Vijana wa Arusha, chuki ya nini kwa wenzenu wa Dar? Mkubwa atabaki kuwa Mkubwa tu

smarte_r

JF-Expert Member
Nov 8, 2013
4,538
11,868
Nimeandika uzi huu baada ya kuvutiwa na mjadala unaondelea kwenye uzi wa APPROXIMATELY: ARUSHA, nakupenda sana, najivunia kuzaliwa Arusha...

Licha ya jiji la Dar kuwa na hali ya hewa ya joto kwa kipindi kirefu cha mwaka, hali ambayo sio rafiki kwa baadhi yetu, Mungu ana kusudi lake kulifanya jiji hili liwe the capital city of Tanzania.

Utake usitake, Dar ni jiji namba moja la kibiashara nchini na Afrika Mashariki likicheza ligi moja na Nairobi, Kampala na Kigali.

Ni jiji ambalo kila mtu kutoka kila kabila lake, anapatikana na kufanya shughuli zake za kiuchumi kwa amani bila kusimangwa au kubugudhiwa na wenyeji ambao ni wazaramo, wandengereko na wakwere.

Niseme tu ukweli, watu wa Pwani licha ya mapungufu yao machache, ni wastaarabu, waungwana na wakarimu sana. wenyeji wa mji huu wamewakaribisha na kuwakarimu wageni wengi waliohamia Dar na kupageuza kuwa makazi yao ya kudumu.

Dar ni jiji la fursa, jiji la kutengeneza network na connection za kutoboa kimaisha kupitia wadau mbalimbali utakao kutananao kwenye mishe zako. Huwa naifananisha Dar na taifa la Marekani kupitia ile concept yao ya chasing the American Dream.

Kama wewe ni kijana uliyeweka malengo ya kufanikiwa kupitia talent mbalimbali hususani uigizaji au mziki, utake usitake lazima utoke mkoani kwenu uje dar ujiweke karibu na big fish wa industry husika.

Mfano mdogo ni wasanii wa Arusha kama Dogo Janja, Joh Makini na wenzake wa kundi la weusi. Hawa wote wamefika hapo walipofika baada ya kuhamia Dar halafu wakashikwa mkono na watoto wa mjini wa jiji hili(sina haja ya kuwataja, jamii inajua).

Laiti kama Arusha ndio ingekuwa the main capital city ya Tanzania kama lilivyo jiji la Dar, basi vijana wa mikoa mingine ambao wangehamia Arusha, wangeishi kwa manyanyaso sana kutoka kwa vijana wazawa wa Arusha. pengine wangefukuzwa warudi makwao na labda tungekuwa tunashuhudia xenophobic incidents kama zile za South Africa.

Nalisema hili kwasababu ya arrogant, rude behaviour and uncivilised culture ya vijana wa Arusha. Hapo kwenye uncivilised culture wote ni mashahidi wa ile tabia yao kuvuta bangi kiholela na kijisifiia kana kwamba ni ufahari.

Pia ile dress code yao ya kuvaa mashati oversize na mabuti makubwa. Nakumbuka huu uvaaji walikuwa wanavaa vijana wa Dar katikati na mwishoni mwa90s. For now this dress code style is out of date.

Mtindo huu wa uvaaji ulichochewa na wasanii wakubwa wa mziki wa rap huko Marekani. Ni miaka ambayo Dr Dre na Snoop Dogg walikuwa wanatamba na ngoma yao ya nuthin' but a "G" thang, the late 2pac akitamba na me against the world.

Jambo lingine ni tabia ya chuki na kujiona superior dhidi ya vijana wenzao wa mikoa mingine specifically wa Dar.

Mimi ni mhanga wa hili, huwa natembelea Arusha mara nyingi tu. Kuna siku niliingia duka moja la kuuza viatu, wale vijana walinipokea vizuri tu. Ila baada ya kusikia kiswahili changu na kugundua natokea Dar, customer care yao ikabadilia ghafla. Wakajifanya kama hawanisikii nilipokuwa nawaongelesha. Mbaya zaidi wakapandisha bei ya viatu ili wanikomoe. Nikaondoka zangu.

Sio hilo tu, hata unapotembelea maeneo ya starehe ndani ya Arusha, kama meza yako ipo jirani na meza ya vijana wenyeji halafu wagundue wewe ni wa Dar, kuna chuki flani unaiona machoni mwao, wanapoteza uchangamfu.

Ni kweli hali ya hewa ya Arusha ni nzuri na mji unapata wageni wengi wa kimataifa wanaokuja kufanya utalii, bado Dar itabaki kuwa juu na bado vijana wa Dar watabaki kuwa na exposure kubwa dhidi yenu.

Karibu kwenye mjadala. Changia kwa lugha ya staha.
 
Mi na watu hao tofauti japo nishakutana nao nawaona wa zamani sana bado wako jamii ya miaka ya zamani. Hawana confidence ya kusimama mmoja kama mmoja wanapenda kuingiza ukabilaz ukanda, hawana cha maana nguo hawajui kujipangilia kuvaa manguo mazito kama bodaboda kifupi hawapendi na fashion.

Shobo kibao mbele ya wazungu
 
Ila madem wa arusha wanawakubali sana watu dar. Hua nukiendaga arusha kiswahili yangu tu hii nawang'oa sana yaani ni kama kenya tu au uganda.
Wanawakubali vijana wa Dar kwasababu wapo romantic halafu ni wabembelezaji wazuri.

Kuna wakati watoto wa kike wanapenda kubembelezwa na kudekweza kidogo.

Vijana wa Arusha hawawezi mambo hayo, wao mapenzi ni kama vita kuanzia utongozaji mpaka mda wa ku-Do. kila kitu wana demand.
 
Dar inatakiwa isifiwe na wazawa halisi na sio nyie mlioenda Dar kwa magari ya ng'ombe na Treni ya kati.
Japo wazazi wangu kiasili sio wenyeji wa Dar, mimi ni mwana Dar es salaam halisi, mtoto wa mjini, born town, nilizaliwa Muhimbili national hospital miaka kadhaa iliyopita.

Utoto na ujana wangu wote nime spend Dar, primary, secondary(o-level na high level) mpaka Chuo Kikuu nimepiga Dar.

Halafu hunielezi kitu kuhusu TZ yangu, naijua vizuri sana. sijajifunga eneo moja, nimefika sehemu kubwa sana ya nchi hii.

Mkoa ambao sijafika mpaka sasa ni Rukwa na kisiwa cha Pemba, soon nitafika.

Hiyo Arusha yenu nimefika mara nyingi sana japo huwa naishia katikati ya mji, kule pembezoni kwenye zile neighborhood zenu za uswahilini bado sijafika. Siwezi kufika huko kwa kuhofia usalama wangu maana wengi wenu ni vibaka na wakabaji.

Hapa chini nakuwekea picha kutoka google map ikionyesha baadhi ya maeneo niliyofika ndani ya Tz. Mwezi may nilikuwa Kigoma kwa siku chache, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufika mkoa huo. Bahati mbaya sana nilisahau kuwasha GPS, ndio maana kwenye picha hii haionyeshi kama nimefika Kigoma.

IMG_20220925_114623.jpg
IMG_20220925_114623.jpg
IMG_20220925_114641.jpg
 
japo wazazi wangu kiasili sio wenyeji wa dar, mimi ni mwana dar es salaam halisi, mtoto wa mjini,born town, nilizaliwa muhimbili national hospital miaka kadhaa iliyopita.

utoto na ujana wangu wote nime spend dar,
primary, secondary(o-level na high level) mpaka chuo kikuu nimepiga dar.

halafu hunielezi kitu kuhusu tz yangu, naijua vizuri sana. sijajifunga eneo moja, nimefika sehemu kubwa sana ya nchi hii.

mkoa ambao sijafika mpaka sasa ni rukwa na kisiwa cha pemba,soon nitafika.

hiyo arusha yenu nimefika mara nyingi sana japo huwa naishia katikati ya mji, kule kwenye neighborhood zenu uswahilini sijafika bado.

hapa chini nakuwekea picha kutoka google map ikionyesha baadhi ya maeneo niliyofika ndani ya tz. mwezi may nilikuwa kigoma kwa siku chache, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufika mkoa huo. bahati mbaya sana nilisahau kuwasha GPS, ndio maana kwenye picha hii haionyeshi kama nimefika kigoma.
View attachment 2367480View attachment 2367481
Kaka Smarter ukimalizana na hao uje na huku uzungumze na akina mwaisa uwaeleze sio kila aliyezaliwa dar ni mjanja mjanja na ni muhuni kama wadhanivyo
 
Back
Top Bottom