Vijana Tuchague fungu sahihi, Historia itatuhukumu vibaya

Medicci

JF-Expert Member
Dec 26, 2016
553
915
Leo tarehe 25|04|2018 asubuhi mida ya saa kumi na mbili asubuhi, niliamshwa na milipuko ya risasi na mabomu nikaharuki kidogo lakini nikakumbuka trh 26|04|2018 kutakuwa na maandamo.

1.Nikajiuliza ni kwa nini watumie nguvu nyingi kiasi hiki kututishia side walipa kodi, tuliowanunulia silaha kwa kodi zetu na kuwaajiri kwa kodi zetu pia, tukiwapa jukumu la kutulinda pale tunapotekeleza haki yetu ya kuihoji na kuiuliza serekali yetu? Uhuru wa kupata habari, kutoa habari, kuhoji na kukemea matukio ya watu kupotea.
NB: Uongozi si kuogofya
waliochini yako, Bali dhamana ya kiongozi ni kutoa hamasa chanya kuelekea maendeleo na demokrasia ya kweli.

2. Nikajiuliza tena hivi ni kweli kwamba mtanzania ndio amekuwa adui wa maendeleo.

Nikalazimu kuamini Adui mkubwa tulie nae watanzania kwa sasa ni UBINAFSI na UJINGA na UWOGA. TANZANIANS ENEMY WITHIN.

3. Nikaendelea kujiuliza hivi tungelikuwa wapi kama Wale waliotusaidia kupigania Uhuru...
Kina: 1.Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
2.Bibi Titi Mohammed.
3. Ali Sykes
4. Lameck Makaranga.
5.John Rupia .
6. Na wengine wengi..
Je.? Wangekaa kimya kama wengi wetu vijana Tungekuwa wapi..?

Tuchague upande sahihi wa historia vijana wenzangu.

" I prefer dangerous freedom over peaceful slavery" ~ Thomas Jefferson.

They have guns we have flowers.
Cc mshana Jr
Cc Carol ndossy
Cc Zitto Kabwe
 
Back
Top Bottom