Vijana tufanye nini

Vijana ni wavivu kuchambua na kudaka fursa ukimpa fursa anadhani ni utapeli pasipo kuichambua, pia waondoe ile kasumba ya kufanikiwa tit potati on the spot, zaidi wakosentrate katika kufanya iyo fursa ilete manufaa
Nikweli mkuu hichi pia inabidi tukitekeleze Kwa ufanisi sio kusubiri zari la mentali
 
Tatizo la vijana wasomi ni kuingia katika mtego wa hadhi inayotokana na kiwango cha elimu waliyofikia, inapotokea ajira rasmi zinazoendana na hadhi yao ya kielimu hazipo au zinachukua muda mrefu kupatikana wanajikuta katika wakati mgumu, ingawaje wapo wachache ambao wanaukwepa huu mtego wa hadhi. Kingine ni vijana wengi kupenda kuiga maisha wasio na uwezo nayo, akipata pesa kidogo huyo kaenda kununua iphone ya 1.5m au kaenda club anaagiza heinkein na nyama choma. Kingine ni vijana wengi kutokuwa waaminifu, unaweza kuta kuna watu wana pesa zao lakini inawawia vigumu kuwekeza katika project ambazo watahitaji kuwa na vijana waaminifu wa kusimamia, kijana anakuwa na ndoto ya ku make ndani ya muda mfupi matokeo yake anaua mradi.
vijana wanavimba sawa Na wazee sehemu za starehe kweli hapa hua tunachemsha
 
Muachane na mawazo ya kujiona wasomi fanyeni kazi za kawaida na biashara zenye mtaji kidogo mfn.ballo la viatu linauzwa 12000 lenye PC 50 za viatu km sikosei kwa bei ya 10000 viatu 12 vimerudisha mtaji faida utajiongeza kwa vilivyo baki sehemu ya biashara mahali popote wanapita watu wengi unatandika chini ngoma inasonga.
 
Mkuu wazo zuri hili nashukuru sana pengine nisingelijua pasipo wewe Kwa bei hio hapo juu ninaweza nikapata kwasehem gani naomba msaada wako mkuu
 
Back
Top Bottom