Vijana tufahamishane fursa zinazopatikana Chato kwa sasa

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,305
Kwa sasa Chato inakuzwa na kukua kwa kasi ya ajabu, tunaona miradi mingi ya ujenzi inaanzishwa huko na kuota kama uyoga.

Kama vijana ni hili tuliangalie kwa jicho la fursa badala ya kukaa na kumlaumu Rais na juhudi zake za kuigeuza Chato kama New York.

Miradi mikubwa iliyoko huko kwa Sasa:
1:
Uwanja wa Ndege haujaisha bado unaoendele kujengwa.

2: Hospital kubwa ya Kanda yenye uwezo wa kuhudumia raia zaidi ya milioni 18, kwa maana hii itakuwa Muhimbili ya pili.

3: Kwa ukubwa wa hii Hospitali muda wowote mtasikia ujenzi wa chuo cha Sayansi ya Afya wanafunzi watamwagwa wa kutosha huko.

4: Uwanja wa mpira Chato (Chato Stadium) mradi unaoendelea kujengwa.

5: Chuo Cha Veta Chato, kimeshazinduliwa na Waziri wa China juzi. Wanafunzi wanajazwa hapo muda wowote.

Hiyo ni baadhi ya tu miradi waliyopenda kutuonesha kwa sasa bila shaka kuna miradi midogo midogo mingi inayoendelea ambayo haitangazwi.

Tushauriane kama wa WanaJF na Watanzania kwa ujumla ni fursa gani Mtanzania yeyote anaweza kuipata huko.
 
Umeongea kweli. Japo tunaweza tusifurahie miradi yote kujaa Chato lakini haimaanishi tusijiongeze kufaidika nayo.
 
Kwa sasa Chato inakuzwa na kukua kwa kasi ya ajabu, tunaona miradi mingi ya ujenzi inaanzishwa huko na kuota kama uyoga.

Kama vijana ni hili tuliangalie kwa jicho la fursa badala ya kukaa na kumlaumu Rais na juhudi zake za kuigeuza Chato kama New York.

Miradi mikubwa iliyoko huko kwa Sasa:
1:
Uwanja wa Ndege haujaisha bado unaoendele kujengwa.

2: Hospital kubwa ya Kanda yenye uwezo wa kuhudumia raia zaidi ya milioni 18, kwa maana hii itakuwa Muhimbili ya pili.

3: Kwa ukubwa wa hii Hospitali muda wowote mtasikia ujenzi wa chuo cha Sayansi ya Afya wanafunzi watamwagwa wa kutosha huko.

4: Uwanja wa mpira Chato (Chato Stadium) mradi unaoendelea kujengwa.

5: Chuo Cha Veta Chato, kimeshazinduliwa na Waziri wa China juzi. Wanafunzi wanajazwa hapo muda wowote.

Hiyo ni baadhi ya tu miradi waliyopenda kutuonesha kwa sasa bila shaka kuna miradi midogo midogo mingi inayoendelea ambayo haitangazwi.

Tushauriane kama wa WanaJF na Watanzania kwa ujumla ni fursa gani Mtanzania yeyote anaweza kuipata huko.

Hivi mnapoongelea Chato kama vile inapendelewa uwa mnawaza kuhusu maeneo mengine ambayo pia miradi mikubwa sana imeelekezwa huko pekee mfano Dar es Salaam kuna miradi ya matririoni ngapi hapo na hakuna anayelalama, Rufiji kuna mradi wa tririoni saba na hakuna anayelalama, dodoma kuna miradi ya mabilioni kama sio matririoni kila sehemu hii inchi kwa sasa kuna miradi ya matririoni inaendelea chato haipendelewi ila imecheleweshwa saaaana.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom