Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,944
Habari wadau!
Nimetafakari kwa muda kidogo nimegundua njia rahisi ya kufanikiwa katika maisha hapa nchini, ambayo ni kujitosa kwenye siasa.
Hii ni kutokana na asili ya wananchi (waajiri wa wanasiasa ambao ni wananchi wa Tanzania) kuwa wafuata mkumbo, wasiojielewa na wepesi kusahau makonzi waliyopigwa siku za nyuma.
Hivi kitendo cha Watanzania kuishangilia na kuitumainia bajeti iliyosomwa majuzi ni dhahiri kwamba Watanzania wameshasahau kwamba bajeti ya 2016/17 imefail kwa asilimia nyingi, pia wameshindwa kubaini njia zilizoainishwa na waziri wa fedha majuzi kwamba zitatumika kukusanya mapato hazina utofauti na zilizotumika mwaka wa jana ambazo hazikuzaa matunda.
Ajabu zaidi ni kwamba mpaka wasomi nchi hii wageuka kuwa mzigo; haiingii akilini msomi kusifu hatua ya kuondoa ushuru wa kusafirisha mazao yasiyozidi tani moja kwenda halmashauri nyingine, kimsingi hakuna mkulima au mfanyabiashara atakayekubali kuingia hasara ya kukodi gari au kutumia gari yake kusafirisha mbali mzigo usiozidi tani moja(kg. 1000). Tani moja ni kama gunia kumi hivi, nani aunguze gharama za kusafirisha gunia 8 au 9 za mahindi kutoa Morogoro mpaka Dar ili kutafuta soko zuri Dar es salaam huku utofauti wa bei ni elfu 15 kwa kila gunia?
Yaani ngoja tu niishie hapa.