Vijana tufunge mikanda safari ya kudai Katiba Mpya imeanza

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
14,304
29,831
Nipo katika hatua ya mwisho sasa kufanya maamuzi magumu kama hamtaniunga mkono basi nitaandamana peke angu potelea pote.

Ninafadhaika sana kuona nchi yenye maliasili zakutosha lakini tangu uhuru hatuoni mabadiliko yoyote, mada ni zilezile, agenda ni zilezile mpaka tunasikia kichefuchefu yaani mpaka leo tunakimbizana na matundu ya Choo mashuleni, watanzania wanakufa kwa kukosa madawa hospitalini, tunaishi maisha yakutisha mpaka aliyeko kuzimu anatucheka. Nasema hapana liwalo naliwe.

Hapa naongea na vijana, ebu tuangalie yafuatayo halafu tutajiuliza hii serikali inatuchukuliaje
1. Wabunge 19 waliofukuzwa uanachama na kamati kuu ya chadema wapo pale kwa katiba ipi. Naapa kama hamna majibu yenye tija tutaonana wabaya, ivi hizi ni akili au matope. Kama katiba imeeleza kuwa kama mbunge atafukuzwa uanachama naubunge wake utakoma hapo hapo sasa Kuna katiba ipi nyingine ambayo imewaweka hawa watu?

2. Hizi tozo za miamala wananchi wamekataa hali zao ni duni ila nyinyi mnafosi. Wananchi ndowenye maamuzi ya mwisho kama wameona swala la tozo ni maumivu kwao kwann mnafosi? Vyanzo vyamapato vipo vingi nendeni huko acheni tamaa Wananchi sio kwamba wamesahau swala la tozo ipo siku kitalipuka nahuo moto hamtaweza kuuzima.

3. Nisheria ipi mnayotumia kuzuia vyama vya upinzani kufanya mikutano na kuruhusu CCM kufanya mikutano. Kama hamna majibu yakutosha jiandaeni vijana tumechoka kuburuzwa na wazee wenye tamaa zakubaki madarakani milele.

4. Nisheria gani mnayotumia kuzuia maandamano ya Amani yakudai katiba mpya. Katiba mpya nimatakwa ya Wananchi sio mbowe wala chadema nasiyo kila mnayemuona anaandamana basi ni mpinzani lahasha. Kudai katiba mpya ni uzalendo uliopitiliza vijana tuamke tudai haki yetu.

NB. Haki haiombwi haki inapiganiwa vijana tuamke sisi ndowahanga wakila matatizo yenye maumivu makali, ukosefu wa ajira ni sisi, umasikini ni sisi, imefika wakati mpaka tunafedheheshwa na spika wa bunge kuwa hatuna uaminifu nawakati kashifa zote zauwizi wa mabilioni ya escrow epa Richmond kigoda rada ni wao halafu cha ajabu tumekaa kimya. Tupaze sauti zetu tudai haki zetu wasipotupa haki zetu tutajichukulia wenyewe.


download.jpg


EnHQT8aUYAEzEM-.jpg
 
Watu wako tayari kinahitajika ni hata ka-ji-uongozi tu:

Katiba Mpya: Mapambano yako katika Hatua za Mwisho
"Watu" walio tayari ni WACHUMIA TUMBO WACHACHE wasiojielewa ambao kimsingi wanaongozwa na matumbo yao kwa matumaini yasiyokuwepo, kwani "watu" hao wanadhani "Katiba Mpya" ndio ufunguo wa wa kupata kile matumbo yao yanayowaambia. Sasa "uongozi" wa Gaidi Mwenyekigoda hamuutaki tena au naye habari yake kwisha!? Ila sasa mnataka "hata ka-ji-uongozi tu"! Mmekwisha na mmeishiwa maono. Nawashangaa kweli sana.
 
"Watu" walio tayari ni WACHUMIA TUMBO WACHACHE wasiojielewa ambao kimsingi wanaongozwa na matumbo yao kwa matumaini yasiyokuwepo, kwani "watu" hao wanadhani "Katiba Mpya" ndio ufunguo wa wa kupata kile matumbo yao yanayowaambia. Sasa "uongozi" wa Gaidi Mwenyekigoda hamuutaki tena au naye habari yake kwisha!? Ila sasa mnataka "hata ka-ji-uongozi tu"! Mmekwisha na mmeishiwa maono. Nawashangaa kweli sana.

You have the same things in common:

IMG_20211001_170537_564.jpg


Appropriate message to your boss Mr. Akili Kudanga:

IMG_20210930_170832_807.jpg
 
Back
Top Bottom