Vijana tuingie kwenye ufugaji wa kuku, kuna dhahabu isiyoonekana

Tanzania ni nchi yenye walaji wa nyama wengi na kuku huliwa kwa kiasi kikubwa sana. Hata kama bei zinapanda, ulaji unaendelea kukua kila siku.Matokeo yake ni kwamba kufuga kuku inaweza ikawa biashara yenye faida kubwa kwako kwa kuwa yanahitajika kwa wingi. Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka wimbi la viojana wengi kukimbilia katika tasnia hii ya ufugaji wa kuku kwa kuwa kumekuwa na mwamko wa ujasiriamali na pengine inachangiwa na kukosekana kwa nafasi za kutosha za ajira. Nimefanya tahmini ya muda mrefu kabla sijaingia katika ufugaji wa kuku na hata nilipoingia nilikuwa nafanya ufugaji kwa uoga sana kwa sababu ya kukosa maarifa.

Lakini baada ya ajira ya ofisni kuwa ngumu nilikaa chini na kujiuliza mambo yafuatayo;
(a) Mbona ambao hawajasoma wanafanya kazi zao na wanajiinguizia kipato?
(b) Mimi nilienda shuleni ili nifanye tu kazi za kalamu?
(c) Mbona wazazi wangu hawakusoma lakini walitulea,tukasoma na mavazi na tuliisha kwenye nyumba hata kama sio za kisasa?
(d) Mbona kuna watu duniani wanaishi kwa kilimo na ufugaji na wanakuwa matajiri?
(e) Kwanini duniani hakuna Maprofesa ambao wanaongoza kwa utajiri uliotokana na elimu zao ama kazi zao?
(f) Ni lazima ujasiriamali ufundishwe vyuoni? mbona nikiwa mdogo nilikuwa nalima mbogamboga na kufuga kuku najinunulia daftari?
(g) Ni jukumu la serikali kunitafutia ajira?Mbona kule kijijini kwetu watu hawajaajiriwa na wanaishi?
(h) Ni kweli mambo ya ufugaji na kilimo ni maalumu kwa wasioenda shule?

Baada ya kujiuliza maswali hayo nilijikita katika kutafuta taarifa sahihi za ufugaji wa kuku hasa kupitia mitandao,nikaanza kufugia nyumbani,baadaye nikapata kodi nikahama nyumbani na kupanga.Lakini sikutosheka,palepale nilipopanga nikatebngenza banda la kisasa lisilo chafua nikafuga hapohapo.Baadaye mtaji ukawa mkubwa nikajenga banda kubwa kijijini nikaanza kufuga na wakati huo nafanya kazi ya kuajiriwa. Leo hii nafuga kijijini na mjini na bado nimeajiriwa pamoja na kuwaajiri wasaidizi wangu kwenye mradi ambao bado unafanya vizuri tu.Hivyo siandiki hapa ili kukushawishi lakini nataka nikuonyeshe ni kwanini ni muhimu uingie kwenye ufugaji wa kuku kama fursa inayoweza kukupatia ajira ya kudumu.

Kwanini uingie katika ufugaji wa kuku?

Ni mrdi unaoanza na mtaji mdogo.
Hii ni moja kati ya faida za kuanzisha mradi wa kuku. Kwa kawaida mtu yeyote anaweza kuanzisha mradi huu wa kuku kwa sababu hauhitaji mtaji mkubwa ili kuanza. Mfano kuku mmoja ambaye ni mtetea ma jogoo mmoja unaweza kuanza kama mradi. Mchanganuo ufuatao unaonyesha ni kwa jinsi gani. Mtetea mmoja na jogoo unaweza kununua kwa elfu 25 kwa maana jogoo elfu 15 na mtetea 10, baada ya mwezi mtetea atakuwa ameanza kutaga.Kipindi amemaliza kutaga ukamuwekea mayai 10 na 15 ndani ya siku 21 atatotoa vyote au 10. Vifaranga 10 ukawalea mpaka miezi 6 watakuwa kuku wakubwa na baadaya hapo wataanza kutaga na kulalia na kupata vifaranga wengi na ukaendelea kupata kuju wengi zaidI. Ndio maana unaweza kutumia mtaji mdogo na baada ya kuwa na kuku wengi na kuanza kuuza. Kanuni hii niliitumia wakati nimemaliza chou kikuu na kuanza kuzunguka nikitafuta ajira bila mafanikio,baada ya muda nikawa na mradi mjini na kijijini kama nilivyoeleza hapo juu.

Ufugaji ni chanzo kizri cha mapato halalio. Kuku ana bidhaa muhimu kama vile mayai, mbolea, nyama n.k. Vyote hivi ni mahitaji ya binadamu katika maisha ya kila siku. kupitia kufuga Kuku utapata fursa ya kutengeneza fedha nyingi tu. Kama utakuwa mfuatiliaji makini, kwa maana kuwapa chanjo kwa wakati, chakula bora na kutibu magonjwa pindi yakitokea. Kuku wa kienyeji ama chotara aliyekoma anauzwa 15000, 20000, 25000, 30000 na kuendelea inategemeana na kuku mwenyewe. Tatizo kubwa tulilonalo Watanzania hasa kwa kuku wa kienyeji kadhalaulika na kuonekana ni wa kawaida lakini tukikaa kujua trei moja mayai ya kienyeji linauzwa 15000. Je? Ukiwa unaweza kuzalisha trai 5 kwa siku utakuwa na shilingi ngapi. Binafsi nimefuga kuku kwa muda sasa na naadnika jambo ambalo nina uhakika nalo.Ndio maana nakueleza ukitaka kupata usaidizi wa karibu namna ya kuanzisha mradi wako hadi ufikie hatua ya mafanikio unaweza kututafuta au ukanunua kitabu chetu kinachotoa mwongozo wa kitaalamu.Tupigie/andika sms/Whatsap kwenda namba 0767141643.

Udhibiti wa mradi wa kuku ni rahisi. Urahisi huu hauna maana kuwa hakuna ugumu hapana ila maana kubwa ni kwamba hata kama ni mfanyakazi wa kuajrliwa utapata muda wa kufuatilia kwa karibu maendeleo ya kuku wako. Mfano umeanza na mradi wako wa kuku 100, umewafugia nyumbani kwa kawaida unatakiwa kujipangia ratiba. Kwamba kabla ya kwenda kazini fika bandani na kuwahudumia kuku wako, hata kama utamwachia kijana aendelee kuwa hudumia kipindi ukiwa kazini, utakuwa unajua kuku wako wako salama. Pia jioni ukitoka kazini inabidi upate muda wa kipitia bandani na kuona hali ilivyo na kupata mrejesho kutoka kwa kijana uliyemwachia.Wakati Fulani nikiwa mfugaji wa kuku wa kienyeji nilikuwa naamka mapema alfajiri nasafisha vyombo vya kuwawekea chakula na maji,nawawekea chakula katika vyombo vyao halafu nazima taa naenda kazini.Kukikuchwa wanakula chakula na maji,nikirudi usiku naokota mayai na kuandaa utaratibu wa chakula chao cha kuku.Ila kwa kuku wa kisasa ama chotara lazima uandae utaratibu wa mtu kuwepo sababu wanahitaji uangalizi wa mara kwa mara.

Soko la kuku na bidhaa zake ni kubwa. Hili swala ni fursa kubwa kwetu sisi vijana hasa ambao tumekuwa tukilalamikia kukosekana kwa ajira za serikali na mashirika binafsi. Lakini tazama watu wa nje ya nchi na baadhi ya wenyeji wanaoingiza bidhaa za kuku kama, vifaranga, kuku na mayai. Wakati nafasi ya kuzalisha hapa hapa tunayo ni swala la maamuzi na kuacha kulalamikia serikali juu ya ajira. Vijana ajira tunayo mikononi mwetu ni swala la kuchukua hatua. Uwezekano upo kwa Tanzania kuanza kujihidumia yenyewe na kuanza kutoka nje ya mipaka pia. Takwimu zinaonyesha bado wafugaji waliopo nchini hawajaweza kufikia hata nusu ya mahitaji ya bidhaa za kuku nchini Tanzania. Jambo la msingi ni sisi kutafuta taarifa sahihi ili kuweza kufanya maamuzi sahihi. mojawapo ya chanzo kizuri cha taarifa za kilimo na ufugaji ni wizara ya mifugo,mitandao ya kijamii na semina na makongamano yanayohusiana na ufugaji.

Mradi wa kuku ni benki hai. Benki hai ni namna ya kuhifadhi pesa yako kwa matumizi ya baadae. Sasa ufugaji wa kuku ni benki hai maana yake ukiwekeza pesa yako katika kuku itakuwa sehemu salama na itaongezeka kwa kadri unavyozidi kuzalisha kuku wengi. Benki hii ni tofauti na benki za kawaida kwa sababu hakuna gharama yoyote ya makato ya uendeshaji, hapa ni kuhakikisha pesa yako inakuwa ni jitihada zako kuhakikisha unazalisha kuku wengi.

Sasa basi,yapo mambo ya muhimu ambayo wewe ukiwa kama mfugaji wa kuku au mfugaji mtarajiwa unapaswa kuyazingatia ili uweze kupiga hatua na kufikia hatua ya kilele cha mafanikio kupitia sekta ya ufugaji wa kuku. Ufugaji wa kuku kama shughuli nyingine yoyote inapofanywa kwa kuzingatia mambo haya ni wazi kuwa safari yako kuelekea kule unapoata itakuwa ni ya rahisi sana. Wafugaji tuliowengi tumekuwa tunafugafuga tuu bila hata kujua nini tunachohitaji ili kuweza kupiga hatua za kutosha na hatimaye kuufanya ufugaji kuwa sehemu ya kiungo muhimu cha kipato na ajira kuanzia kwetu na kwa familia zetu. Hivyo basi ni vyemea kila mfugaji akazingatia mambo haya;-

1) Tathmini kwa kina na chagua kwa umakini fursa mojawapo zilizopo ndani ya sekta ya ufugaji wa kuku na uanze nayo.

Sekta ya ufugaji hasa wa kuku ni sekta kubwa kidogo ndani yake ina fursa nyingine nyingi ambazo ukiwa kama mfugaji unaweza anza nazo na kukupa uelekeo ambao unaweza ukawa ndiyo njia sahihi kwako ya kuelekea kwenye ufugaji wa ngazi ya juuu zaidi.Si lazima ili uwe mfugaji mkubwa basi uanze moja kwa moja na kufuga kuku peke, ndani ya sekta ya mifugo zipo fursa nyingi kama uuzaji wa vifaranga,uuzaji wa chakula cha kuku,uuzaji wa madawa,uuzaji wa bidhaa za wafugaji kama kuku,mayai n.k. Hivyo kabla ya kuanza rasmi ufugaji wa kuku ni vyema kama mfugaji akajitathmini ni eneo gani anaweza akaanza nalo yapo maeneo amabayo yana wafugaji wengi hivyo kwenye maeneo haya unaweza ukaanza ana uuzaji wa mahitaji yao mbali mbali kabla ya kuamua rasmi kujikita moja kwa moja kwenye ufugaji.Mambo haya pia yatakuimarisha vyema na kuifahamu fika sekta ya ufugaji wa kuku.

2) Wekeza katika elimu kama sehemu kuu na muhimu kwenye mtaji wako.

Linapokuja suala la ufugaji ni wazi kuwa elimu juu ya utendanji wa mambo mbali mbali inahitajika ili kuweza kukuwezesha kupiga hatua stahili kwa muda stahili. Tumekuwa na kasumba ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kwenye kuwekeza kwenye mambo mengine kama ujenzi wa mabanda na utafutaji wa mbegu badala ya kutumia walau kiasi kidogo cha fedha kuwekeza katika elimu itakayokusaidi kuweza kufikia matokeo stahili kwa wakati. Elimu ya kutosha inahitajika kuanzia kwenye ufugaji wa kuku wenyewe hadi kwenye mbinu za utafutaji wa masoko ya bidhaa zako, si ajabu kumkuta mfugaji kafuga kuku wengi bila kutathmini vyema hali ya masoko na upatikanaji wake.Mwisho wa siku anawekeza mamilioni ya fedha akianza uvuna mayai au kuku hana pa kuuza.Ni vyema sana kuwekeza katika elimu namaarifa sahihi ya ufugaji kabla hujaanza kufuga kuku.

3) Anza na ulichonacho lakini fikiri na tenda kama mshindi.

Safari ya kilele cha juu ya mafanikio ya jambo lolote haitegemei na wapi ulipoanzia bali itaratibiwa na namna ambavyo utaziepuka na kukabiliana na changamoto utakazokutana nazo njiani. Ufugaji kama lilivyo kama jambo lolote ni wazi pia unakabiliwa na changamoto mbali mbali hivyo kabla ya mfugaji kuanza kufuga ni lazima awe tayari kukabiliana na changamoto hizo bila kukata tamaa ili kimuwezesha kupiga hatua stahili na kwa wakati. Mfugaji mwenye mafanikio ni wazi anapaswa kuwa mtu atakayepambana na changamoto zote atakazokutana nazo njiani bila ya kuchoka.Jiandae kukutana na changamoto kama za magonjwa,vifo,kuishiwa fedha za kulisha kuku n.k.Ukiyashinda haya ndipo utakapoona mafanikio katika mradi wako wa ufugaji.

4) Dhamiria kujifunza bila ya ukomo.

Mfugaji aliye na mafanikio lukuki ni wazi atakuwa yule ambaye kujifunza kwake litakuwa ni jambo la kufa au kupona ni lazima tujifunze mambo yote yahusuyo sekta ya ufugaji wa kuku kwa kina zaidi ili kutatua kwa usahihi kabisa baadhi ya changamoto za kiutendaji na za kimafanikio. Ufugaji kama zilivyo sekta nyingine ni sekta ambayo inakuwa kwa kasi sana hivyo basi ni wazi mfugaji anapaswa kujifunza bila ya ukomo hadi atakapofikia kilele cha juu kabisa cha mafanikio na jambo hili haliwezi kufikiwa bila kuruhusu kujifunza kwa usahihi kwenye kila hatua. Si kila aliyefanya jambo hili kwa muda mrefu basi ni lazima ndiyo aweze kukupa njia sahihi ya kufanikiwa kwenye jambo hili lazima utathmini njia alizotumia yeye kuweza kumfkikisha alipo unajua kwenye kujifunza kila mtu anaweza akawa mwalimu ila kuwa mwalimu mzuri ni sifa nyingine ya ziada.

5) Usiache kabla ya kumaliza.

Jambo lolote litendwalo na binadamu huwa halikosi changamoto zake, hivyo basi ukiwa kama mfugaji mpya utakabiliana na changamoto mbali mbali ambazo zitatokana na kukosa elimu au uzefu wa kutosha hivyo katu usiruhusu changamoto hizo zikurudishe nyuma na kuona kama haupo kwenye njia iliyosahihi.Utatuzi wa changamoto mbalimbali utakazokutana nazo njiani ni wazi kuwa utakuongezea hali ya kujiamini uwapo safarini hivyo changamoto hizi ni sehemu muhimu ya kutuimarisha kibiashara,kitendaji na kifanisi zaidi.

6) Usitegemee kufanya jambo hili kama ziada na ukapate matokeo sawa na shughuli kuu.

Ni uwazi usiopingika kuwa kwenye mafanikio ya jambo lolote muda ndiyo jambo la msingi la kiuwekezaji kwenye kupima mafanikio ya jambo hilo. Hivyo basi kama tunategemea ufugaji kuja kuwa shughuli yetu kuu itakayoweza kuwa chanzo cha ajira kwetu na kwa familia zetu ni wazi kuwa muda wa kutosha unahitajika kwenye kuhakikisha kuwa matokeo yanayopatikana yalingane na muda uliowekezwa. Tukifanya jambo hili kama ziada na matokeo yatakuwa ya ziada hivyo hivyo.

7)Tafuta, tathmini na tumia kwa usahihi taarifa za kifugaji unazozipata toka kwenye vyanzo vilivyo sahihi.

Ni wazi pia kwenye kujifunza ni lazima utakutana na watu wasiowaaminifu watakaoweza kutumia udhaifu wako wa kutokujua jambo kwa kina kuweza kujiingizia kipato. Hivyo jaribu kulinganisha taarifa mbalimbali unazozipata na kuzitathmini kwa kina kabla ya kuchukua hatua yoyote maana uwezekano wa kupewa taarifa zisizo sahihi kutokana na kutokuwa na uzoefu ni mkubwa mno kutokana na kuwepo kwa baadhi ya watu wasio waaminifu. Uzoefu usiwe kigezo cha kukufanya ushindwe kutafakari na kufikiri mambo mbalimbali kwa kina na kwa usahihi na wala si kweli kila jambo utakaloambiwa na mtu kwa kigezo cha uzoefu ukaliona ni lipo sahihi wapo wazoefu wa kutenda makosa pia hivyo jiuepushe nao.

8) Jiepushe na wauwa ndoto.

Katika kuhakiisha kuwa ndoto ako inatimia bila kikomo ni wazi kuwa lazima kuwa makini na watu ambao wataweza kuyatia dosari mawazo yako hivyo basi unapaswa kuwa makini na watu hawa wasije wakakufanya ushindwe kuifikia safari ya kilele cha mafanikio. Katika safari yako hiyo tegemea kukutana na watu watakaokwambia kuwa haiwezekani, wapo watakaokwambia subiri hadi upate hela ndiyo ufanye,wapo watakaokushauri ili ukosee kwa makusudi huvyo ni vyema ukajitahidi kuzungukwa na kutafuata watu ambao mission zenu zitaendana na kuwa sehemu muhimu ya msaada kwenye safari yako.Kwa usahihi kabisa tafuta watu ambao watakwwambia twende pamoja pindi utakapohisi kukata tamaa.

9) Toa pato au sehemu ya biashara yako kama sadaka kwa wengine.

Kutoa ni nguzo kuu na ya muhimu ya muhimu ya kupokea ama kwa lugha nyingine tunaweza sema kuwa hakuna kupokea bila ya kutoa na hii ni universe law.Tukiwa kama wafugaji tunaowajibu usiopingika wa kuweza kutoa sehemu ya biashara yetu kama sadaka ili kesi za kuku kula mayai,na kuku kufakufa hovyo ziweze kupungua. Hakuna biashara inayoweza kufanikiwa bila ya kutoa sehemu ya pato kama sadaka. Kutowa kama sehemu ya kupokea kumekuwa ndiyo sehemu muhimu ya mafaniko tangu kuumbwa kwa binadamu hivyo katu hatuwezi epuka jambo hili.


Tunakutakia kila la heri katika kutafakari na kuchukua hatua.Ukihitaji kufundishwa ama kusimamiwa mradi wako wa ufugaji wa kuku unaweza kututafuta tukakusaidia,pengine ukihitaji pia kitabu chenye mafunzo ya ufugaji ussisite kututafuta kwa namba za simu +255767141643.View attachment 2052252
Hakuna Biashara inayo lipa ambayo mtu alishwa wahi washirikisha wenzake
 
Kwa uzoefu wangu ili ufanikiwe kwenye ufugaji hauhitaji mtaji mrefu sana, ila unahitaji ni uvumilivu tu. Unaweza kuanza na kuku 1 ila baada ya miaka 5 ukawa umetoboa mbaya sana
 
Acha wenye kejeli waendelee kukejeli,Tatizo la vijana watanzania wanaamini kubet wakiwa kwenye stuli ndefu.Hawataki kuchafuka.
Badala ya kumsikiliza mtu na kujifunza, wao ni kejeli mtindo moja, inaonyesha ukomo wao wa kujielewa!
  1. Kuna wengi wanalaani biashara ya daladala, lakini kuna watu biashara yao ya daladala inakuwa kwa kasi!
  2. Kuna watu wanafunga biashara ya shule sababu biashara mbaya, lakini wapo wanaofungua shule mpya kwa kasi sababu biashara inalipa!
  3. Kuna watu wanalaani bar ni biashara kichaaa kwani imewakata mtaji, lakini kina wengi bar zinawapa faida kubwa na kupelekea kufungua miradi mingine!
  4. Kuna watu wamefunga biashara za ufugaji kuku sababu hailipi kama ndugu wanaokejeli hapo juu, lakini kuna watu nawajua wamenunua viwanja kwa bei kubwa na kupanua uzalisha Sababu biashara ya kufuga kuku inawalipa!
Kwa hiyo issue siyo kulaani biashara fulani kwamba haifai sababu imekushinda, la, issue ni kujifunza kwa waliofanikiwa wamefanyaje.
 
U
Fuga kuku kwa PDF. wanakuwa tayari siku 3 tu maana ni shughuli kuu.

baada ya huo utani niseme wazi ufugaji sio jambo jepesi unahitaji kupata maarifa sahihi namna ya kuufanya. na ni vyema ukapata mafunzo kwa vitendo kabla ya kuingia.
Jakoseaaaaaa ..mie nafuga lakin sio kuku kuna wakat kilimo cha pdf nilkipnda mno ila nilfuga mnyama wa miez mi 2na wek 3 nikauza 60elfu kuna wakati niliuza mkubw wa miezi u kwa elfu 50 oyah ufugaji sio jambo jepes..
 
Nimekuwa mfugaji wa kuku kwa muda mrefu kidogo. Wacha nikupe nondo zangu
1. "Jua gharama kubwa iko wapi. "

Kuna tofauti kubwa sana kufuga kuku mjini na kufuga kuku kijijini. Mjini vyakula vya mifugo utanunua kwa bei kubwa. Kijijini utanunua kwa bei ndogo nafaka na utanunua vya kichanganyia kwa bei ndogo. Zaidi ya asilimia 70 ya gharama ziko kwenye chakula.

2. "Zalisha bidhaa soko linahitaji"

Kwamba hicho unachozalisha kiwe kinahitajika kwa wingi na kina soko la uhakika. Mfano mayai ya kisasa. Broiler, nk

3. Elewa msimu. Kila kitu kina msimu wake. Mfano soko la december la kuku tofauti na la Januari. Msimu wa mavuno bei za malighafi zinashuka tofauti na msimu mwingine. Hasa kwa wanaofuga kuku wa kienyeji ni muhimu sana kujua wakati gani soko linakuwa juu na wakati gani soko sio zuri.

4. Elewa namna ya kuzuia magonjwa.
(usalama wa kibayologia) biosecurity.

Matibabu kwenye mifugo ni gharama zaidi kuliko kinga. Sasa kwenye kinga inajumuisha mfumo mzima wa ufugaji kuanzia banda, namna ya uhudumiaji na mfumo unaotumia kufuga. Pia elewa hali ya hewa na magonjwa ambayo hali hiyo ya hewa inaambatana nayo.

5. Kama una malengo makubwa kabisa ili kupata faida kubwa anza na yafuatayo.
Moja, tafuta shamba kubwa.
Mbili, lima mazao ya nafaka kwa kiwango ambacho utahitaji kwenye mradi wako na ziada kidogo
Tatu, kuwa na ghala ya kuhifadhia chakula kwa kipindi hicho utakachofuga chakula kiwepo cha kutosha.
Nne, peke yako hutoboi. unahitaji wataalamu wawili. Mmoja wa kilimo akusaidie kwenye kilimo wa pili wa mifugo akusaidie kwenye mifugo.(kama humudu gharama hizo)

Hudhuria mafunzo na jenga urafiki wa karibu sana na wataalamu.
 
Haahaa mkuu, twende taratibu, binafsi unaleta kwenye platform? Mimi kuku nimefuga na ninafuga sana. Mimi ni miongoni mwa Tz wachache tuliokitana na Mkurugenzi wa KegFarms ambao ndo wazalishaji wa kuroiler India kwenye hotel ya coral reef.
So ni naongea kitu ninachokijua. Kwenye kuandika kila mtu anapata mafanikio. Kumeshakuja stori za green house, hydroponic, kware, sungura nk. Wengi waliowakimbilia ninyi wazee wa fursa waliishia kupoteza.
Kilimo, ufugaji vinalipa lkn siyo kama mnavoandika na kuielezea, waambieni watu ukweli siyo mnaeleza faida tu. Ufugaji una changamoto sana tofauti na unavoelezwa. Wewe unalenga kuuza vitabu vyako na si ufugaji. Ikiwa unavision yako leave your vision. Ukija hapa jukwaani tutakuchalenge tu. Unaongea miaka kumi kumaliza chuo mwezio nina miaka zaidi ya 17 ya ufugaji wa kuku, kuanzia broiler, layers, Malawi, sasso, kuroiler nk.
Nawapinga sana wale ambao Mnalenga kupata hela huku mkiacha watz wakiumia na hasara
Hapo kwenye Green house haaahaaaa umenikumbusha mbali
Ziliingia Kwa Kasi acha kabisa
Ila sijui zimepotelea wapi Saa HV

Maturubai yametoboka na jua,nguzo zimecharangwa kuni za kupikia supu
Fad fades
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom