huyu shariff hamad anaaminiwa mno na wapemba, hata akiongea pumba wanaamini ni kweli. Atawahadaa kwamba 'tuko tayari kwa lolote' lakini vikianza kutokueleweka yeye anapanda pipa na kuwaacha kwenye matatizo!
   
 17. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hao vijana wa bara (Tanganyika) wamekuwepo huko kwa muda gani? Je endapo wametimiza muda unaotakiwa kisheria kutambuliwa kama wakazi hawana haki ya kupata vitambulisho vya ukazi? Kwani ni haramu kwa wanaoitwa vijana wa bara kuwa na haki za ukazi Zanzibar?

  Ni kweli kuwa CCM wanacheza sana rafu huko na ahswa katika zoezi hili ambapo tayari kituo cha sheria za zanzibar kimefungua kesi kadhaa huko unguja kuhusiana na suala hilo lakini pia ni wajibu wetu kuwa makini katika kutoa malalamiko yetu.

  Kama ambapo "vijana wa kizanzibari" wana haki za ukaazi Tanganyika na pia vijana wa kitanganyika (kibara) wana haki za ukaazi Zanzibar. Hayo ndio matamu na machungu ya muungano na mfumo wa demokrasia ambao wengi wetu hapa tunapenda kujinasabisha nao.

  omarilyas
   
 18. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Wanaopewa ni mamluki kwa lengo la kuwapigia kura chama mahututi CCM hakuna masuala ya haki ya ukaazi au kutokuwa wakaazi na kwa taarifa tu ni kuwa vijana hao wengine tayari wameshaletwa huko na karibuni zitafunguliwa kambi katika vikosi vya SMZ kwa kisingizio cha "recruitment" na watawahifadhi huko, mambo ya utamu na uchungu wa muungano ndo yawe kulazimisha lazima CCM ibaki madarakani kwa kutumia wapiga kura mamluki, kama muungano wenyewe itakuwa hivyo Wazanzibar hawana haja nao, simply, unakwaza demokrasia ya uchaguzi huru na haki.
   
 19. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  This morally bankrupt, riot inciting, politically misguided thinking and entertainment of unconstitutional ideas must not be allowed to prevail amongst serious union watchers, well wishers and even mrere peaceable Tanzanians .

  Tanzania did away with the requirement of travel documents some years ago (For Tanzanians from mainland to go to Zanzibar) due to it's unconstitutionality, while I condemn any political machination aimed at some less than honorable electioneering, I equally condemn any attempt to infringe upon the people of Tanzania's constitutionally guaranteed freedom of movement within the United Republic, and last time I checked Zanzibar was part of The United Republic.

  I recognize - given the history of Zanzibari elections- that there may be a legitimate concern presented, nevertheless this concern must be addressed with means confined to the categorical upholding of not only the letter of our Union Constitution, but also the spirit behind this central document.

  Restriction of movement, or any such bureaucratic Orwellian construct, will only serve to restrict people's freedom, encourage regionalism and factionalism, incite torrents of oscillating reciprocal rebuttals (What if mainland Tanzanians require the same documentation for all Zanzibaris?) and this will only lead to a more combustive atmosphere.

  If there is an issue of election fraud, let us deal with the issue without introducing other and quite possibly bigger issues.
   
 20. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kwenye hiyo process ya kuwachoma muangalie tu msije mkaanza kuuana wenyewe kwa wenyewe kwa kukisia mtu ni mamluki.
   
Loading...