Vijana tusipo oa tunasemwa, tukitaka kuoa mnatupangia mahali kubwa

Hendisamu

JF-Expert Member
May 9, 2019
319
500
Wakuu habari za weekend!

Moja kwa moja kwenye mada, nimekuwa nikisotea mke wa kuoa muda mrefu sana hata humu nilishawahi kutafuta japo sikupata nimekuja kumpata mtaani kwangu.

Huyu binti ananipenda sana na mimi nampenda, akasema nitume mtu kwao nikatuma mshenga, wakati huo kila mtu alikuwa ana getto lake, baada ya mshenga kunipa majibu nikamwambia nimepangiwa mahari 3.6 millions, kiukweli wakati namwambia sura na akili yangu ilikuwa mbali sana na uzuri anafahamu kipato changu licha ya kuwa ni mwajiriwa lakini hakitoshi.

Niliona anaingiwa huruma akafikia kuniambia anatamani tuanze kuishi, nikaona sio issue akahamia kwangu hadi sasa. Ndg zake ameshakuja home, ila mzee wake kafichwa hadi sasa wanasubili nikatoe mahari na mimi mambo bado.

Kila nikijipanga mipango inapanguka, sio siri hicho kiasi kinanisumbua akili licha ya kuwa nimeambiwa mahari haimalizwi !

Wadau na wajuvi wa mambo haya naomba uzoefu wenu nifanye hatua gani kunusuru mahusiano yangu?
 
MLEVi Mmoja

JF-Expert Member
Jun 29, 2019
7,037
2,000
Toa robo sio nusu mwambie nyengine utamaliza ndo imetoka hio

Au mimba tu kama jamaa hapo juu alivyosema

Ukizishindwa hzo njia last option mwambie binti aongee na kwao we huna uwezo wapunguze Si anataka aolewe ataongea nao tu maana sio wazazi wanao olewa

Ikishindikana piga chini tafuta mwengine acha tabia ya sogeza tuishi huwez kaa na mtoto wa mtu bila ridhaa ya wazazi wake mikosi mingine ni ya kujitakia

Ngoja nikanywe bia we endelea kusubir michango mingine
 
Sawa Mkuu ila kuhusu kupunguza nilishamwambia akaongea na mama ake lakini sikuoata jibu !

Uko wapi nije kukuongeza masanga Mkuu!
 
Hannah

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
4,842
2,000
Mtie mimba mkuu, utajipangia mahali mwenyewe
Kuna kijana alidhani kumtia mimba binti ndio atapewa mke kirahisi rahisi.
Wazazi wakakomaa.
Mtoto akazaliwa, mwanaume anadhani atapewa mwanamke lakini wapi.
Kosa alilolifanya alipigwa marufuku kutia mguu nyumbani kwa mwanamke. Mtoto akafikisha miaka miwili mwanaume haamini macho yake.
Ilibidi akaombe, alipe mahari na faini(hela ya matunzo ya mtoto yangu alipozaliwa) wakafunga na ndoa wakakabidhiwa mtoto sasa.

Kuna wazazi hawachezewi nyie, labda ujiandae kukaa mbali na mtoto wako hadi siku akutafute mwenyewe.
 
Requal

JF-Expert Member
Jun 5, 2020
901
1,000

Huyo mwanaume nae boya uniendeshe hivo, nachukua mwingine nakuachia wenu na nina uhakika baada ya mda nitaendelea kumla tena Kama nyumba ndogo.
 
Mtoto wa Golden Paste

Senior Member
Jul 7, 2020
167
250
Iko hivi cha kufany kwa sasa nikumuweka binti wazi kuhusu kipato chako na kisha aweze kuwaeleza wazazi wake juu ya hilo angalau wapunguze mahari maana hiyo ni pesa nyingi sana.

Pia kumbuka utaishi na uhalisia wa mtu si muonekano wake usije ukatoa mahari kubwa kwa kujua yuapendwa sana kumbe mwenzako ana lake moyoni baadae ukajajutia juu ya maamuzi yako na kuanza kuumia kwa pesa uliyopoteza kwenye mahari. Hivyo fanya maamuzi sahihi kwanza kwa upande wa wazazi wa binti.

Kumpa mimba sio suluhisho la kupunguziwa mahari au kupewa mke bure mkuu.... just think deeply.
 
Bwana kaduga

JF-Expert Member
Apr 18, 2018
786
1,000
Chakwnza wewe sio muoaji kwasababu. Tayali Ushaweka Ukalibu wakukaa Nyumba moja Nae au kulala kitanda nimoja Nae bila Ya ndoa ivo Ingekuwa muoaji kabisa Yani Tayali Ushapeleka Ulichokuwanacho kwenye iyo Mahali Ata iwe 500000 matumaini Hapo sasa Mpka Family Yake ishajua kwamba Yupo kwako kwakupika na kupakua Mpka kufikia malengo Ya ndoa Miaka Tayali ishapita pia Nijambo Mbaya kumficha Baba Ake Kwan Wenda kupungukiwa na Kipato chako na kujua kwamba kweli mwanawe Unamuitaji Bs Inshlla mwenyezimungu Angefanya wepes wake Kwa mwanawe ila Bado Unaendelea kuzini2 na kujua kila idala Yake Yeye me Naishia Hapo Kwanza
 
Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
28,259
2,000
Kuna kijana alidhani kumtia mimba binti ndio atapewa mke kirahisi rahisi.
Wazazi wakakomaa.
Mtoto akazaliwa, mwanaume anadhani atapewa mwanamke lakini wapi.
Kosa alilolifanya alipigwa marufuku kutia mguu nyumbani kwa mwanamke. Mtoto akafikisha miaka miwili mwanaume haamini macho yake.
Ilibidi akaombe, alipe mahari na faini(hela ya matunzo ya mtoto yangu alipozaliwa) wakafunga na ndoa wakakabidhiwa mtoto sasa.

Kuna wazazi hawachezewi nyie, labda ujiandae kukaa mbali na mtoto wako hadi siku akutafute mwenyewe.
Bila Shaka Mleta Mada Kapata Jambo Jema
Fuata Ushauri Mzuri Huu
 
Hendisamu

JF-Expert Member
May 9, 2019
319
500
Iko hivi cha kufany kwa sasa nikumuweka binti wazi kuhusu kipato chako na kisha aweze kuwaeleza wazazi wake juu ya hilo angalau wapunguze mahari maana hiyo ni pesa nyingi sana.

Pia kumbuka utaishi na uhalisia wa mtu si muonekano wake usije ukatoa mahari kubwa kwa kujua yuapendwa sana kumbe mwenzako ana lake moyoni baadae ukajajutia juu ya maamuzi yako na kuanza kuumia kwa pesa uliyopoteza kwenye mahari. Hivyo fanya maamuzi sahihi kwanza kwa upande wa wazazi wa binti.

Kumpa mimba sio suluhisho la kupunguziwa mahari au kupewa mke bure mkuu.... just think deeply.
Anafahamu kila kitu Mkuu!
 
Hendisamu

JF-Expert Member
May 9, 2019
319
500
Chakwnza wewe sio muoaji kwasababu. Tayali Ushaweka Ukalibu wakukaa Nyumba moja Nae au kulala kitanda nimoja Nae bila Ya ndoa ivo Ingekuwa muoaji kabisa Yani Tayali Ushapeleka Ulichokuwanacho kwenye iyo Mahali Ata iwe 500000 matumaini Hapo sasa Mpka Family Yake ishajua kwamba Yupo kwako kwakupika na kupakua Mpka kufikia malengo Ya ndoa Miaka Tayali ishapita pia Nijambo Mbaya kumficha Baba Ake Kwan Wenda kupungukiwa na Kipato chako na kujua kwamba kweli mwanawe Unamuitaji Bs Inshlla mwenyezimungu Angefanya wepes wake Kwa mwanawe ila Bado Unaendelea kuzini2 na kujua kila idala Yake Yeye me Naishia Hapo Kwanza
Ahsante kwa ujumbe Mkuu, yeye ndiye alianza na kutaka tukae nadhani alihisi nitamuacha sababu hata yeye hakuridhika na mahali hiyo na kutokana na familia yao hana haki hata ya kuchangia wazo kuhusu mahali kutokana na maelezo yake!
 
G.Jacob

JF-Expert Member
Aug 12, 2013
3,569
2,000
Huyo mwanaume nae boya uniendeshe hivo, nachukua mwingine nakuachia wenu na nina uhakika baada ya mda nitaendelea kumla tena Kama nyumba ndogo.
Wewe sio muoaji ama la basi umri wako bado sana....hakuna kitu kigumu cha kunyima raha kama kuishi mbali na mtoto wako wa kumzaa mwenyewe.
Usione watu wanaburuzana hadi mahakamani huko ama vikao vya familia kung'ang'ania watoto wao, ukiwa mbali na mtoto wako amani na furaha inatoweka kabisa.
 
Requal

JF-Expert Member
Jun 5, 2020
901
1,000
Wewe sio muoaji ama la basi umri wako bado sana....hakuna kitu kigumu cha kunyima raha kama kuishi mbali na mtoto wako wa kumzaa mwenyewe.
Usione watu wanaburuzana hadi mahakamani huko ama vikao vya familia kung'ang'ania watoto wao, ukiwa mbali na mtoto wako amani na furaha inatoweka kabisa.
Nyie Wajinga ndio mnaooa kwa kupelekeshwa pelekeshwa...ukiona wewe ni dhaifu usidhani ni wote ...huwa wanaangalia na watu, Mimi huniletei huo UPUMBAVU eti wa faini kwani tulibakana? Au nawezaje kulipa faini ya mwanangu niliyemzaaa?

Wewe endelea na udhaifu ukidhani kila aliye na mawazo tofauti na wewe ana umri mdogo...
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
5,820
2,000
Kuna kijana alidhani kumtia mimba binti ndio atapewa mke kirahisi rahisi.
Wazazi wakakomaa.
Mtoto akazaliwa, mwanaume anadhani atapewa mwanamke lakini wapi.
Kosa alilolifanya alipigwa marufuku kutia mguu nyumbani kwa mwanamke. Mtoto akafikisha miaka miwili mwanaume haamini macho yake.
Ilibidi akaombe, alipe mahari na faini(hela ya matunzo ya mtoto yangu alipozaliwa) wakafunga na ndoa wakakabidhiwa mtoto sasa.

Kuna wazazi hawachezewi nyie, labda ujiandae kukaa mbali na mtoto wako hadi siku akutafute mwenyewe.
Wazazi wa kichaga ndio wana hiyo tabia
 
Chindy

JF-Expert Member
Apr 5, 2020
351
1,000
Nyie Wajinga ndio mnaooa kwa kupelekeshwa pelekeshwa...ukiona wewe ni dhaifu usidhani ni wote ...huwa wanaangalia na watu, Mimi huniletei huo UPUMBAVU eti wa faini kwani tulibakana? Au nawezaje kulipa faini ya mwanangu niliyemzaaa?

Wewe endelea na udhaifu ukidhani kila aliye na mawazo tofauti na wewe ana umri mdogo...
Sio udhaifu au UPUMBAVU kama unavyosema , ni utaratibu tu au ni kufuata mila na desturi za jamii zetu.

Kuna mijitu imezoea kubisha hata akiambiwa atende vitendo vya kiungwana ambavyo wala havina madhara ni kubisha tu 😂😂😂😏
 
Saint Anne

JF-Expert Member
Aug 19, 2018
33,800
2,000
Toa robo sio nusu mwambie nyengine utamaliza ndo imetoka hio

Au mimba tu kama jamaa hapo juu alivyosema

Ukizishindwa hzo njia last option mwambie binti aongee na kwao we huna uwezo wapunguze Si anataka aolewe ataongea nao tu maana sio wazazi wanao olewa

Ikishindikana piga chini tafuta mwengine acha tabia ya sogeza tuishi huwez kaa na mtoto wa mtu bila ridhaa ya wazazi wake mikosi mingine ni ya kujitakia

Ngoja nikanywe bia we endelea kusubir michango mingine
Unaenda wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usher-smith MD

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
8,620
2,000
Mahari ni kitega uchumi cha familia sikuhizi

Wanawake wanalalamika wanaume wa kuoa wapo wachache ila akitokea jamaa akatangaza ndoa, anapigwa milioni 5,.
Hizi mahari zifutwe tu, hazina maana tena, kama ni shukrani kwa kumtunza binti yao, wengi wamefeli kutunza mabinti zao.
Wakati mwingine unakuta wewe muoaji umetunzwa kuliko huyo binti.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom