Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe si upo Denmark Mkuu au ulikuja lini Vongo land!!!!!Nyie walugaluga,tuachieni mji wetu. Nendeni au bakini huko mikoani kwenu kwenye maisha mazuri. Kila siku Dar hivi Dar vile. Mikoani kwenyewe kumechoka tu mkiwa humu kila mtu eti mkoani anatengeneza pesa!
Kama unalala pazuri mkuu mshukuru mungu,hii dunia tuAisee kuna watu wanakaa kwenye vijumba vibovu vibovu tu vya mabati na makuti kama vichaa.
Umenifananisha, nipo kwa Mtogole hapa since day oneWewe si upo Denmark Mkuu au ulikuja lini Vongo land!!!!!
Wanajipa moyo hao....Mi nachojua maisha ni popote,halafu kiuchumi ukiona sehemu ina watu wengi jua hata mzunguko wa pesa ni mkubwa...........ingekua kweli mkoani kuna fursa munazoziongea hapa musingepata hata muda wa kuingia jamii forum........
Cha ajabu lundo la watu kila siku wanakimbia huko mikoani wanaingia Dar. Hayo usemayo yangekuwa kweli hii movement ingekuwa kinyume.Tanzania ina watu million 50 milioni 5 wapo hawa 45 wapo mikoani wana maisha mazuri tatizo waliopo dar wana jifanya wana maisha mazuri lakini uhalisi wana maisha magumu wanakula ovyo wana lala ovyo
Sasa huko mwanza kama maisha mzuri, mbona nimeambiwa usafiri mkubwa wa wananchi wa huko ni Baiskeli.umesema kweli kabisa,,kuna mikoa inafursa nyingi za kiuchumi,,,
mfano mkoa wa mwanza ukiishi ulemkoa mpaka ubongo unakua na afya,,nimeshuhudia hilo kwa jamaa nilisoma nae,aliyehama kutoka dar kwenda mwanza..
Wakati yupo dar alikua kama mbwa koko,
Kitu kilichonifanya nichukie ajira ni maisha ya dar. Nilijaribu fikiria kama mfano ningepata ajira dar, mshahara 1m. Pango 200k kwa mwezi, chakula 300,000. Usafiri 300,000 mengneyo 200k. Hiv apo unaweza fanya maendeleo gan au ndyo kusubiri kiinua mgongo?
Nami natamani kusema hili, wengine Dar ndo tunapiga mishe mnoNimebatika kuishi mikoa mitatu mikubwa nje ya dar,hakuna mji wenye mzunguko mzuri wa hela zaidi ya dar...wacha tupambane na dar yetu.
Njoo mjini weweDk 3 zilizopita shost angu wa dar kaniomba nimsaidie chcht..dar kaeni tu kwakwel...kugumu...kuna mikoa hela inakifata mmwyeweee....sitok huku ng'o
Kuna siku niliona rangerover autobiography imebeba majani ya ng'ombe maeneo ya nyakato mwanza,Sasa huko mwanza kama maisha mzuri, mbona nimeambiwa usafiri mkubwa wa wananchi wa huko ni Baiskeli.
Labda shinyanga na tanga mkuu,,ila mwanza ni cardlack,,porche,,ferari,,bugati veron,,lamborghini,,Audi za kumwagirire mpaka basi,Kuna siku niliona rangerover autobiography imebeba majani ya ng'ombe maeneo ya nyakato mwanza,
Wakati Arusha range km hiyo ndo gari ya kutegemewa na matajiri wa Arusha,,
!,,Nasubiri Povu la manjeree,,,
Basi yule mtangazi uwanjani alipotosha, kule misungwi wakati mpira unaenda dakika za mwishoni, watu wakanza kuondoka, akataja maeneo ambayo alihisi watazamaji wale walitokea.
Akasema wanawahi makwao, huku usafiri mkubwa ni baiskeli, hapa kila mtu anaenda kuchukua baiskeli yske alikoficha aende zake.
Leo ninaposikia mwanza ndiko maisha mazuri na shangaa, maana wasukuma mjini hapa na nchi mzima wamezagaa wakitumikishwa mikazi ya mabavu.
Hii ndo point kubwa inayonifanya nitembelee Dar mara kwa mara.dar ninachokipendea wametuzidi kwa kuwa na wanawake wazuri,karibia kila mwanamke unaekutana nae dar ni mzuri unakuta dada jeupe shuzi hilo huku mikoani wanawake zetu wengi wamefubaa sijui huko dar joto lenu huwa linachangia uzuri
Hii nayo point pia.Mimi ushauri wangu ukichanganya mambo ya mkoani pamoja na Dar ndio utatoka kimaisha.Mfano unalima na kufuga mkoani halafu soko linakuwa Dar. Halafu na huko Dar unapitia kariakoo na unabeba bidhaa na kwenda kuuza mkoani.Lakini ukipotelea mkoani mazima unaweza ukaLost, ukaishia kunywa pombe za kienyeji!