Vijana tuliobaki benchi tujifunze kwa wanaotumbuliwa

Nyakarungu

JF-Expert Member
May 1, 2011
472
375
Wanabodi,
Hakuna mwanadamu aliyekamilika kabisa hapa duniani.
Hivyo nawaomba vijana wenzangu tujifunze kujikubali kwa kujikosoa na kukubali kwamba hata sisi tuliwahi kufanya makosa au madudu ambayo yalisitahili adhabu kabisa, lakini kwa sababu ya Kona tuliyofanyia madudu yetu hayo haikuwa na nguvu ya kujadiliwa na jamii kwa sababu ya udogo wa vyeo au umaarufu wetu, ndio maana Hadi Leo imebaki Siri baina yetu na wachache wanaoyafahamu.
Lakini Cha kusikitisha Ni kwamba sisi haohao ambao hatujapata kukalia viti vya uteuzi wa Rais tuko mbio na wepesi wa kushangilia maanguko ya wenzetu wanaotumbuliwa bila kujifunza na kutubu kwa mungu na kubadilika.
Nawaomba Sana tukumbuke kwamba, hakuna mwanadamu alokamilika hapa duniani kabisa, wote tuko sawa, Ila tofauti inaanzia kwenye kukubali kwamba na sisi tuliwahi kukosea ili tujifunze kubadilika.
Nachokiona ni shangwe na nderemo tele watu wanaotumbuliwa bila kujifunza.
Hulka hii haitujengi Wala haituinui kamwe, tujifunze kwao ili tujikosoe na tujenge jamii Bora.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom