Waterbender
JF-Expert Member
- Oct 2, 2018
- 6,813
- 8,659
mods mnamuona huyuNaomba kuwaasa vijana wenzangu tuendelee kuchukua tahadhari, UKIMWI bado upo na ni hatari.
Miezi 4 iliyopita nilifanya ujinga nikalala na mwanamke bila kutumia condom ama bila kumfanyia vipimo vya kiafya kujua hali yake, baada ya ngono tukafanya vipimo na ikagundulika mwenzangu alikua na maambukizi.
Huyo mwanamke nilikua nimefanya nae ngono mara mbili ila kwa time interval ya mwezi mmoja, hii mara ya pili ndio tukafanya vipimo na ikagundulika mwenzangu hakuwa mzima na wakamuanzishia dozi na mimi nikaanza kumeza PEP. Nashukuru baada ya miezi 4 niko salama.
Vijana tuendelee kuchukua tahadhari, Ukimwi ni hatari na unaweza kuzima ndoto zako kwa starehe ya siku ama sekunde chache. Tuendelee kuchukua tahadhari hadi pale chanjo ya Ukimwi itakapopatikana. Nilisikia wakubwa wa Dunia wameazimia kufikia 2030 wawe wametokomeza Ukimwi, ndio unasikia ujio wa chanjo na labda wataleta dawa sio muda mrefu ila for the mean time tuendelee kujilinda.
View attachment 1930729