Vijana tusipo oa tunasemwa, tukitaka kuoa mnatupangia mahali kubwa

Muuza simu used

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
3,725
2,000
Wakuu habari za weekend!

Moja kwa moja kwenye mada, nimekuwa nikisotea mke wa kuoa muda mrefu sana hata humu nilishawahi kutafuta japo sikupata nimekuja kumpata mtaani kwangu.

Huyu binti ananipenda sana na mimi nampenda, akasema nitume mtu kwao nikatuma mshenga, wakati huo kila mtu alikuwa ana getto lake, baada ya mshenga kunipa majibu nikamwambia nimepangiwa mahari 3.6 millions, kiukweli wakati namwambia sura na akili yangu ilikuwa mbali sana na uzuri anafahamu kipato changu licha ya kuwa ni mwajiriwa lakini hakitoshi.

Niliona anaingiwa huruma akafikia kuniambia anatamani tuanze kuishi, nikaona sio issue akahamia kwangu hadi sasa. Ndg zake ameshakuja home, ila mzee wake kafichwa hadi sasa wanasubili nikatoe mahari na mimi mambo bado.

Kila nikijipanga mipango inapanguka, sio siri hicho kiasi kinanisumbua akili licha ya kuwa nimeambiwa mahari haimalizwi !

Wadau na wajuvi wa mambo haya naomba uzoefu wenu nifanye hatua gani kunusuru mahusiano yangu?

Acha ujinga,mahari hata ukiambiwa milioni 10,isitoe zaidi ya laki 4 hizo zingine zilizobaki utalipa mwisho wa dunia
 
Amigoh

JF-Expert Member
May 15, 2016
782
1,000
Wakuu habari za weekend!

Moja kwa moja kwenye mada, nimekuwa nikisotea mke wa kuoa muda mrefu sana hata humu nilishawahi kutafuta japo sikupata nimekuja kumpata mtaani kwangu.

Huyu binti ananipenda sana na mimi nampenda, akasema nitume mtu kwao nikatuma mshenga, wakati huo kila mtu alikuwa ana getto lake, baada ya mshenga kunipa majibu nikamwambia nimepangiwa mahari 3.6 millions, kiukweli wakati namwambia sura na akili yangu ilikuwa mbali sana na uzuri anafahamu kipato changu licha ya kuwa ni mwajiriwa lakini hakitoshi.

Niliona anaingiwa huruma akafikia kuniambia anatamani tuanze kuishi, nikaona sio issue akahamia kwangu hadi sasa. Ndg zake ameshakuja home, ila mzee wake kafichwa hadi sasa wanasubili nikatoe mahari na mimi mambo bado.

Kila nikijipanga mipango inapanguka, sio siri hicho kiasi kinanisumbua akili licha ya kuwa nimeambiwa mahari haimalizwi !

Wadau na wajuvi wa mambo haya naomba uzoefu wenu nifanye hatua gani kunusuru mahusiano yangu?
Mlaumu mshenga..
 
The real Daniel

JF-Expert Member
Jan 5, 2017
1,721
2,000
Ok, Kwan wewe unakiasi gani?

Ninachojua Mimi, pesa ambazo unatakiwa kulipa zote Ni ambazo ziko nje ya mahali Kama vile( kabila letu) pesa ya mama, suti, blanketi na pesa nyingine zote ndogondogo.

Kwenye mahali unalipa kidogo tu.
Mfano Mimi nilipangiwa 1.5m Ila nilitoa laki 4 tu, nikasema zingine nitamalizia.
Ikaisha hivyo

Ila ikitokea shida kwao ya pesa za kawaida Kama elfu 20 mpaka 50 huwa nawasaidia Kama Nina uwezo na Ni mara chache Sana.

Chunguza utaratibu wa ukoo wao kwa kumuuliza mkeo au watu wa karibu.

Wakigoma kupokea pesa uliyonayo HIYO NI DALILI MBAYA either wamekuona unapesa Sana, au wamekuona umempenda Sana mtoto wao hivyo hauwezi kuchomoa hata wakukazie vipi au ni tabia yao.
 
Amigoh

JF-Expert Member
May 15, 2016
782
1,000
Mahari ni kitega uchumi cha familia sikuhizi

Wanawake wanalalamika wanaume wa kuoa wapo wachache ila akitokea jamaa akatangaza ndoa, anapigwa milioni 5,.
Hizi mahari zifutwe tu, hazina maana tena, kama ni shukrani kwa kumtunza binti yao, wengi wamefeli kutunza mabinti zao.
Wakati mwingine unakuta wewe muoaji umetunzwa kuliko huyo binti.
.. We acha tu sema ukishapenda umependa mkuu hata kama ni mchafu kuliko bata
 
Statistics

JF-Expert Member
Sep 22, 2013
1,544
2,000
3.6 unapata Carina used safi kabisa.
Nakushauri ununue boda mbili uanze kula pesa. Ndani ya mwaka umekusanya m5 unaoa kwa laki 6.
 
Tr Paul

Member
Mar 18, 2020
83
125
Ok, Kwan wewe unakiasi gani?

Ninachojua Mimi, pesa ambazo unatakiwa kulipa zote Ni ambazo ziko nje ya mahali Kama vile( kabila letu) pesa ya mama, suti, blanketi na pesa nyingine zote ndogondogo.

Kwenye mahali unalipa kidogo tu.
Mfano Mimi nilipangiwa 1.5m Ila nilitoa laki 4 tu, nikasema zingine nitamalizia.
Ikaisha hivyo

Ila ikitokea shida kwao ya pesa za kawaida Kama elfu 20 mpaka 50 huwa nawasaidia Kama Nina uwezo na Ni mara chache Sana.

Chunguza utaratibu wa ukoo wao kwa kumuuliza mkeo au watu wa karibu.

Wakigoma kupokea pesa uliyonayo HIYO NI DALILI MBAYA either wamekuona unapesa Sana, au wamekuona umempenda Sana mtoto wao hivyo hauwezi kuchomoa hata wakukazie vipi au ni tabia yao.
Nimeipenda falsafa yako 1.5 M had I laki 4 sawa na 26.6% ,,very relevant
 
Mtukutu wa Nyaigela

JF-Expert Member
Sep 4, 2018
3,453
2,000
Toa robo sio nusu mwambie nyengine utamaliza ndo imetoka hio

Au mimba tu kama jamaa hapo juu alivyosema

Ukizishindwa hzo njia last option mwambie binti aongee na kwao we huna uwezo wapunguze Si anataka aolewe ataongea nao tu maana sio wazazi wanao olewa

Ikishindikana piga chini tafuta mwengine acha tabia ya sogeza tuishi huwez kaa na mtoto wa mtu bila ridhaa ya wazazi wake mikosi mingine ni ya kujitakia

Ngoja nikanywe bia we endelea kusubir michango mingine
Umeshauri vizuri sana.
Mahari ni negotiable mkuu. tafuta mwenye skills ya kuongelea hiyo mahari. kisha waambie una milioni moja na nyingine utalipa siku za mbeleni
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom