Vijana tuna la kujifunza kutoka kwa Lissu

Ha ha na imagine how utopolo you are. Uko na role model wa kipuuzi kabisa. Hapo kwa Mbowe na Lissu unapata modalities gani? Za kupiga ruzuku? Kula vitu maalum? Michango saccos? Pole Sana.
Nadhani hujasoma post. Ndio maana pale juu alianza kwanza kwa kusisitiza siasa iwekwe pembeni.
Mbowe hausiki kwenye post hii.

Tunaongelea mtu kama mtu mwenyewe. Kazi na madudu yake weka pembeni.

Naona ww umejibu siasa.
 
Jidanganye umuige utakufa siku sio zako yule ni watu dizaini ya tupac huwa hawazeeki wanauawa au wanafia jela.
Hahaha nigga pls. Where i am now nahitahi vitu vitu kidogo sana. Na ww sio Mungu unitishie kifo.
 
Kwahiyo chama chenu kupitia mzeee wenu wa kiiki za maigizo na kutetea ushoga, kumbe mumeshainama mda mrefu ndiomaana beberu kwenu ni nguzo muhimi? Sasa tutawagalagaza nyinyi na beberu wenu.
Ni waoi na lini alitetea ushoga? Na uweke ushahidi hapa
 
Ujasiri wa Lissu sasa unatokana na aliyopitia, ukiachilia mbali uwezo wake mkubwa wa akili, zile risasi kumi na sita zilizomuingia mwilini mwake zimemfanya awe na ujasiri wa hali ya juu.
Ujasiri ndio sifa kuu kabisa ya TL na inaoekana kazaliwa akwiwa nao na haya aliyo yapitia ndio yana mkomaza zaidi. May our Lord bless him further.......
 
TUNDU LISSU NI SOMO KWA VIJANA TUNAOJIFUNZA SIASA

Vijana wenzangu mnaodhani kuwa siasa ni nyepesi leo naomba tuweke itikadi zetu pembeni tujamjadili Lissu kwa angle nyingine. Kama wewe ni mfia chama huwezi nielewa hapa, bora uka-scroll down tu.

Huyu mtu anaweza kutumika kama kielelezo cha kujifunzia hususani kwa vijana ambao wana ndoto za kujijenga kisiasa bila kujali chama gani unatokea.

Nini nataka.kusema?, Kama huwa unadhani siasa ni mseleleko kwamba ukishakuwa upande mmoja tu kazi imeisha basi tega makini tujifunze kwa Lissu.

Kivipi?, twende kazi;

1. Lissu ametoka kwenye matibabu yaliyogharimu kukaa nje ya nchi na familia yake takribani miaka 3 na amefikia kwenye kampeni moja kwa moja. Hapa hata watoto na ndugu zake hawakupata muda wa kukaa na mtu wao wampe hata pole.
KUJITOA MUHANGA

2. Tundu Lissu akiwa matibabuni UbelIgiji aliporwa ubunge wake na stahiki zake zote za malipo kwa sababu kuwa Spika wa bunge hajui sehemu alipo. Na alipokwenda kulalamika kwenye vyombo vya sheria, mahakama ilitupilia mbali shauri lake kwa kuona halina mashiko lakini hakuonekana kujali.
UVUMILIVU

3. Tundu Lissu anafanya kampeni kwa bajeti ndogo sana kulinganisha na mpinzani wake mkuu, Rais Magufuli. kuna wakati mwingine watu humchangia kwenye mikutano yake ili kuwezesha utendaji wa kazi yake.
MALENGO

4. Tundu Lissu ndiye mgombea wa kwanza kutoka chama kikuu cha upinzani asiyetangazwa sana iwe kwa Redio, TV wala mabango ya wazi lakini mikutano yake inajaa watu kuliko kawaida.

Alichokifanya ni kutumia fursa ya teknolojia ya habari hasa mitandao ya kijamii kujitangaza wakati mpinzani wake Magufuli mabango ya picha zake yamejaa nchi nzima huku magazeti, TV na Redio zikirusha ziara zake kila siku. Hapa tunaona kwamba tunakoelekea hizi picha na mabango mengine yatapoteza umuhimu kwenye kampeni.
UBUNIFU

5. Tundu Lissu anaonekana kulimudu vyema jukwaa la kampeni kwa kujenga hoja nzito kuhusu maisha ya watu hasa katika kufafanua mambo anwai ya kila eneo analokanyaga kiasi kwamba anafanya usahau kuwa mtu huyu hajawahi kuwa hata Naibu waziri. Je akiwa Rais itakuwaje?
UWEZO

6. Tundu Lissu anafanya kampeni huku akiwa na kipande cha risasi, Operations 21 na vyuma mwilini tena wakati mwingine anacheza na muziki bila kujali nini kinaweza kuikumba afya yake. Mjuba anasonga mbele tu.
MAONO

7. Tundu Lissu amezushiwa kila aina ya propaganda ikiwemo ya kibaraka wa mabeberu na matusu mengi toka kwa wapinzani wake lakini yeye hujibu kwa hoja nzito bila matusi na kuwapoteza kabisa.
UKOMAVU

8. Tundu Lissu tangu mwaka 2001 amekuwa akibambikiwa kesi za makosa ya uchochezi ili kummaliza kisiasa lakini hajawahi kukutwa na hatia.

9. NEC, CCM, POLISI nadhani wamepata somo wakati mwingine wasifanye makosa ya wazi wazi Teknologia inaenda kwa kasi sana

C&P
Cha kujifunza ni keki ya taifa iliwe na wote na si baadhi.

Haya yote yangetokea kama kaka mkubwa angekuwepo kwenye payroll ya mzee baba?


Sent from my POT-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Pamoja na hayo yote, Lissu ni JASIRI. Kuna watu wenye maarifa na uwezo mkubwa hata kumzidi Lissu lakini ni waoga.
Vijana wajipatie maarifa sahihi na wawe majasiri kutetea kile wanachoamini.
Itachukua muda kujijengea ujasiri wakutosha kwani wazee wengi na watoto wao bado wanaugua ugonjwa wa "u-kondoo wa nyerere" yaani kutokuhoji kulikopitiliza kukiambatana na woga wa aliyeshika madaraka na wapambe wake. Mfano mmoja mzuri ni haya yanayoendelea kwenye vyombo vya habari sasa hivi.
 
Hawa ndio vijana ambao Nyerere aliwahitaji "tunataka kuwaona vijana jeuri,vijana wanahoji bila woga,vijana wenye misimamo"
Afadhali hili umeliibua nilikua nalitafuta. Nyerere alikuwa fundi wa kusema kitu kimoja na kutenda kitu kingine. Ukisoma hiyo nukuu yake mtu unapata msisimko lakini ukweli Nyerere ndiye alitufanya kwa ujumla (Baba zetu, sisi wenyewe na sasa watoto wetu) tuugue huu ugonjwa niuitao "u-kondoo wa Nyerere". Tuwaoga kupitiliza na tuna ambukizana uwoga huo. Wakati wake JKN nani alisema kwa sauti kile ambacho ni tofauti na mwalimu? Maamuzi yote tulimwachia yeye. Akaua vyama vya upinzani akabakiza chake tukawa Chama kimoja na Chama dola. Kana kwamba havitoshi akatuachia hili likatiba. Akawa na sheria ya kuweka watu ndani hadi pale atakapo "kukumbuka". Hili gonjwa hili ndio Lissu na wenzake wachache wanalopambana nalo. Wengi wetu tumelala usingizi fofo ndio kwanza tunawakebehi wakina TL. Naomba tu wengi wa watoto wetu na wajukuu zetu waponyeshwe ugonjwa huu na wakina TL ndio tutaelewa kinachoendelea na kuchukua hatua.
 
Afadhali hili umeliibua nilikua nalitafuta. Nyerere alikuwa fundi wa kusema kitu kimoja na kutenda kitu kingine. Ukisoma hiyo nukuu yake mtu unapata msisimko lakini ukweli Nyerere ndiye alitufanya kwa ujumla (Baba zetu, sisi wenyewe na sasa watoto wetu) tuugue huu ugonjwa niuitao "u-kondoo wa Nyerere". Tuwaoga kupitiliza na tuna ambukizana uwoga huo. Wakati wake JKN nani alisema kwa sauti kile ambacho ni tofauti na mwalimu? Maamuzi yote tulimwachia yeye. Akaua vyama vya upinzani akabakiza chake tukawa Chama kimoja na Chama dola. Kana kwamba havitoshi akatuachia hili likatiba. Akawa na sheria ya kuweka watu ndani hadi pale atakapo "kukumbuka". Hili gonjwa hili ndio Lissu na wenzake wachache wanalopambana nalo. Wengi wetu tumelala usingizi fofo ndio kwanza tunawakebehi wakina TL. Naomba tu wengi wa watoto wetu na wajukuu zetu waponyeshwe ugonjwa huu na wakina TL ndio tutaelewa kinachoendelea na kuchukua hatua.
Tunaenda kubadilika taratibu mkuu
 
Ni kweli ndio mana mkuu alisema na kushauri apumzike tu

baada ya kuapishwa angemtafutia ka kazi ka hapa na pale

sidhani kama kuna mtu yuko tayari ajiri kilaza kwa maana

hiyo uliyoyaongea yana chembe za ukweli,muhimu akubali

kujishusha ili aweze kula chakula na watu wazima,kiburi mwisho 28th oct.
 
Vijana tunataka amaniii, vijana hatutaki kuchochewa wala kuvurungwa na mabeberu. Vijana wakitanzania tuko kwa masilahi ya taifaa ili tunufaike na maendeleo
Hahahaha Lisu si kijana ma si wa kizazi hiki ambacho kinarubuniwa jitahidi,kisichokuwa jasiri,chenye harufu kubwa ya rushwa.vizazi Kama vya TL kwa Sasa Ni wachache Sana.Majasiri Kama Lisu walikuwapo enzi hizo wakati jkt ilikuwa mwaka mzima na huko ndo tulikopata ujasiri.

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom